Kama wewe unajua imechakachuliwa, lete ya kwako ambayo haijachakachuliwa tuione.
Jenga hoja kwa evidence na siyo mihemko ya kibavicha.
Hizi kelele unazopiga ni kelele za debe tupu. Huoni huyo aliyeleta uwongo kuhusiana na hili swala ameamua kufunga thread yake haraka na kuukimbia uongo wake.
tunaomba nape aweke video yote, kwani shida iko wapi, video itasema yenyewe, hawa wanaodai imechakachuliwa nao wana hoja, kwann video isiwe na mwanza wala mwisho uliona wapi, hii ni hoja ya msingi. ikiwa nape hakutamka hayo ukiweka video yote isiyofanyiwa uhariri itajibu yote wala ww hutahitaji kuja kuanza kuafuta kujitetea
kuhusu CDM kuchangisha hela wananchi sioni kama ni baya, hata ccm ina utaratibu wake wa kupata fedha na baadhi ya mbinu zimekuwa zikilalamikiwa na wapinzani kuwa mna makapuni ynayopewa tenda wakai mwingine bila hata kufuata taratibu kama skakata la mwaka jana, hii kama ipo ni mbaya zaidi kuliko ya CDM. pili kama ulisoma historia rejea mada za luddism movement na Chartism movement, ukisoma mada hizi utafuta kibwagizo chako
kila la kheri wenye vyama mnaovitetea hata pale ambapo inaonekana kuna maosa yamefanyika
NB: Kukosea kwa binadamu ni jambo la kawaida, yy aliye muungwana pale anapokosea hatafuti kujisafisha kwa njia zinazoleta mashaka bali hukiri na kuomba msamaha kuwa ameikosea jamii, mtu anayetubu makosa yake ndiye huibuka kuwa shujaa katika jamii, ikiwa hatuna tabia ya hivo sio rahisi kufanikiwa katika maisha yetu. Hii haina tofauti na mtu kumkamata mke/mke anazini nje ya ndoa halafu anaaanza kusema ulinifananisha haikuwa mm, hv utajisikiaje?
Nape alishatoa kauli nyingi za kebehi ambazo zingine zilirushwa na vyombo vya habari wananchi wakazisikia na zilihusu wazee hao hao, je hizo nazo mnasemaje?
kumbukeni msitukane wakunga uzazi ungalipo