Hotuba ya Mbowe mkoani Iringa; Asema CHADEMA inachokozwa, ataja bendera ya CCM

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,458
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyoandaliwa na Baraza la Wanawake wa Chadema (Bawacha) mkoani Iringa

Sehemu ya kauli za Mbowe katika hotuba yake:
"Tumekataa kuwa chama cha tamaa za fedha na uongozi, hata watu tuliokuwa nao walipojaribu kuwa na tamaa hizo, tuliwaachia waondoke."

"Kila mmoja ana mchango katika Chadema, na asitokee mtu kusema ni kazi ya Mbowe, ni kazi ya kila mmoja wetu waliopo hai na waliotangulia mbele za haki. Kadiri watakavyotumia nguvu dhidi ya CHADEMA wajue kuwa wanazidi kutuimarisha zaidi na zaidi"

"Nguvu yetu ya umma tuliyokuwa nayo, tumeheshimishwa na kuaminiwa kwa nguvu hii, wenzetu wanaheshimishwa na nguvu ya dola.

“Nilipokuwa njiani nakuja Iringa nilipata taarifa kuwa kuna kamanda ametoa gizo bendera za Chadema zishushwe, nikiwa njiani nakaribia nikaona bendera nyingi za CCM, nikisema tunaandama kulalamika kitendo hicho watasema nani mchokozi?

“Tumevumilia sana, nawaomba tuendelee kuvumilia, kiongozi wa kisiasa hasa kwa nafasi kama yangu kuna wakati unatakiwa kufanya maamuzi magumu.

“Kabla sijakamatwa nilimuandikia Rais Samia barua mbili nikiomba tukutane naye, sikuweza kukutana naye muda ule kabla ya kuingia gerezani licha ya kuwa alijibu barua yetu ya kuridhia kukutana nasi vyama vya upinzani.

“Niliomba kukutana na Rais aliyepita (kabla ya Samia) lakini haikuwezekana.

“Nilikutana na Magufuli katika matukio mengine lakini siyo kikao cha kazi, wakati kila mmoja alikuwa anamuogopa, mimi nilitaka kumwamba ukweli.

“Nilisema nitamwambia lakini hakunipa hiyo nafasi.

“Rais wa mwisho ambaye tulikaa naye kikao cha kazi ni Kikwete, tumetafuta nafasi ya kuonana na viongozi kwa kuwa tunajua Wanachadema mioyoni mwenu mmebeba nini.

“Ndiyo maana nilipopata nafasi ya kuonana na Rais siku ileile nilipotoka sikutaka kufikiria mara mbili.

“Namshukuru Rais kwa kunipa nafasi hiyo ya kukutana naye, kwa kuwa mimi mwenyewe nilikuwa najiuliza nitoke kwa nafasi ipi baada ya kutoka gerezani.

“Nashukuru mazungumzo yetu yalienda vizuri, nampa hongera kwa kutamua nafasi ya Chadema kama chama kikuu cha upinzani.

“Rais Samia amekuwa Rais wa kwanza tangu kupata uhuru kwa nchi hii kusimama na chama cha upinzani kuzungumza Pamoja lengo likiwa moja kuondoa maumivu katika taifa hili.

“Aliniambia nimueleze Chadema tuna shida gani, nikamwambia sijaenda kumwambia shida, muhimu kwanza ni kujenga msingi wa uvumbuzi wa haki za Watanzania.

“Nilimuomba mama tuzungumze kuhusu haki, kwa kuwa kuendelea kuhubiri amani amani wakati watu wetu wanapigwa risasi si sawa.

“Namshukuru, Waswahili tunasema ‘Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni’

“Nikamwambia mama tuyafanya haya kwa vitendo na siyo maneno, akasema nia yake ni ya kweli. Nikamwambia kuwa Chadema hatujawahi kuwa na nia mbaya, tunataka Serikali iwajibike na wananchi wawe na neema ya kweli, watuachie sisi nafasi yetu kama wapinzani, tuijenge demokrasia, mambo yafanyike kwa uwazi na siyo kwa ukandamizaji.

“Tukakubaliana tutaweka taratibu. Niwaulize Wanachadema kuwa nilikosea wapi?

"Watanzania wana hofu hasa Wanachadema wana hofu sana, ningekuwa ni mjinga kwa kiwango cha lami, kama nafasi tunayoitafuta ya kuweka mambo sawa nisiitumie.

“Tunataka wanachama wa vyama vyote wafanye kazi yao kwa haki, vyombo vya dola vifanye haki.

“Hiki kinachofanyika (polisi Iringa kushusha bendera za Chadema) sicho tulichokubaliana na mama.

“Taharuki iliyojitokeza kwa mimi kwenda Ikulu ni kielelezi kwa jinsi hali ilivyo ya kutoaminiana kama taifa. Mchakato wa kutafuta amani ya taifa siyo jambo la siku moja.

“Wengine wanahisi mimi kwenda kuzungumza na mama Ikulu labda Chadema watakuja kutuambia kuacha habari za Katika. Chadema siyo Mbowe.

“Wengine wanaiambia nikitaka nieleweke nielezea kila kitu nilichozungumza na Rais, haiwezekani, kila jambo lina muda wake, hata Makamu Mwenyekiti alivyokutana na Rais hakuzungumza kila kitu.

“Unatakiwa kuhifadhi chakula, sina nia ya kuwalisha chakula kibichi, lazima ufanye mambo taratibu.

