...Mwisho wa UONGO ni AIBU!

...Mwisho wa UONGO ni AIBU!

Nape Nnauye kuna njia moja rahisi kabisa ya kujitoa hili fupa kooni. Njia yenyewe haigharimu muda au pesa nyingi kuliko zinazotumika katika kupanga upya, kuandaa na kueneza propaganda ambazo jinsi zinavyofanywa na mtu wa upeo wa kadri na kumbukumbu ndogo zinazidi kumbomoa badala ya kumsafisha. Njia yenyewe ni hii:

Kama wewe mwenyewe wahiamini hii clip kwamba ni "bona fide genuine" katika sakata lako, na kweli umesingiziwa hukusema, basi yashitaki magazeti yote yaliyopotosha matamshi yako. Mshtaki pia Mzee Mengi aliye tweet kuuonyesha upumbafu uliokithiri katika yale matamshi.

Usipofanya hivyo, haya mengine yote unayofanya ni mbwembwe tu na propaganda za mtaani
Naamini Nape kalala ataukuta ushauri wako, but nina link ya gazeti la Mtanzania mnaloli reffer hapa likiomba radhi kwa kumnukuu vibaya Nape. Sasa kwa kuwa Bavicha majanga hilo hamkuliona. Nalo mtadai imechakachuliwa
 
Naamini Nape kalala ataukuta ushauri wako, but nina link ya gazeti la Mtanzania mnaloli reffer hapa likiomba radhi kwa kumnukuu vibaya Nape. Sasa kwa kuwa Bavicha majanga hilo hamkuliona. Nalo mtadai imechakachuliwa

uko Night shift leo? vp una thread ya Dr.Slaa
 
uko Night shift leo? vp una thread ya Dr.Slaa

Kwangu hapa saa 18:47 kama kwako huko usiku pole sana waambie wakuongezee posho kidogo upunguze machungu. Bavicha majanga
 
hivi whats a point mtu kuanzisha thread na Id Moja,halafu kuanza kuitetea na id nyingine.!
Labda na wewe sema atakuelewa. Mwenzio nimemwambia katika jinsi ya kumkonyeza ili astuke kwamba kalog-in na ACHEBE ambayo niID ya shift ya usiku na watu wanaifahamu kitambo!
Kwa hiyo wabisha juu ya unasaba na umiliki wa PenIDs hizi ACHEBE, Honey K (Nnauye Jr), Nape Nnauye? Wataka tuanze kufunua? Crashwise naomba ushauri!......umesahau kwamba umelog-in kwa kutumia ACHEBE?...
 
Nape nilitegemea wewe kama Kiongozi utajutia kauli ulizotoa. Waliokuwekea kauli zako wamesahau hii ya siku za hivi karibuni uliyosema wenye akili timamu ni wale wanaosimamia msimamo wa serikali mbili, ikiwa na maana kuwa wasio waumini wa msimamo huo hawana akili timamu.

Rasimu ya Katiba imeletwa tujadili wote kwa kuheshimu uhuru wa mawazo. Wewe unasema sisi tusiounga mkono hoja za CCM hatuna akili timamu. Nilitegemea hili unalielewa hata baada ya kujadiliwa na vyombo vya habari na mitandao, kukomaa kwako kwa jambo hili sikuungi mkono.

Kila tamko lina gharama, lakini sisi tunakuambia kwenye mitandao tu. Subiri wazee kama watakuelewa au watanzania wengine watakaotafsiri kauli zako.

Nape kasema hivi "Huu ndio ukweli wa nilichosema juu ya wazee. Sasa pimeni wenyewe aibu ya nani kwa uzushi wenu! Si kila unacholishwa unabeba!" na ushahidi kauweka hapo juu. Sasa wewe unakuja na mambo mengine ya ajabu. Hivi unazo kweli?
 
Wacha tuweke mkusanyiko wa makanusho ya maneno ya Nape ili ajue historia imemuhifadhi kama mtu wa aina gani. Pia itamsaidia kujipima na kuamua mwenyewe kama ni mtu anaaminika na jamii katika kusimamia matamshi yake. Binafsi nimekuwa nikimpongeza katika lile la kuwa miongoni mwa watu wachache waliomwambia Lowassa kwa macho makavu kwamba yeye ni fisadi na wakaendelea kusisitiza hivyo. Lakini katika mengine yote ni mtu wa ndimi mbili!
n1.JPG


Nape Mnauye wakati akiongea na vyombo vya habari mjini Dodoma leo ambako vikao vya Chama cha CCM vikiendelea amebadilisha kuali mbiu ya awali aliyokuwa akizunguka nchi nzima kutangaza majina ya wanaotakiwa kuachia ngazi . Leo kaja na mpya kwamba vyombo vya habari vilipotosha ukweli wa maana ya kuvua magamba kwa maana ya kubadilika na wala si kuwafukuza watu. Hii imekaaje?

Waliopinga kwamba Nape hakuongea hayo, hapa ni ushahidi zaidi kutoka gazeti la Habari leo, pamoja na kuchakachua habari lakini ukweli umebaki kama mada hii ilivyo

GAZETI LA HABARI LEO LIMEANDIKA HABARI HII KAMA IFUATAVYO


Kichwa cha habari: Kujivua gamba si Lowassa, Chenge, Rostam pekee

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimewataka wanachama wake na wananchi kuondoa wasiwasi kuhusu vikao vyake vya juu vinavyofanyika Dodoma.

