Mwigulu amvisha mbwa bendera ya CHADEMA

Mwigulu amvisha mbwa bendera ya CHADEMA

Status
Not open for further replies.
Dr. Slaa alisema mkiichagua CCM ni maafa, sasa tumeisha yashuhudia
 
duh...hivi CCM imefikia hapa?Kweli Mwal angefufuka angepat akifo ghfla.
 
Hivi karibuni tumeona Mwigulu Nchemba ukimvalisha mbwa bendera ya CHADEMA, lakini kabla haujafanya hivyo ebu shughulikia yafuatayo halafu ukipata majibu yake endelea kufanya hivyo. Huu ni Ushauri wa bure

1. Kwanini miaka ya 1970 kulikuwa na viwanda vingi ukilinganisha na nyakati hizi za ulimwengu wa sayansi na teknolojia-vimefirisika katika utawala upi?

2. Kwanini Reli zote za zimeacha kufanya kazi- isipokuwa ile inayokwenda ZAMBIA?

3. Kwanini TANESCO imefikia hatua ya kuzalisha umeme kwa kutumia generator na kuingizia nchi hasara ya mabilioni ya pesa kwa siku kwa kununua mafuta mazito?

4. Kwanini serikali ya chama chako inaendelea kulipa SYMBION Tsh milioni 152 kwa siku tena kwa siri kubwa wakati bunge lilizuia kupitia ripoti ya MWAKYEMBE . Na mnajua kwamba pesa hii ni ya Watanzania maskini?

5. Kwanini wakulima wa jimbo lako la Iramba wanaendelea kulima kwa jembe la mkono na kula mlo mmoja (Ugali wa mtama) baada ya miaka 50 ya uhuru?

6. Kwanini mawaziri ndani ya chama chako wanakuwa na uwezo wa kumiliki nyumba ya milioni 700 ndani ya muda mfupi na hakuna anaewafuatilia?

7. Kwanini viongozi ndani ya CCM wanaweza kuchangia milioni 100 katika harambee ndani ya mwezi mmoja wakati wao ni watumishi wa UMMA-hizo pesa wametoa wapi?

8. Kwanini viongozi ndani ya chama chako wanamiliki bilioni 315 uswisi- wamepataje?

9. Kwanini aliyeiba pesa za EPA hawatajwi na matokeo yake serikali inanunua watu ili iwavalishe kesi za danganya toto?

10. Kwanini kampuni ya ndege ya Serikali (ATCL) nayo Imesimama kama ilivyo kwenye treni?

11. Kwanini serikali yako inalipa wabunge Tsh 200,000 kwa siku huku mkijua kwamba watanzania waliowengi hawajui hata kesho yao?

12. Kwanini wabunge ndani ya chama chako wanaingia mikataba na TANESCO na kusuply matari mabovu, kuiuzia TANESCO mafuta mazito, kuiuzia TANESCO nguzo za umeme toka Iringa na kudanganya kuwa zimetoka Africa kusini hivyo kuwauzia kwa mamilioni ya pesa?

13. Kwanini hamsemi nani anamiliki RICHMOND na DOWANS?

14. Kwanini watumishi wa HALMASHAURI walioiba mabilioni ya pesa kama ilivyo ripotiwa na CAG serikali yako haiwachukulii hatua?

15. Kwanini kodi ya madini inazidiwa na kodi ya machinga?

16. Kwanini hospital nyingi hazina X-ray na CT scan, pia wagonjwa wanalala chini?

17. Kwanini hadi leo wanafunzi wanakaa chini?

18. Kwanini rushwa ya RADA mmeibatiza jina tamu la ‘’CHENJI YA RADA’’

19. Kwanini watanzania wanakwepa kupitishia mizigo yao kwenye bandari ya Dar na kuhamua kupitishia ya Mombasa?

20. Kwanini wezi wa mabilioni adhabu yao huwa ni kujiuzuru bila kuchukuliwa hatua?, tena hujiuzuru kwa kulazimishwa na bunge na siyo chama tawala

Najua kuna mambo mengi ya kukueleza lakini ebu anza na hizo point kumi ndiyo ufanye maamuzi

Mkuu si point kumi tu ni ishirini! Nakushukuru sana kwa jinsi ulivyoweza kuchambua maudhi haya ambayo yanatokana na utawala mbovu wa CCM na serikali yake.
 
haki ya Mungu naogopa ban. ila hy mwigulu sijui nimfanishe na nani maana akili yake nimefeli kumwelewa je kura za maoni alipita vipi. hy bwana anapenda mipasho sana nadhani hajakomaa kisiasa

Mtu anayejifanya ni mzalendo kuliko wengine ujue si raia,Mwigulu huvaa bendera ya taifa kumbe ni mtu hatari sana.sijui tunaenda wapi na mtu huyu hatari.
 
Me nadhani Mwigulu ni mpuizi sana kwana hanaga point hata moja zaidi ya ujinga ujinga tu kila siku.

