...Mwisho wa UONGO ni AIBU!

...Mwisho wa UONGO ni AIBU!

Mods, kama kweli tuna hakikishiwa kuwa JF sio mahali pa mtu kuleta uongo wake na kuendelea kudunda tu humu jukwaani, ningependa huyu mtu anaeitwa Ben Saanane awajibishwa kwa kuleta taarifa ya uongo humu jamvini.

cc: Paw, Buchanan, Moderator

Wewe acha kulialia hii habari chanzo chake si Ben Saanane bali ni magazeti zaidi ya matatu na kwanini video aijaanzia mwanzo? Yani kwa nini Nape Nnauye asiweke video yote ya uliyo ongea siku hile kuhusu wazee bali ameweka anapo papenda yeye? Kwanini tusiamini alipo pakata ndipo alipo watukana wazee wetu wakina MAKAMBA,LOWASA,MAMGULA,MALECELA,SITTA,MAKINDA NA WENGINE.

hivi magazeti yote yanamZUSHIA NAPE
 
Last edited by a moderator:
Kamanda ben saa8 ni nouma.mkuu hiyo inaitwa twanga kote kote! Mwaka huu magamba yatakoma.
Mimi kinacho ni shangaza zaidi hawa wazee ndio wamemsaidia nape kwa ushauri lakini kumbe yeye anataka wafe.

Nape Nnauye tafadhali weka clip yote pale ulipo kata ndio tunapataka kusikia maanà sioni sababu ya kuleta vitu nusu kama unataka wazee wetu wakina Makamba,MAMGULA wakuelewe.

Nape Nnauye ni bora uwambie kabisa ccm hamtaki wazee kuliko kuwaombea dua kama hizi,kama wewe huwapendi sisi tunawapenda na tunataka waendelee kuishi,kufa kwao yawe mapenzi ya muumba lakini si ya kwako.
Aiseee hivi wazee wetu huwa wanatumia pumzi yako Nape Nnauye?
 
Last edited by a moderator:
Kwa Ben Saanane, Mawio na wote wanaowatuma, MSISAHAU MWISHO WA UONGO AIBU!

Huu ndio ukweli wa nilichosema juu ya wazee. Sasa pimeni wenyewe aibu ya nani kwa uzushi wenu! Si kila unacholishwa unabeba!


Nape Nnauye acha kufanya siasa za ujanja ujanja, Toka utuhumiwe kutoa hiyo Kauli ni karibia wiki mbili na zaidi zimepita hii clip yako ulikuwa umeificha wapi, au ilikuwa stuido?
 
Last edited by a moderator:
Babu aliwaambia bila utafiti Huna haki ya kusema lakini wasomi hawa hawakumbuki hayo
 
Kwa Ben Saanane, Mawio na wote wanaowatuma, MSISAHAU MWISHO WA UONGO AIBU!

Huu ndio ukweli wa nilichosema juu ya wazee. Sasa pimeni wenyewe aibu ya nani kwa uzushi wenu! Si kila unacholishwa unabeba!


Nape Nnauye,

Hongera kwa kutoka hadharani na nina imani kuwa leo utakua na ujasiri wa kukaa hapa na kujibu hoja zaidi ya kukimbia na pengine ukaingia na silaha za msituni(ID fake)

Hoja yangu nilianza kuijengea juuu ya msingi wa kilichoripotiwa na vyombo vya habari na pia baada ya kuona Tweets malalamiko mengi ya wazee dhidi ya kauli hiyo zikiwamo Tweets za Mzee Reginald Mengi.

Nadhani hizi tuhuma za 'Mwisho wa UONGO NI AIBU' zinafaa kukurudia maana ungekua mkweli ungeweka video yote.Je kuweka video ya Youtube hapa inatosha?Ni kitu gani kitakachothibitisha kuwa hii video haijawa Edited na kuondolewa vipande ambavyo ni awkward ikiwemo hiyo kauli 'Wazee wanaosubiri kufa Kesho'?Tangu tuhuma hizi zilipoibuka ni siku nyingi zimepita sasa hiyo video ulikua ukiifanyia nini?

Kama ulisoma post yangu vizuri uliona kwamba nilianza kuamini kilichoripotiwa kutokana na rekodi ya matamshi yako ya kibaguzi na mengine ya kukurupuka.Historia ndiyo inayokuhukumu.Rekodi zako ndizo zinazokuhukumu.