Chama hicho kimesisitiza kuwa, dhana ya ‘kujivua gamba' ambayo inaendelea, haihusu watu watatu tu, ni pana, iliyosheheni mageuzi kuanzia chini hadi juu.

Chama hicho mbali na kukiri kuwa vikao hivyo vilivyoanza Jumamosi na kutarajiwa kumalizika Alhamisi vimesababisha hisia kali kwa wanachama, kimeonya kuwa hakitavumilia upotoshwaji wa habari kuwa ‘kujivua gamba' kunahusu watu watatu, wakati kuna mengi zaidi ya hilo.

Akizungumza jana na waandishi wa habari katika ofisi za makao makuu ya CCM mjini hapa,
Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC) ya CCM, Nape Nnauye,alisema habari zinazotolewa zimekuwa zikipotosha kuwa vikao hivyo vinashughulikia watu watatu kwa maslahi aliyosema hajui ni ya nani.

Mpaka sasa watu wanaolengwa na habari hizo kuwa 'watavuliwa gamba' alizosema zinapotoshwa, ni Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa, Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge na aliyekuwa Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz.
 
Lonesome,
Bila kuathiri majibu ya Nape akiamua kuja kujibu lakini, hivi mwanaume mwenye mtoto mwenye watoto naye anaitwaje kama sio Babu?!! Dr. Slaa ana watoto wenye watoto nao, kama sio babu tumwite bibi? Linageukaje kuwa tusi hili???!

JK ana wajukuu kamavtu alivyo Dr Slaa!Mtaanza kumuita babu lini?
 
..hivi mwanaume mwenye mtoto mwenye watoto naye anaitwaje kama sio Babu?!! Dr. Slaa ana watoto wenye watoto nao, kama sio babu tumwite bibi? Linageukaje kuwa tusi hili???!
JK ana wajukuu kama tu alivyo Dr Slaa! Mtaanza kumuita babu lini?
22.jpg

Rais Kikwete akimlisha Keki mmoja wa wajukuu zake katika moja ya hafla za sherehe yake ya kuzaliwa
kikwete.jpg

Mwenyekiti wa UDP Mh.John Momose Cheyo, Katikati ya Rais na Mama Salma ni Mjukuu wa Mheshimiwa Cheyo anayejulikana kama Gabriel Cheyo. (Picha Freddy Maro)​

Kwa hiyo kama siyo kebehi, jina Babu likitumika kwa tafsiri na maana aliyotoa ACHEBE-Nape, katika nchi hii basi tutakuwa nao viongozi wengi wa kuitwa "Babu" zaidi ya Dr.W.Slaa
 
Last edited by a moderator:
Umefanyia usaili vidio hii. Ile halisi anayo mzee mengi ambaye ali tweet muda mfupi baada ya kuongea utumbo wako.
 
Kwa Ben Saanane, Mawio na wote wanaowatuma, MSISAHAU MWISHO WA UONGO AIBU!

Huu ndio ukweli wa nilichosema juu ya wazee. Sasa pimeni wenyewe aibu ya nani kwa uzushi wenu! Si kila unacholishwa unabeba!



Kaka, message ilishakuwa sent na delivery report wazee wanayo!!
 
Last edited by a moderator:
Kaka, message ilishakuwa sent na delivery report wazee wanayo!!

"Wazee hawa wanaosubiri kufa wanataka kutuletea matabaka, vijana ndio nguvu kazi ya taifa, kitendo cha kuwepo kwa serikali tatu ni kusababisha mgogoro, kwa nini wasingevunja Muungano enzi za ujana wao? Wamenufaika na Muungano kwa kipindi cha miaka 50, sisi vijana wanataka kutuachia mgogoro!"alisema Nnauye.

Source: Mwananchi
Na baadhi yao hawakuunyamazia huo upuuzi:
attachment.php

 
  • Thanks
Reactions: ral
Lukolo Kama kawaida yako, so much hot air ambazo ni
debe tupu.

Hoja yako hapa ni nini?. Video ni fake or timing.

Hao walioleta habari ya uongo walikupa na video kama ushahidi?. Kama hawakukupa video, kwa nini unaona tatizo kwa Nape kuifuta habari yao ya kuchonga bila kuweka ushahidi wa video. Hakuishia hapo baada ya kubaini kina Tomaso wa kwenye Biblia ni wengi, basi akaamua kuleta video lakini siyo cha kushangaza kama bavicha watadai video ni fake kwa sababu hata ukiwambia tazama, hawawezi kuona.
 
Na hawa nguzo yao ni ipi!?




Hawa ambao CHADEMA inawapa viroba kabla ya kwenda kwenye mikutano ili waweze kuwadanganya kwa urahisi kama ilivyo sera yao ya uwongo na uzandiki kwa sababu akili inakuwa imeishakuwa intoxicated and poisonous.

attachment.php
 

Attachments

  • image.jpg
    image.jpg
    187.6 KB · Views: 393
Wewe topic zako itakua hatuzijibu siku zijazo kwa sababu hujibu maswali yetu ya msingi

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom