Tulimumu
JF-Expert Member
- Mar 11, 2013
- 14,395
- 13,266
Kweli kabisa. Zaidi ya hayo ni kama ameona CCM haiwezi kuipiku CHADEMA kwa sera na ushawishi kaamua kugeukia utengenezaji wa kesi feki za kigaidi. Ukimuangalia hata usoni ni mtu aliyekosa haya. Na nadhati mwenyekiti anamuogopa ndio maana hafanyi lolote kurekebisha uchafu unaofanywa na Mwigulu. Nape pamoja na kelele zote kawa kama mtoto yatima. Ukimuangalia na shughuli zake za kigaidi na Green Guard yake hana tofauti na Jonas Savimbi. Huyu ni laana kwa CCM na taifa. Hivi huu uchumi daraja la kwanza alisoma au alipitia tu chuo? Haendani kabisa na hiyo sifa! Mimi kwa tathmini yangu nasema Sekretarieti iliyokuwa chini ya Makamba ilikuwa na nafuu kubwa kabisa kuliko hii ya kinana. Wale walikuwa wakizungumza kiutu uzima hata wakikosea haikuwa kama mambo ya kitoto na hatari kama tunayoyaona sasa kwa Nape na Mwigulu. Mwenye akili za kiutu uzima katika hii ya sasa ni Kinana peke yake. Ni bahati mbaya amepewa watu wasio na busara na uelewa wa mambo. Sasa ona alivyojichafua na utetezi wake wa GREEN GUARD dhidi ya RED GUARD. Sasa ndio ameharibu kabisa kwani hata yaliyofichika kuhusu Green Guard yamewekwa hadharani!