Mwili wa Samweli Sitta wawasili JNIA

Mwili wa Samweli Sitta wawasili JNIA

Gharama ya kukodi huo mdege sijui ni kodi yangu!!!!?
Bavicha mnapenda kujiegemeza kwenye kodi ili kuhalalisha madai yenu kana kwamba hiyo kodi mnalipa peke yenu.
Mbona hamuulizi viongozi wenu wanalipa pango milioni 60 kwa mwezi kwa kutumia ruzuku ambayo pia ni kodi yetu
 
Ndege ya Emirates iliyobeba mwili wa marehemu Spika mstaafu, Mhe. Samwel Sitta yawasili uwanja JNIA saa 9:05 alasiri. mchana.

View attachment 432202
Mke wa Marehemu Mzee Samuel John Sitta, Mama Magret Simwanza Sitta akiwa ameambatana na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan mara baada ya mwili wa marehemu kutua katika uwanaja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere, Jijini Dar


View attachment 432203

Askari wa Vikosi vya Usalama wakiwa wamebeba mwili wa Mzee Samuel John Sitta mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere leo.
Hiyo picha ya Samia Suluhu hapo juu haikuwa sahihi kwa yeye kufanya kazi hiyo ya kumsindikiza kwa mtindo huo mama Sitta. Nadhani watu wa protocal wamekosea kuruhusu jambo hilo kutokea.
Mama Samia Suluhu ni Makamu wa Rais, Commander in chief, in waiting. Hapaswi kuonyesha kulegezwa hadharani na msiba katika hali yake ya kike mbele ya watu na hasa makamanda wa kijeshi na askari. Katika nyakati kama hizo ni wajibu kumuepusha na maeneo kama hayo hasa hiyo kazi ya kumsindikiza mfiwa aliye kwenye kilio maana naye lazima atalia.
Likitokea la kutokea yeye ndiye Rais na amiri jeshi mkuu, kuna picha gani kama aliwahi kuonekana akiangua kilio hadharani?
Ndio maana huwezi kuona kama Rais kafiwa na mpendwa wake kokote duniani akiangua kilio hadharani.
 
Bavicha mnapenda kujiegemeza kwenye kodi ili kuhalalisha madai yenu kana kwamba hiyo kodi mnalipa peke yenu.
Mbona hamuulizi viongozi wenu wanalipa pango milioni 60 kwa mwezi kwa kutumia ruzuku ambayo pia ni kodi yetu
Ruzuku ni kodi yenu toka lini? Ruzuku ni pesa za wahisani.
 
Marehemu aliwakebehi Watanzania na Maaskofu wetu akidhani hii dunia ni yake na angeishi milele, hastahili heshima yoyote mtu huyu.

Kiukweli kabisa kama binadamu tukiweka kando unafki mwili Sitta unapaswa kuzikwa na City au na Masheikh.

Unamzungumzia Samwel John Sitta au Mwili wa Samwel John Sitta?
 
Kumbe kusafirisha maiti kwa ndege unalipia kama mzigo na maiti inawekwa kwenye buti looh hakyamungu sisi kumbe hatuna thamani dwiiiiiii
Watu tuache ujuaji na jeuri kwa wanadamu wenzetu! Sisi siyo kitu, yaani ni bure kabisa leo hii Sitta ndo anasafirishwa kwenye buti ya ndege? Tunapokuwa hapa duniani tutendeane mema na kuheshimiana huku tukikumbuka kwamba sisi ni mizigo siku tukifariki. Nakumbuka sana maneno aliyoyasema huyu jamaa kwenye kampeni kuhusu ugonjwa wa mzee Lowassa naomba kunukuu (kwanza alianza kwa kuguna - mmmhhh! "Sasa tukisema ugonjwa wa watu wanaanza kunung'unika, watu ni wagonjwa, hii kazi hawataiweza tukiamua kuweka hadharani magonjwa yao itakuwa hatari, hawatufai kwa vile ni wagonjwa na sisi hatutaki mtu wa kwenda ikulu siku mbili amefariki" Sisi jamani ni mizigo sawa na maboksi yaliyojaa ndomu, pichu, n.k Asante Mungu kwa kutukumbusha haya!! Leo watu wamempokea Sitta kwa kumsubiri kama mzigo na siyo kupitia VIP lounge, ni kazi kweli!!
 
Back
Top Bottom