Hapa hapa umekurupuka na kudai tunatumwa bila uthibitisho wowote.Nadhani sasa title ya hii thread yako inakufaa maana unasema uongo hadharani bila kujali nafasi yako katika jamii.Hii inathibitisha ulaghai katika mambo unayofanya na hata hii video itakua na chembe za ulaghai kama vile kufanyiwa 'Editing' maana kama katika post hii tu umedanganya,ni mangapi utakua umedanganya?Post yangu ya jana ilikua hivi



''Nimesikitishwa sana na kauli iliyonukuliwa kutolewa na Nape Nnauye(Katibu wa itikadi na Uenezi wa CCM).


Gazeti la MAWIO la tarehe 8/8/2013 toleo namba 055 ukurasa wa 5 lililikua na kichwa cha habari NAPE NA CCM 'Ni ama Aiue Ama Imuue'

Katika kauli zake nyingi zilizokosa umakini Kwanza kama mwanasiasa Kijana(Namaanisha Muonekano yaani Physical appearance bila kujali weledi wa kifikra) na Pia kama Mwanasiasa msomi mwenye Taaluma ya diplomasia,Taaluma ya Uandishi wa Habari(Kutoka Chuo kikuu cha Acharya maana Syllabus yao naifahamu na ilihusisha somo la saikolojia) na pia kama msomi wa shahada ya uzamili aliyemudu kuandika Tasnifu(Thesis) na ikapitishwa na Maprofesa hakupaswa kutoa kauli hizo ikiwemo kauli hii iliyokera sana, kwamba Wajumbe wa Tume ya Katiba wanaounga mkono serikali 3 ni wazee na wanasubiri kufa.

Hii ni kauli ya kipuuzi kabisa na inadhalilisha taaluma zote nilizotaja hapo juu na weledi anaopaswa kuwa nao.Kauli hii haidhalilishi taaluma tu,bali hata Mwenyekiti wake aambaye ametimiza miaka zaidi ya 60.Kauli hii inawadhalilisha viongozi na wanachama wote wa chama chake na serikali waliovuka umri wa ujana kwa mujibu wa sheria zinazotambulika na vigezo vyote vya kinadharia.Zaidi Kauli hii inatudhalilisha vijana maana hata sisi ipo siku tutakuja kuwa wazee.Sasa kauli hii inaweza kutumika dhidi yetu kwamba tukipewa mamlaka tunaweza kuharibu kama waliopewa ridhaa na vyama vyao bila kujali itikadi wanaweza kuwa na mtazamo wa aina hii.Ni kauli mbaya na ya kibaguzi

Kumbe Kauli ya Kumuita Dr.Slaa Babu ,Haikumaanisha kauli ya kipinzani?Nakumbuka Dr.Slaa aliwaambia Wanachama wa CHASO(Taasisi ya wanafunzi wa vyuo vikuu ambao ni Wafuasi wa CHADEMA) kuwa akiitwa Babu ni heshima kubwa kwake maana uzee unaashiria hekima na busara.Lakini sasa kauli za Nape kumbe zililenga ubaguzi dhidi ya wazee na sio kwa nia njema.Kumbe Nape nnauye anapomtazama Mwenyekiti wake,Katibu mkuu wake,Makamu mwenyekiti wake,waziri mkuu,Makamu Wa Rais,Spika Wa bunge anaona kwamba hao wote wanasubiri kufa?Anawaona wazee Salim Ahmed Salim,Mzee Waryoba na Mzee Lowassa kwa jicho hilolo hilo mana suala hapa sasa limekua umri aidha unaunga mkono serikali 2 au unapinga.Ni jambo la ajabu kuwa Nape alituhumiwa kushiriki kuasisi CCJ,huku akijua washirika wenzake waliotajwa yaani Mzee Samweli Sitta ni mzee na hivyo anasubiri Kufa pengine yeye akifikiria kuwa atakua na fursa muhimu ya ku-takeover chama cha CCJ?Yaani Mwenzako anawaza huyu nipo nae leo lakini "Anasubiri kufa Kesho"?Unafiki huu haufai hata kidogo.

Kauli hii ni ya kulaaniwa na vijana wote bila kujali itikadi zetu za kidini na kisiasa.Mwanzoni niliposikia kauli hii niliona tweets za Mzee Reginald Mengi akitoa ushauri wa busara kwa Nape na kumuonya kuwa ‘Yeye(Nape) Sio Mungu'.Mlolongo wa kauli za kukurupuka ulioanishwa leo hasa ule wa kuwapa mafisadi siku 90 za kujivua Gamba,kauli hii dhidi ya wazee nami naongeza/nakumbushia Kauli ile nyingine ya kuwa 'Wachagga sio watu wa kujichanganya nao'(akilenga rhetorics za Ubaguzi dhidi ya CHADEMA ) bila kujali kuwa ndani ya CCM kuna viongozi na pia serikali ya chama chake ina Mawaziri ambao wana asili ya uchagani na ama wameoa au kuolewa na wachagga ni ulimbukeni.

