Mwigulu amvisha mbwa bendera ya CHADEMA

Mwigulu amvisha mbwa bendera ya CHADEMA

Status
Not open for further replies.
Mwenyekiti naondoka kwenye chama chake na kurudisha bendera zote zinachanwa kwenye makaratasi je zile alizokuwa anatumia ziko wapi,au hakuwahi kutumia hata moja.
Mwigulu hizi siasa uliziiga wapi na je huko ulikoiga wamefanikiwa kwa kiwango gani.
 
Mpotezeeni wana JF hana akili yule,dawa ni kuhakikisha jimbo anachukua Kitila Mkumbo ndipo atakaposhika adabu!Cha muhimu wana CDM siku ya M4C iramba tujitahidi sote kwa umoja wetu mwingi tuwe pamoja kuzunguka vijiji vyote vya iramba kuwaelimisha watanzania
 
hivi karibuni tumeona mwigulu nchemba ukimvalisha mbwa bendera ya chadema, lakini kabla haujafanya hivyo ebu shughulikia yafuatayo halafu ukipata majibu yake endelea kufanya hivyo. Huu ni ushauri wa bure

1. Kwanini miaka ya 1970 kulikuwa na viwanda vingi ukilinganisha na nyakati hizi za ulimwengu wa sayansi na teknolojia-vimefirisika katika utawala upi?

2. Kwanini reli zote za zimeacha kufanya kazi- isipokuwa ile inayokwenda zambia?

3. Kwanini tanesco imefikia hatua ya kuzalisha umeme kwa kutumia generator na kuingizia nchi hasara ya mabilioni ya pesa kwa siku kwa kununua mafuta mazito?

4. Kwanini serikali ya chama chako inaendelea kulipa symbion tsh milioni 152 kwa siku tena kwa siri kubwa wakati bunge lilizuia kupitia ripoti ya mwakyembe . Na mnajua kwamba pesa hii ni ya watanzania maskini?

5. Kwanini wakulima wa jimbo lako la iramba wanaendelea kulima kwa jembe la mkono na kula mlo mmoja (ugali wa mtama) baada ya miaka 50 ya uhuru?

6. Kwanini mawaziri ndani ya chama chako wanakuwa na uwezo wa kumiliki nyumba ya milioni 700 ndani ya muda mfupi na hakuna anaewafuatilia?

7. Kwanini viongozi ndani ya ccm wanaweza kuchangia milioni 100 katika harambee ndani ya mwezi mmoja wakati wao ni watumishi wa umma-hizo pesa wametoa wapi?

8. Kwanini viongozi ndani ya chama chako wanamiliki bilioni 315 uswisi- wamepataje?

9. Kwanini aliyeiba pesa za epa hawatajwi na matokeo yake serikali inanunua watu ili iwavalishe kesi za danganya toto?

10. Kwanini kampuni ya ndege ya serikali (atcl) nayo imesimama kama ilivyo kwenye treni?

11. Kwanini serikali yako inalipa wabunge tsh 200,000 kwa siku huku mkijua kwamba watanzania waliowengi hawajui hata kesho yao?

12. Kwanini wabunge ndani ya chama chako wanaingia mikataba na tanesco na kusuply matari mabovu, kuiuzia tanesco mafuta mazito, kuiuzia tanesco nguzo za umeme toka iringa na kudanganya kuwa zimetoka africa kusini hivyo kuwauzia kwa mamilioni ya pesa?

13. Kwanini hamsemi nani anamiliki richmond na dowans?

14. Kwanini watumishi wa halmashauri walioiba mabilioni ya pesa kama ilivyo ripotiwa na cag serikali yako haiwachukulii hatua?

15. Kwanini kodi ya madini inazidiwa na kodi ya machinga?

16. Kwanini hospital nyingi hazina x-ray na ct scan, pia wagonjwa wanalala chini?

17. Kwanini hadi leo wanafunzi wanakaa chini?

18. Kwanini rushwa ya rada mmeibatiza jina tamu la ‘’chenji ya rada’’

19. Kwanini watanzania wanakwepa kupitishia mizigo yao kwenye bandari ya dar na kuhamua kupitishia ya mombasa?

20. Kwanini wezi wa mabilioni adhabu yao huwa ni kujiuzuru bila kuchukuliwa hatua?, tena hujiuzuru kwa kulazimishwa na bunge na siyo chama tawala

najua kuna mambo mengi ya kukueleza lakini ebu anza na hizo point kumi ndiyo ufanye maamuzi
ushauri wako mzuri,lakini huyu jamaa kuna matatizo zaidi ya hayo,akili zake haziko sawa,kwanza inabidi atafutiwe tiba vinginevyo ni kujaribu kumvalisha nguo kichaa aliyevua nguo hadharani kabla ya kutibu gonjwa lake ata nguo utakazomvalisha atazivua.
 
Equal Rights and Justice. Ingekuwa vipi bendera ya chama chake ingekuwa treated the same? Tuna tatizo la kimfumo.
 
huu utani mwingine bwana inamaana chadema wanafanana na mbwa?
 
lakn hii yote imechangiwa na upuuz wa watz walio weng hambao wanazd kuchaguwa viongo wa aina hii!!..akiamungu na bado watz chamoto watakiona..wameyataka wenyewe
 
Na bado tutavalisha hadi nguruwe hiyo bendera lakini haita zuia nia ya dhati ya ukombozi ya chadema kama sisi CCM tumechemka na tujiulize ni wapi tulipodondokea
 
Amejidhalalisha mwenyewe. Ingekuwa ni kiongozi wa cdm amefanya hivyo ingetoka kwenye ukurasa wa kwanza wa gazeti la uhuru.
 
tehe tehe

Kakende Siasa ndio zilivyo kesho uko huku siku ingine ndo hivyo unarekea huku. Hizo point 20 Mwigulu zote za kwake? Yy anaangalia Jimbo lake akishindwa mwaka 2015 atawaachia wengine
 
Hizo point 20 inabidi azitafakari harafu aone kama kuna aja ya kunvalisha mbwa bendera ya chama kinachoelimisha wananchi kuhusu haki zao
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom