Mwigulu amvisha mbwa bendera ya CHADEMA

Status
Not open for further replies.
Huyu ndie msomi tena mchumi daraja la kwanza???hii ina tija gani sasa au itasaidia nini kuondoa kero za watanzania?jamaha kweli ana akili ndogo sana,na kaishiwa hoja kabisa!anadhani bado Watanzania wanashabikia u.j.i.n.g.a kama huu?c.c.m ni wachache sana wenye fikra zenye hekima na tija
 
Hakika watu hawanazo kabisa!ni dhahiri huyu jamaa,[Chemba] ni kichaa,maneno yake yanadhirisha matendo yake!ndo usomi wake huo na matambo yake ya kijinga!Angekuwa mwanamke tungesema kafaulu kwa kuvua chupi!sasa sijui kwake yeye tusemeje!
 
Hata mie nilitaka kusema hivyo...Lazima mtu wa namna hii anasumbuliwa na laana...!!

Asubiri 2015 ili kichaa chake kipate tiba!!
sometimes huwa tunaachia vitabia fulani viote mapembe, badae ndio tunakuja kugundua kwamba tulionyeshwa dalili
 
mwigulu hawezi kujenga hoja ndiyo maana anafanya utoto huu, inaonekana kwake yeye siasa ni namna yoyote ile awezavyo kumchafua mwanasiasa asiye wa chama chake
 
Anajua kuwa hana chake tena Iramba mashariki,labda aende jimbo lingine.Pale yuko kwa cdm,hata dr.Mkumbo analifahamu hilo.M4C ikija,atamkumbuka huyo mbwa angalau amkumbatie na mbwa atakuwa katwaliwa
 
kumjadili mzinzi huyu ni kumpa coverage isiyo na msingi. aachwe afanye anavyotaka. wananchi wanajua what is wrong and what is right.
 
Update kutoka facebook:-
Mwigulu ansema "Vua gwanda valisha mbwa ndiyo operation niliyoianzisha imezinduliwa iramba"
attachment.php


wadau hii imekaaje? je ni sawa ?
attachment.php

[video=youtube_share;lZerEan2SZ4]http://youtu.be/lZerEan2SZ4[/video]

attachment.php



[video=youtube_share;Pm900e4TFc c]http://youtu.be/Pm900e4TFcc[/video]

View attachment 62326View attachment 62329View attachment 62350

Anacho fanya Mwigulu naweza fananiasha na mchezaji kuingia na msumari kwenye game ili atoboe mpira kisa timu pinzania wanaonekana kuwazidi kiwango
 
Hivi karibuni tumeona Mwigulu Nchemba ukimvalisha mbwa bendera ya CHADEMA, lakini kabla haujafanya hivyo ebu shughulikia yafuatayo halafu ukipata majibu yake endelea kufanya hivyo. Huu ni Ushauri wa bure

1. Kwanini miaka ya 1970 kulikuwa na viwanda vingi ukilinganisha na nyakati hizi za ulimwengu wa sayansi na teknolojia-vimefirisika katika utawala upi?

2. Kwanini Reli zote za zimeacha kufanya kazi- isipokuwa ile inayokwenda ZAMBIA?

3. Kwanini TANESCO imefikia hatua ya kuzalisha umeme kwa kutumia generator na kuingizia nchi hasara ya mabilioni ya pesa kwa siku kwa kununua mafuta mazito?

4. Kwanini serikali ya chama chako inaendelea kulipa SYMBION Tsh milioni 152 kwa siku tena kwa siri kubwa wakati bunge lilizuia kupitia ripoti ya MWAKYEMBE . Na mnajua kwamba pesa hii ni ya Watanzania maskini?

5. Kwanini wakulima wa jimbo lako la Iramba wanaendelea kulima kwa jembe la mkono na kula mlo mmoja (Ugali wa mtama) baada ya miaka 50 ya uhuru?

6. Kwanini mawaziri ndani ya chama chako wanakuwa na uwezo wa kumiliki nyumba ya milioni 700 ndani ya muda mfupi na hakuna anaewafuatilia?

7. Kwanini viongozi ndani ya CCM wanaweza kuchangia milioni 100 katika harambee ndani ya mwezi mmoja wakati wao ni watumishi wa UMMA-hizo pesa wametoa wapi?

8. Kwanini viongozi ndani ya chama chako wanamiliki bilioni 315 uswisi- wamepataje?

9. Kwanini aliyeiba pesa za EPA hawatajwi na matokeo yake serikali inanunua watu ili iwavalishe kesi za danganya toto?

10. Kwanini kampuni ya ndege ya Serikali (ATCL) nayo Imesimama kama ilivyo kwenye treni?

11. Kwanini serikali yako inalipa wabunge Tsh 200,000 kwa siku huku mkijua kwamba watanzania waliowengi hawajui hata kesho yao?

12. Kwanini wabunge ndani ya chama chako wanaingia mikataba na TANESCO na kusuply matari mabovu, kuiuzia TANESCO mafuta mazito, kuiuzia TANESCO nguzo za umeme toka Iringa na kudanganya kuwa zimetoka Africa kusini hivyo kuwauzia kwa mamilioni ya pesa?

13. Kwanini hamsemi nani anamiliki RICHMOND na DOWANS?

14. Kwanini watumishi wa HALMASHAURI walioiba mabilioni ya pesa kama ilivyo ripotiwa na CAG serikali yako haiwachukulii hatua?

15. Kwanini kodi ya madini inazidiwa na kodi ya machinga?

16. Kwanini hospital nyingi hazina X-ray na CT scan, pia wagonjwa wanalala chini?

17. Kwanini hadi leo wanafunzi wanakaa chini?

18. Kwanini rushwa ya RADA mmeibatiza jina tamu la ''CHENJI YA RADA''

19. Kwanini watanzania wanakwepa kupitishia mizigo yao kwenye bandari ya Dar na kuhamua kupitishia ya Mombasa?

20. Kwanini wezi wa mabilioni adhabu yao huwa ni kujiuzuru bila kuchukuliwa hatua?, tena hujiuzuru kwa kulazimishwa na bunge na siyo chama tawala

Najua kuna mambo mengi ya kukueleza lakini ebu anza na hizo point kumi ndiyo ufanye maamuzi
 
mbizi hata upige violin gitaa ngoma na muziki mzuri kiasi gani yeye atandelea kula majani na kutoa karanga feki kama kawa.
 
alichoma bendela ya CDM? sasa huyo naona kapata lift na anataka kupiga na honi kabisa
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom