Reginald Mengi on Nape: Muache Mungu afanye Kazi Yake

Reginald Mengi on Nape: Muache Mungu afanye Kazi Yake

Kitwange

Member
Joined
Apr 10, 2011
Posts
47
Reaction score
48
Mzee Reginald Mengi ame tweet mawazo yake juu ya Kauli ya Nape Nnauye ambae inadaiwa kasema waliopendekeza Serikali tatu ni wazee wanaosubiri kufa.

View attachment 104489
---------------------------
Habari Kamili
---------------------------


NAPE: Waliopendekeza Serikali tatu ni Wazee wanaosubiri kufa​

MZIMU wa serikali tatu bado unaendelea kukitesa Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambapo jana, Katibu Mkuu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, alipinga tena uwepo wa serikali tatu na kudai kuwa waliotoa maoni hayo ni wazee wanaosubiri kufa. Akizungumza jijini Dar es Salaam katika kongamano la Umoja wa Vijana (UVCCM) la kujadili mchakato wa Katiba Mpya, katika ukumbi wa Arnatouglo, Nnauye alisema nia ya serikali tatu ni kuleta matabaka ambayo yatasababisha migogoro.

"Wazee hawa wanaosubiri kufa wanataka kutuletea matabaka, vijana ndio nguvu kazi ya taifa, kitendo cha kuwepo kwa serikali tatu ni kusababisha mgogoro, kwa nini wasingevunja Muungano enzi za ujana wao? Wamenufaika na Muungano kwa kipindi cha miaka 50, sisi vijana wanataka kutuachia mgogoro!"alisema Nnauye.

Nape alisema kuvunjwa kwa Muungano kutasababisha mgogoro mkubwa wa rasimu kutokana na muda ambao Muungano huo umedumu.

Alisema kuundwa kwa serikali tatu si sera ya CCM kama wanavyodai wapinzani, bali ni maoni ya watu waliyoyawasilisha katika ukusanywaji wa maoni ya Rasimu ya Katiba mpya.

"Sera ya CCM ni kuongoza serikali mbili na si tatu, na hii sera tutaendelea kuitetea na kuilinda mpaka mwisho wa dunia, tunachoamini katika chama chetu hatuogopi kutetea sera ambazo tumezitoa wenyewe," alisema Nnauye.

Alisema ni vyema zikamalizwa kasoro zilipo katika mfumo wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano na si kuongeza madaraka yasiyo na tija.

Nape alisema kitendo cha Tume ya Jaji Joseph Warioba kusema imetumia sheria ya mwaka 1964 kuwa kigezo cha kuundwa kwa serikali tatu si sahihi, kutokana na makubaliano ya mwaka huo kwamba ni serikali mbili.

Kiongozi huyo wa CCM pia alishangazwa na kitendo cha Rasimu ya Katiba mpya kutamka wazi idadi ya mikoa pamoja na wilaya ambazo zitatumika katika uchaguzi na kwamba mwenye jukumu hilo ni Rais Jakaya Kikwete na Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein.

"Serikali ya Muungano chini ya mfumo wa serikali tatu itaelea katika madaraka, kwani serikali ya Tanganyika itakuwa haiwezi kuwatetea wananchi, hali itakayosababisha kuwepo kwa mgogoro mkubwa wa urasimu ambao ni adui wa maendeleo," alisema Nnauye.

Aidha alisema kuwa kuvunjika kwa Muungano kutasababisha kuiburuza Serikali ya Zanzibar kiuchumi, kwani asilimia 95 ya uchumi wa visiwani unategemea Tanzania Bara.

Alisema kuwa sera nzuri ya kuwa kiongozi ni kuwatetea wananchi na si kuwazidishia mizigo.

Akizungumzia suala la mgombea binafsi, Nnauye alisema CCM hakiogopi mgombea binafsi, kwani hata akigombea chama hakitapata hasara yoyote.

Nape alisema sera ya CCM ni kukataa wagombea binafsi wanaouza unga na si kukataa mgombea binafsi kama ambavyo vyama vingine vya siasa vinavyodai katika vyombo vya habari.