Ni vioja ju ya vioja kwa Mwigulu hana maana hata kidgo mkiendelea kumfuatilia atawaumiza roho bure km vp tumpotezee tu. Ujue hakuna adhabu kubwa hapa duniani km kuuzwa na walimwengu.
 
Sidhani kama ni taboo mbwa kuvaa bendera ni kitu cha kawaida kabisa. Mbaya ni kuwa mbwa huyu wa Mwigulu amelazimishwa wakati wengine wapo very friendly.

images



E001_A.jpg
Nadhani ni more of a cultural issue.Kwa wabongo mbwa anadharaulika kwenye culture yetu.Kwa wenzetu mbwa anapendwa na hilo ni kama promotion kumvisha bendera.Kuna hadi high school ina symbol ya bulldog,na kwenye matukio ya kuiwakilisha shule hata michezo ie football,basi unakuta wanaingia na bulldog aliyevishwa bendera yao,sasa shangaa utofauti.
 
ndugu mimi nafikiri ya kuwa umepewa kichwa na nywele kwa lengo la kufikiri kama alivyo sema kaka yenu werema kumbe kichwani hamna kitu chochote kwa hicho ulichokifanya inaonyesha ya kuwa uwezo wako wa kufikiria ni mdogo kuliko hata huyo mbwa kwani laiti kama ungemuuliza angekuambia ya kuwa mbona mimi nilishaivaa muda mrefu hiyo bendela lakini kamwe sitavaa ya nyinyiem
 
Bora unipe kazi ya kumpigia mbuzi gitaa acheze nitaifanya lakini si kazi uliyoifanya hapa mkuu
 
Equal Rights and Justice. Ingekuwa vipi bendera ya chama chake ingekuwa treated the same? Tuna tatizo la kimfumo.

ni nini solution ya tatizo la kimfumo?Mwigulu mchemba mm nahisi alipokuwa mdogo alianguka ubongo ukavurugika au kuna lishe muhimu alikosa akili ikaharibika then alipokuwa mkubwa ndio kafojifoji shule kapata degree lakini ile akili asili common sense hana unaweza tu kumuita imbecile au insane utakuwa umemtendea haki kabisa!!
 
Wanajamvi mkiongozwa na MNYISANZU, Mdwenke, Kitila Mkumbo, Filipo Tafuteni kujua kisha mnieleze hapa jamvini, jina "MAKALA" lina maana gani kwa wakazi wa iramba (wanyiramba)

hint;
msengi = simba
kitundu = kifaru
nzetu = nyau aka paka.

Kisha turudi kumjadili mwigulu.
 
Last edited by a moderator:
Mnategemea CCM wafanye nini kwa wakati huu? wamebanwa kila kona, hali yao ni mbaya kiasi tusivyoweza kuelezea hapa, sasa inabidi watafute hata mambo ya kijinga angalau muwakumbuke kama hivi tunavyomjadili Nchemba hapa yeye anafurahi maana anaona kumbe na yeye anakumbukwa na sasa anaongelewa, John Mnyika alisema kule bungeni anawaachia machizi waendelee na uchizi wao, nakushauri mleta mada next time muache Nchemba aendelee na uchizi wake sisi tujadili mambo mengine, hayo maswali uliyomuuliza hata ukiwaita viongozi wote wa CCM ukawauliza watakuambia hawajui, kwani c ulimsikia Mr President akisema hajui kwanini Watanzania ni masikini? hayo maswali hautakaa ujibiwe milele sio na CCM wala Nchemba, unamuuliza Nchemba kuhusu wananchi wake kula mlo mmoja kwa siku? ngoja nikuambie jibu analowaza japo hawezi kulisema hadharani (INANIHUSU NINI MIMI NA SHIDA ZAO)hayo ndio majibu ndani ya mioyo yao.
 
Mpotezeeni wana JF hana akili yule,dawa ni kuhakikisha jimbo anachukua Kitila Mkumbo ndipo atakaposhika adabu!Cha muhimu wana CDM siku ya M4C iramba tujitahidi sote kwa umoja wetu mwingi tuwe pamoja kuzunguka vijiji vyote vya iramba kuwaelimisha watanzania

hapo nakuunga mkono, nawasihi wanachadema kutojiingiza kwenye mtego wa ujinga watu wajinga na limbukeni wa kisiasa, hoja ni kutwaga M4C wilaya nzima , na hawezi kuzuia sababu hakuna sheria yenye hati miliki na wilaya, bali vyma vyote vinaruhusiwa kufanya shughuli za kisiasa mahala popote.
 

Matendo ya mtu yanatakiwa yaendane na hadhi yake katika jamii,upeo wake katika kufikiri,elimu yake na haiba yake.Sasa kama ni kweli ni yeye ndiyo amefanya hayo,ni aibu kwa wapiga kura wake,bunge na chama anachokitumikia kwa sababu:

1.Mbwa ana husika nini na siasa?
2.Labda anataka kuhusisha heshima ya mbwa na bendera ya chadema,lakini ukweli ni kwamba mbwa ni mnyama mwenye heshima kwa binadamu ndiyo maana hufugwa kwa ulinzi,hata jeshi la polisi linamtumia mnyama huyu katika kazi za kiusalama,hinyo uwezo wake kufikiri ni finyu kwa jambo dogo kama hilo.
3.kama msomi,alitakiwa kusema ni kwanini anadhani bendera ile anastahili mnyama kama mbwa na si vinginevyo
Kijume na hapo,the person is a fool and mad.
 
