Mwigulu atawaponza wengi!

Mwigulu atawaponza wengi!

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,140
Reaction score
18,004
Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Mwigulu Nchemba ni mwanasiasa wa ajabu sana. Hajali. Hasikii.Haelewi. Anachojali yeye ni kujijenga(pia kujibomoa) katika siasa.Anataka kuaminika kama dawa pekee ya kuwadhibiti CHADEMA kati ya makada wote wa CCM.

Ndiyo maana anafanya anayoyafanya. Mwigulu Nchemba anaamini kuwa anaungwa mkono na Mwenyekiti wa chama pamoja na viongozi wengine waandamizi wa CCM Taifa. Ndiyo maana anaweza hata kubuni 'mijivazi' yake hata inayokwenda kinyume na sare rasmi za chama.Anaweza asiwe sahihi.Aweza kuwa anapotoka. Mwigulu amelewa sifa. Anapepesuka. Kwa wasio makini kisiasa na wanaomtii Mwigulu Nchemba kwa kila alisemalo wataponzeka.

Watasawajika kisiasa na kichama. Jana tu, kijana Mtela Mwampamba ameingia mkenge wa Mwigulu.Amekurupuka na habari za kizushi kuwa eti Mgombea wa Udiwani wa Elerai wa CHADEMA amejiunga CCM. Sasa kijana Mtela Mwampamba HAAMINIKI TENA. Hapa JF ameshapata 'zawadi' yake.

Bado chamani.Bado uraiani.Bado maishani. Bado akilini mwake. Bado atakavyomuona kivingine Mwigulu Nchemba. Bado. Ni wakati sasa wanachama wenzangu wa CCM kuchuja kila kauli na vitendo vya viongozi wetu kama Mwigulu Nchemba ili tuwe huru.Tuwe makini. Kama tunamtegemea Mwigulu Nchemba na siasa zake za aina hii ionekanayo,hatutakuwa makini. Tutakimbiwa.

Siasa iwe ni hoja na si vihoja. Vinginevyo, Mwigulu Nchemba ataponza wengi!

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
 
Ngoja awaponze tu kwakuwa wameamua wenyewe kupumzisha akili zao kwa sababu ya njaa zao.
Sisi tunafurahia sana hizi mbwembwe na vitimbi vya mwigulu na wafuasi wake wawili kwakuwa tunajua ni suala la muda tu wataangukia pua muda si mrefu!
 
Mwampamba amekuwa robot la mwigulu. Anaamriwa afanye ki2 fulani naye anafanya kweli,nahisi hata 0713 akiambiwa na mwigulu atakuwa tayari kumegea angalau mini kabang
 
VUTA NKUVUTE, Mzee Tupa tupa

Tabia za ukweli zinajulikana. Mwalimu Nyerere alipenda kuzisema chache. Yote yafanyikayo sasa yatapata hesabu zake. Bahati nzuri ni kwamba hata wale watu waliokuwa wanaamini kuwa "huu ni mtego wa CHADEMA", sasa wameshaona dhahiri kuwa huu ni "mtego wa wote".

Kwa sababu tunaelekea kunaswa wote kama taifa katika mtego wa siasa za chuki, hila, ukatili, ujambazi na mauaji.

Ni wajibu wetu sote kuutegua mtego huu.
 
Peleka ujinga wako huko. Mwigulu amewashika sehemu mbaya na bado
 
VUTA NKUVUTE, Mzee Tupa tupa

Tabia za ukweli zinajulikana. Mwalimu Nyerere alipenda kuzisema chache. Yote yafanyikayo sasa yatapata hesabu zake. Bahati nzuri ni kwamba hata wale watu waliokuwa wanaamini kuwa "huu ni mtego wa CHADEMA", sasa wameshaona dhahiri kuwa huu ni "mtego wa wote".

Kwa sababu tunaelekea kunaswa wote kama taifa katika mtego wa siasa za chuki, hila, ukatili, ujambazi na mauaji.

Ni wajibu wetu sote kuutegua mtego huu.
Ni kweli Mkuu. Mimi nimejitwika suala hilo. Tupo pamoja kuelekea kupata demokrasia ya kweli ya vyama vingi Tanzania
 
Kijana ambaye kazaliwa baada ya mwaka 1977, haijui CCM na katu hawezi kuijua CCM. Kijana mwenye umri wa miaka chini ya 36 kama anaishabikia CCM haelewi na katu hawezi kuelewa anachoshabikia, hajui kwamba hajui. Kijana ambaye kapata ukombozi wa kifikra na kuijua CCM, lazima ataasi na kuipa CCM mgongo. Ni bahati ilioje kwa taifa kwamba namba ya vijana hawa wanaoamka kutoka usingizi mzito inaongezeka siku hadi siku! Hakika ukombozi unakaribia.
 
hakuna mtu anayenipa raha siku zote kama vuta nkuvute jinsi anavyomalizia post zake kwa utambulisha wake..hah hah hahaaaaaaaaaaaa.n Namafurahi sana rafiki
 
VUTA NKUVUTE, Mzee Tupa tupa

Tabia za ukweli zinajulikana. Mwalimu Nyerere alipenda kuzisema chache. Yote yafanyikayo sasa yatapata hesabu zake. Bahati nzuri ni kwamba hata wale watu waliokuwa wanaamini kuwa "huu ni mtego wa CHADEMA", sasa wameshaona dhahiri kuwa huu ni "mtego wa wote".

Kwa sababu tunaelekea kunaswa wote kama taifa katika mtego wa siasa za chuki, hila, ukatili, ujambazi na mauaji.

Ni wajibu wetu sote kuutegua mtego huu.
Mkuu mbona jina lako matusi nani alikupa hilo jina,kwa nafasi yako ni aibu kuhangaika na watu kama july wadogo sana.

we saizi yako ni akina nape ndiyo hangaika nao kwani john milya n bananga wapo wapi kimya.
 
Back
Top Bottom