Alisema katika Rasimu hiyo sura ya 9 inazungumzia umri wa Mbunge kuwa kuanzia miaka 25, lakini kwa CCM suala hilo si sahihi, kwani wabunge wenye miaka 21 wanawajibika vizuri kuliko wazee.

Source: Mwananchi
 
mkuu hata mimi nimeiona tweet. nape sasa anafilisika kisiasa kwa kasi.

mengi-tweet.jpg
 
Nape ni limbukeni anayetumia matope badala ya ubongo katika kauli zake...
 
hahahaha....... nape + mwigulu= messi na Ronaldo wa CCM
 
Nape anaitumbukiza CCM kaburini,Hana adabu kabisa huyu dogo,Anajiona yuko juu ya kila kitu!!!!!!! Kwani wewe Nape unazijua siku za maisha yako? mbona unakuwa ----- sana we dogo!!!
 
Sitoshangaa baadaye atapakosema nilinukuriwa vibaya pale atakapo ulizwa alimaanisha nini aliposema "Waliopendekeza serikali tatu ni wazee wanaosubiri kufa." Kwa kifupi lugha hiyo haifai kutolewa na kiongozi wa haiba yake.

Hatokuwa kijana milele.Hao wazee walikuwa vijana pia.Atakuwa mzee hata yeye.Wazee bado wana nafasi yao muhimu katika jamii yetu huo ndio utamaduni wetu kama Watanzania na Waafrika kwa ujumla wake.
 
Sitaki kuongelea upeo wa nape maana wengi tu mashahidi kutokana na aina ya matamko na majibu ayatoayo!

Mengi amemjibu kwa busara sana!
 
Wakati flani kukaa kimya unaonekan una bupgqara hata kama huna kuliko kufyatuka as if umechomolewa kichwa... kuna haja ya watu kutathmini kwanza thamani ya dhamana waliyopewa kabla ya kuruhusu maneno yakawatoka vinywani mwao...
 
Mmeanza kuwekea watu maneno mdomoni make hamchelewi kusema fulani kasema hivi kumbe umepika tory,
1+1=2 na siyo vinginevyo serikali tatu ndiyo mnyama gani watuondolee uchuro huo.
 
Ndo majembe ya ccm hayo, plus Hammy D, chilisosi, chris lucos. Sijawahi kuona wameongea la maana. Sasa mpaka mzee aw watu kamwona bogus. Kauli ya nape ni sawa na ya wavuta unga kijiweni
 
Nape anaitumbukiza CCM kaburini,Hana adabu kabisa huyu dogo,Anajiona yuko juu ya kila kitu!!!!!!! Kwani wewe Nape unazijua siku za maisha yako? mbona unakuwa ----- sana we dogo!!!
Kwani ccm ya nape mbona unakurupuka bila hata kujua ufanyalo.
 
mkuu hata mimi nimeiona tweet. nape sasa anafilisika kisiasa kwa kasi.

Mkuu Hapo kwenye bold umekosea tena sana!Nape hajawai kufilisika kwani masikini hafilisiki au hujawahi kusikia usemi huo?Nape hajawahi kuwa na akili timamu na mchango wa maana hata cku moja.Namfananisha na mtu asiyejua aendako kwani huwa hapotei.
 
Ndo majembe ya ccm hayo, plus Hammy D, chilisosi, chris lucos. Sijawahi kuona wameongea la maana. Sasa mpaka mzee aw watu kamwona bogus. Kauli ya nape ni sawa na ya wavuta unga kijiweni
Nitahakikisha nchi haitawaliki hii vipi....imekaaje.
 
Hana akili wala adabu huyo Nape. Hata hajui maana ya wazee. Ni kukosa adabu na heshima kwa wazee wetu.

Kila mtu mwenye Akili timamu na kulelewa vyema anajua kabisa Maneno ya mwisho mwisho kwa mzee anayekaribia kufa ni Wosia na busara za msingi sana na siku zote yanaheshimiwa na kuenziwa kama lulu.

Nape naona unatafuta laana za wazee tu. Ipo siku atakuja kuwapigia magoti hao wazee anaowadhihaki sasa.
 
Back
Top Bottom