Kijana yeyote katika jamii iliyostaarabika mwenye ujasiri wa kuwatukana wazazi na hata wakwe zake kwamba 'Ni wazee wanaosubiri kufa' anazua maswali mengi.


Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM anapotangaza maneno hayo inamaanisha kuwa anaeneza sera za chama chake kilichounda serikali inayoshindwa kuwalipa wazee wa Afrika Mashariki kwa sababu tu ya dhana na fikra potofu kuwa ni 'Wazee wanaosubiri Kufa Kesho'
? Bila shaka kama sio msimamo wa chama chake basi Madaraka aliyopewa ni makubwa sana kwake

Wazee ni tunu inayopaswa kuheshimika.Kupitia Itikadi zetu tujifunze kushinikiza kupitia ujana wetu kuhakikisha vyama vyetu vinatunga sera zinazoheshimu wazee.Kwa kufanya hivi tutakua tumejenga utamaduni na misingi inayoheshimu wazee
Nape Nnauye atoke hadharani sasa kueleza alichomaanisha kuhusu kauli hii na hayo mengine yaliyonukuliwa.Asipofanya hivi,vijana tumuhesabu kama msaliti wa vijana na tujitenge na kauli hii aliyoitoa.Kama kweli alisema,Labda pengine msimamo huu ni wa chama chake ambacho naamini kuwa vijana wanaoheshimu wazee hawataiunga mkono.

Msomi Mzuri ni Yule anayechagua cha kuongea,Mwanasiasa mzuri ni Yule anayechagua maneno.Kijana mzuri na makini ni Yule anayeheshimu tunu za uzee bila kushinikizwa na itikadi au mazingira yoyote.Binadamu mzuri ni Yule anayeheshimu uhai wa mwenzake.Binadamu mstaarabu ni Yule anayeheshimu mamlaka ya kiroho na pia anayeheshimu katika falsafa ya ‘Law of Nature'.''



CC: Paw , PainKiller , Fang , bachanan
 
Last edited by a moderator:
Ni kweli Nape Nnauye hata wewe vua Gamba ilikuaibisha na sijui hatima yako Lowassa akiingia
 
WanaJF

Nimecheka sana leo baada ya kuona hii video iliyokatwakatwa.Namshauri bwana Nape alete Video yote mwanzo hadi mwisho.

Nape hana pa kutokea kwa sababu tulisikia matusi yake kwa wazee kwamba wanasubiri kufa na hapa alikuwa anawalenga kina Mzee Warioba,Joseph Butiku na Salim Salim.
 
Wamekurupuka kama alivyokurupuka Ben Saanane, haya walete na wao video, Nape kaleta ushahidi kamili kuwa waliosema ni waongo, si maneno yake hayo.

Umewashuka shuu.
Ushahidi kamili ni upi ikiwa hawezi kututhibitishia kuwa video haijawa edited?
 
Kwa Ben Saanane, Mawio na wote wanaowatuma, MSISAHAU MWISHO WA UONGO AIBU!

Huu ndio ukweli wa nilichosema juu ya wazee. Sasa pimeni wenyewe aibu ya nani kwa uzushi wenu! Si kila unacholishwa unabeba!





Ha Nape kiongozi mkubwa wa Chama it seems that unatumia sembe kama si sana basi kwa kiwango fulani kwani unayosema na unayoyafanya hauna tofauti na wale wanaobembea baada ya kutumia sembe

Kwa hiyo clip uliyoweka haiwezi kuufuta ukweli wa maneno uliyowaambia wazee kana kwamba wewe hauna wazee huko kwenu eti wanakaribia kufa kwa kutaka serikali 3 wewe hautazeeka?

Ni aibu kwa chama kuwa na kiongozi anayeongea bila kupima kinachotoka mdomoni kwake kitakuwa na madhara gani kwa wanaomsikiliza na akishalaumiwa anakuwa wa kwanza kukana kwamba sikusema mara nimelishwa maneno ni jinsi gani usivyo makini na ulipewa kimakosa huo uongozi hata aliyekuteua unamshushia hadhi kwamba alikuteua wakti hauna uwezo wa uongozi i mean DEBE TUPU

Kwa kiongozi kama mfano lazima upime kinachotoka mdomoni kwako kinamkwaza nani na kinamfurahisha nani pia,uongozi sio kupayuka na kuwa kama MC litakalokuja mdomoni ndilo unalolisema,lazima ulipime kwanza kabla ya kulisema

Kwa elimu yako unafikiri kwa kuweka hiyo clip utafuta utovu wa nidhamu kwa wazee na kauli uliyoitoa dhidi yao? You are fooling yourself
 
Last edited by a moderator:
Nape Nnauye acha kufanya siasa za ujanja ujanja, Toka utuhumiwe kutoa hiyo Kauli ni karibia wiki mbili na zaidi zimepita hii clip yako ulikuwa umeificha wapi, au ilikuwa stuido?

