Nape kadhihirisha uongo wake Dodoma leo

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,883
6,883
n1.JPG


Nape Mnauye wakati akiongea na vyombo vya habari mjini Dodoma leo ambako vikao vya Chama cha CCM vikiendelea amebadilisha kuali mbiu ya awali aliyokuwa akizunguka nchi nzima kutangaza majina ya wanaotakiwa kuachia ngazi . Leo kaja na mpya kwamba vyombo vya habari vilipotosha ukweli wa maana ya kuvua magamba kwa maana ya kubadilika na wala si kuwafukuza watu. Hii imekaaje?

Waliopinga kwamba Nape hakuongea hayo, hapa ni ushahidi zaidi kutoka gazeti la Habari leo, pamoja na kuchakachua habari lakini ukweli umebaki kama mada hii ilivyo

GAZETI LA HABARI LEO LIMEANDIKA HABARI HII KAMA IFUATAVYO


Kichwa cha habari: Kujivua gamba si Lowassa, Chenge, Rostam pekee

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimewataka wanachama wake na wananchi kuondoa wasiwasi kuhusu vikao vyake vya juu vinavyofanyika Dodoma.

Chama hicho kimesisitiza kuwa, dhana ya ‘kujivua gamba' ambayo inaendelea, haihusu watu watatu tu, ni pana, iliyosheheni mageuzi kuanzia chini hadi juu.

Chama hicho mbali na kukiri kuwa vikao hivyo vilivyoanza Jumamosi na kutarajiwa kumalizika Alhamisi vimesababisha hisia kali kwa wanachama, kimeonya kuwa hakitavumilia upotoshwaji wa habari kuwa ‘kujivua gamba' kunahusu watu watatu, wakati kuna mengi zaidi ya hilo.

Akizungumza jana na waandishi wa habari katika ofisi za makao makuu ya CCM mjini hapa,
Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC) ya CCM, Nape Nnauye,alisema habari zinazotolewa zimekuwa zikipotosha kuwa vikao hivyo vinashughulikia watu watatu kwa maslahi aliyosema hajui ni ya nani.

Mpaka sasa watu wanaolengwa na habari hizo kuwa 'watavuliwa gamba' alizosema zinapotoshwa, ni Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa, Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge na aliyekuwa Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz.
 
alishakana ID yake humu itakua hayo! tumemzoea bana! siasa ni kwa wanaojua kucheza!
 
n1.JPG


Nape Mnauye wakati akiongea na vyombo vya habari mjini Dodoma leo ambako vikao vya Chama cha CCM vikiendelea amebadilisha kuali mbiu ya awali aliyokuwa akizunguka nchi nzima kutangaza majina ya wanaotakiwa kuachia ngazi . Leo kaja na mpya kwamba vyombo vya habari vilipotosha ukweli wa maana ya kuvua magamba kwa maana ya kubadilika na wala si kuwafukuza watu. Hii imekaaje?
sasa unacho shangaa ni nini? Mbona hata hapa jamvini alisha likana jina lake...
 
Mie huwa nafikiri labda hizi cream ukitumia kwa muda zina madhara. Huenda system ya kumbukumbu zake zimeathirika au amegundua alipokua anachezea ni hatari kuliko alivyojiingiza bila kujua.
 
Toka siku ile, aliposema eti itikadi ya CCM ni ujamaa na kujitegemea na bado wanavisamamia hvyo, nkamkubali Mwalimu Nyerere kuwa kweli lazima uwe na moyo wa mwendawazimu!
 
Amegundua ataadhirika kwa sababu hakuna hata mmoja atakaye jivua gamba. Hiyo ndio CCM na hao ndio viongozi wao.

Sisi tumewazoea hawa CCM wanapenda sana kula matapishi yao. Hawawezi kusimamia kile wanachokiamini. Aibuuuuuuuu
 
kasalimu amri,Lowassa for 2015 apende asipende.:A S 465::juggle::smash::photo::shock::eyebrows::canada::A S-coffee::nerd::rant::director::ballchain::washing::hatari::photo::shock:
 
Siamini aisee anaweza kusema hivyo! Hapana............, nadhani mkuu umesikia vibaya tu, da!
 
nape na ujanja wote huu unatumia ipad 1??????? aaaaaaaamimi nilijua wewe ni mjanja kumbe hakuna kitu.
watu siku hizi wanakula bata na ipad 2 +3G
 
oooh mndio nilijua tu itakua hivyo, kwa hio wale aliowataja kwa majina walikua akina na nani na wa nini??
 
Hivi hawa wanasiasa huwa wanatufanya sisi mazezeta sana? Huko kupayuka kote kwenye majukwaa leo anasubuthu kukana. Tusije kushangaa kusikia JK akikana kuwa hakutamka kuwa "watu wanaoishi kwenye nyumba za makuti wanaishi kwa kupenda kwao".
 
Huyu mbona ndiyo zake kamkana baba yake mzazi, ameshindwa hata kwenda kumjulia hali huko Apollo India, ashindwe kukana kauli aliyoisema mwenyewe? Mimi nawashauri wale aliowataja majina wamshitaki huyu mbwiga.
 
Back
Top Bottom