“Mimi nimekaa kwenye chama hiki kwa miaka 30 ya shuruba, ningekuwa nina haraka nisingefika hapa. Wiki moja ijayo tutakaa kikao cha kamati kuu, baada ya hapo tutaendelea kupakua chakula kidogo kidogo kwa uhitaji utakavyokuwa.

“Nikiwa gerezani nilijulishwa mambo kadhaa yanayoendelea kuhusu Chadema ikiwemo makongamano…

“Bila kujenga uwezo wetu wa ndani tutakuwa tunagombanishwa, hatutakiwi kutegemea ruzuku.

“Ningewachangia lakini tangu nimetok gerezani sina simu wala kompyuta, wakubwa hawajanirudishia.
 
Watamrudisha kwenye kanyampasila soon
Bi Tozo ashapiga mahesabu ya kupata hela zaidi za mabeberu so hawezi yauzi mabeberu kwa kumweka tena ndani hasa wakati huu ambapo mabeberu yanapambana na babu Puto wa urusi na so misaada itapungua kwa Africa
 
Screenshot_20220308-165002.png
Screenshot_20220308-213449.png
 
Kama nikweli kayaongea, bac ajiandae tena kurudishwa rumande, na safari hii mama hatasamehe mtu, mama ameshaonyesha wema akawasamehe lakini bado mnaendeleza chokochoko. Haya bwana.
Kaongea nin kibaya hapo cha kuwakasirisha nyie ccm?
 
Kama nikweli kayaongea, bac ajiandae tena kurudishwa rumande, na safari hii mama hatasamehe mtu, mama ameshaonyesha wema akawasamehe lakini bado mnaendeleza chokochoko. Haya bwana.

Hivi akili hizi watanzania mnazitoa wapi. Hivi kazi ya chama cha Upinzani ni nini? Kazi ya chama cha Upinzani ni kuichokonoa serikali pale wanapoona kuna mapungufu.

Ni haki yao na ndiyo wajibu wao namba moja katika mfumo wa kidemokrasia wa vyama vingi. Tatizo watanznia wengi sio tu kuzaliwa hata mimba zetu zilitungwa kwa uoga na nidhamu ya kinafiki.
 
Bi Tozo ashapiga mahesabu ya kupata hela zaidi za mabeberu so hawezi yauzi mabeberu kwa kumweka tena ndani hasa wakati huu ambapo mabeberu yanapambana na babu Puto wa urusi na so misaada itapungua kwa Africa

Mtamuekewa tu mama.
 
Nafikiri Chademqa sometimes wa ignore vitu vidogo vidogo wajikite kwenye main issues

Vibendera tu ndivyo kuvigeuza main issue ya media attention?
Mfano Kesho utakuta vichwa vya habari magazetini vinasema magari ya Chadema yashushwa bendera na Polisi !!! Habari ya Mbowe kahutubia nini hawaandiki

Wangeyashusha chap chap bila mtafaruku ili media zijikite zaidi kwenye alichosema Mbowe

Washaharibu vichwa vya habari vya magazeti Kesho

Vizuri Chadema kwenye siasa kujua main issue ni ipi na minor ni ipi?
Swala la kufanya hivyo vibendera kuwa main issue hawajitetendei haki wenyewe
 
Wakishusha vibendera, wataambiwa waondoe viti. Wakiondoa viti wataambiwa waondoke ukumbuni. Kesho vichwa vya habari vitakuwa '' Mkutano wa Bawacha Wavunjwa kwa vurugu''

Kitu cha kujiuliza, hizo bendera zimevunja sheria gani za nchi?
Mbona za CCM zinapepea wakati wa shughuli zao kuanzia Airport hadi Ikulu?

Kuna tatizo sehemu mbili. Jeshi la Polisi limechoka na ni wakati sasa uongozi ubadilishwe

Msajili wa vyama yupo kimyaaa! hebu atoke aeleze ni sheria gani ya vyama vya siasa imekiukwa
Nadhani Msajili naye ni tatizo kubwa kama la Polisi. Ni tatizo kubwa sana

JokaKuu Pascal Mayalla
 
Kwaleo sijaelewa kitu kwamara yakwanza toka namfahamu mbowe Leo ndo sijamwelewa ngoja tusubirie hotuba baada ya kikao chakamati kuu
 
Nafikiri Chademqa sometimes wa ignore vitu vidogo vidogo wajikite kwenye main issues

Vibendera tu ndivyo kuvigeuza main issue ya media attention?
Mfano Kesho utakuta vichwa vya habari magazetini vinasema magari ya Chadema yashushwa bendera na Polisi !!! Habari ya Mbowe kahutubia nini hawaandiki

Wangeyashusha chap chap bila mtafaruku ili media zijikite zaidi kwenye alichosema Mbowe

Washaharibu vichwa vya habari vya magazeti Kesho

Vizuri Chadema kwenye siasa kujua main issue ni ipi na minor ni ipi?
Swala la kufanya hivyo vibendera kuwa main issue hawajitetendei haki wenyewe
Tatizo lako haujafundishwa maana na sifa ya bendera, ujaribu kutembea wakati bendera inapandishwa au inashushwa ndipo utakapojua ni kijibendera.
 
Tatizo lako hsujafundishwa maana na sifa ya bendera, ujaribu kutembea wakati bendera inapandishwa au inashushwa ndipo utakapojua ni kijibendera.
Hiyo ya heshima kubwa ni bendera ya nchi sio ya Chama cha Siasa hata kiwe CCM !! Bendera za vyama hazina hadhi hiyo ya bendera ya taifa

Wewe ndio hujui hakukuwa na sababu ya C8 kuona kama big issue
 
Back
Top Bottom