Alienda kushona gwanda, yaani kila jambo full kuiga. Wanahangaika hao na urais 2013 huku kila gamba na kambi yake.
 
Last edited by a moderator:
Mods, kama kweli tuna hakikishiwa kuwa JF sio mahali pa mtu kuleta uongo wake na kuendelea kudunda tu humu jukwaani, ningependa huyu mtu anaeitwa Ben Saanane awajibishwa kwa kuleta taarifa ya uongo humu jamvini.

cc: Paw, Buchanan, Moderator

Nadhani Nape Nnauye anatakiwa kuchukuliwa hatua za kinidhamu kwa kudai tunatumiwa/tunatumwa bila kuja na uthibitisho wowote.Pia kama mnataka hilo litimie Mwambie Nape alete video ambayo imethibitishwa kuwa ni original maana video hii haionyeshi alipoanzia wala alipoishia.Je hiyo video haijawa edited na kukatwa baadhi ya vipande?If you come,come correctly otherwise don't come at all!
 
Last edited by a moderator:
Wamekurupuka kama alivyokurupuka Ben Saanane, haya walete na wao video, Nape kaleta ushahidi kamili kuwa waliosema ni waongo, si maneno yake hayo.

Umewashuka shuu.



Hivi we nae umetokea pori gani make haueleweki ni binadamu au mnyama,haujulikani unachangia nini au ni nini msimamo wako,kwamba unatetea alichokisema Nape au ni nini

Mzee Mengi umeona tweet yake hapo akilaumu alichokiongea Nape wewe unasema Ben anakurupuka,sishangai ni kawaida yenu kujipendekeza ili muweze kupata posho na bia muendelee kuishi mjini kwa migongo ya watu kwa hiyo hata akiandika au akisema tusi mtamtetea make ni waganga njaa tu

Unaleta mambo ya kike ya kijinga watu wanaongea na kujadili mambo ya maana unaleta mambo ya Josephina kwenye kauli alizozitoa Nape ni wapi alimgusia Josephina?

Hawa wadudu aina ya huyu mbweha ni kukaa jikoni hawana lolote vichwa panzi tu kazi yao kuzaa,kupika na kuwalaza wanaume unono akili hamna kabisa
Hebu usituletee habari za kike hapa kaongee na wanawake wenzio huko hili jukwaa halikufai kwa akili yako hiyo idiot

Video unayoisapoti unauhakika nayo? Kwa hiyo Mengi anaugomvi na Nape hadi amzulie kwenye hiyo Tweet?

Utajuaje hiyo clip ni genuine haikuchakachuliwa? Unaelewa nini kwenye hilo?

FaizaFoxy inaonekana hata wewe kwenu hauna wazazi wewe kama unasapoti upumbavu,hebu kabla haujaandika kitu elewa kwanza unachokiandika acha KUKURUPUKA
 
Last edited by a moderator:
Ingekua jambo la maana kama ulitaka kuprove a point ungeweka clip nzima tangu umeanza kuongea mpaka mwisho. You tube haina shida na mda wa clip. Hata ingekua masaa 3. Tatizo umeweka kile ulichodhani kina prove your point basi. Yale madubwasha mengine uliyoongea umeamua kuyakata.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Babu aliwaambia bila utafiti Huna haki ya kusema lakini wasomi hawa hawakumbuki hayo

Hivi kwa nini nape ametuwekea video nusu? Na haijaanza mwanzo? Hivi kwanini @nape awachukie wazee wetu kiasi cha kuwapangia siku za kufa? Kwanini Nape Nnauye unafanya hivyo? Ina maana kumbe ndio maana hata mafao yao mnayachelewesha ili wafe? Nape Nnauye una hitaji kutoka hadharani na kuwaomba msamaha wazee wetu. Najua wazee wetu wakina MANGULA
,MALECELA,MAKAMBA,SITTA WAMENYIMWA RAHA YA KUISHI NA HII KAULI. INA SIKITISHA SANA.
 
Last edited by a moderator:
Siasa za kizee karne ya 21! Eti huyu na Mwigulu ndio vijana tegemezi wa CCM!
The two of you lack the finesse of convincing let alone leading the increasingly well informed youth of Tanzania.
Tafuteni kazi za kufanya after 2015.
 
Back
Top Bottom