Nadhani ni more of a cultural issue.Kwa wabongo mbwa anadharaulika kwenye culture yetu.Kwa wenzetu mbwa anapendwa na hilo ni kama promotion kumvisha bendera.Kuna hadi high school ina symbol ya bulldog,na kwenye matukio ya kuiwakilisha shule hata michezo ie football,basi unakuta wanaingia na bulldog aliyevishwa bendera yao,sasa shangaa utofauti.

Mkuu, nikweli tamaduni zinatofautiana. Si unaona hata katika swala la ushoga tunavyotofautiana na hao wenzetu.
 
ukikuta mtu mzima kaamua asichambe,,hakuna namna unaweza kumrekebisha! ile tabia iko kwenye damu... ila 2015 ndio mwisho wao! sisi tujitahidi tu kupiga kura na kuzilinda!
 
Sioni sababu ya kuumiza kichwa na huyu mwigulu wacha apeperushe hiyo bendera awavalishe hata punda nao waendeleze kuitangaza CHADEMA. Lakini mwigulu anapofanya haya akumbuke jimbo lake lina maendeleo kiasi gani nini matatizo ya jimbo lake. mwigulu kama wewe ni mtu uliye na uchungu na nchi yako hebu tueleze. Umeshughulikia vipi suala la Rada,EPA,Rushwa na rasilimali za nchi zinazoibiwa na majangili hapa tz. Inakusaidia nini grade A yako kama mchumi wa nchi kwa uchumi unaoporomoka kila kukicha? Nakufananisha na mtu yeyote asiyeitumia akili yake ipasavyo! Siasa umedandia ulipofanikiwa kupewa hiyo post umeota mapembe! Endelea na huo upuuzi wako nenda Mwanza, Iringa, Mbeya, Arusha,Kilimanjaro, Bukoba na Kigoma ukaone watu wanavyoendelea kiuchumi na elimu kama utakutana na hayo matembe! Think Twice.
 
Wadau kitendo kilchofanywa na wafuasi wa ccm kwenye mkutano wa Mwigulu Nchemba ni kitendo cha uzalilishaji mkubwa.Swali langu ni hivi kama mtu anaweza kufunguliwa kesi na kunyanganywa ubunge kwa kosa la kutoa lugha ya matusi kwenye campain inakuwaje kitendo kama hichi kisiwe kosa kisheria?Na kama ni kosa kisheria waliokuwa wanatenda jambo hili hadharani walikuwa hawajui kuwa ni kosa kisheria?Na kama walijua na kufanya vile hadharani kwanini tusihisi kuwa wamefanya hayo kwa maelekezo ya wakubwa?Polisi kutokuchukua hatua mpaka wakati huu kwanini tusiamine ni mkakati wa wakubwa?Polisi huwa wanazuia maandamano kwa kisingizio cha kuhofia vitendo vya uvunjifu wa amani sasa kitendo hichi hakiwezi kuwa cha uvunjifu wa amani?Na kama ndio wamechukua hatua gani?Je kitendo hichi kingefanywa na wafuasi wa chadema polisi wasingechukua hatua?Ni makosa kusema polisi wanatumka kisiasa kwa maslahi ya chama tawala?Je chadema wakiamua kulipiza kisasi amani itakuwepo?

Mlioko madarakani mkumbuke cheo ni dhamana na nyinyi na chama chenu hamatadumu madarakani milele.

Mwisho mkumbuke maovu yote mnayoyafanya kama ufisadi n.k yatabaki ktk kumbukumbu.Swala la nyinyi kushitakiwa si tatizo hata mkiwa na umri wa miaka 80.Mjifunze kwa Mbaraka wa Misri na watawala wengine.

Hizi tuhuma na kesi mnazozizima kila siku ni kazi bure bali mnachofanya ni kuziahirisha tu.Usahahidi na ukweli utadumu milele lakini chama chenu hakitadumu milele na siku mkitoka madarakani ndio mwanzo wa nyiniyi kushitakiwa.Labda mwenyemuzi awachukue na hata hivyo lazima baadhi miongini mwenu mje kuwajibika.
 
Nadhani tuachane na huyu mwehu makamanda, tunampandisha sana kujadili kile kituko chake...na ndio maana sijasikia tamko lolote la chama chetu maana CHADEMA haina kawaida ya ku-deal na wehu.
 
huyo ni mnafiki na chama chake cdm itawakomboa watanzania tuone atajificha wapi ,atafuta umaarufu asiokuwa nao hana sera inaonekana hata darasani alibebwa ,hata kazini alishikwa mkono ana uwezo mdogo kama chama chake
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom