Mwenyekiti wa Wazazi Taifa atembelea eneo litakalojengwa Mradi wa Kiwanda cha Wazazi

BWANKU M BWANKU

JF-Expert Member
Jan 12, 2019
328
414
IMG-20231117-WA0000.jpg

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi- Taifa Ndugu Fadhili Maganya (mwenye suti nyeusi) wiki hii Jumanne Novemba 14, 2023 akiongozana na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi mkoa wa Tanga Ndugu Mbezi pamoja na baadhi ya viongozi wa Chama na Jumuiya wamekagua eneo panapotarajiwa kujengwa kiwanda cha kusindika matunda, wilayani Muheza katika eneo la Kwa Fungo.

Jumla ya hekari 50 zimepatikana Kwa ajili ya uwekezaji huo utakaofanywa na Jumuiya ya Wazazi. Huu ni uelekeo wa Jumuiya hiyo kujikita kiuchumi kwa kuwa na miradi mbalimbali ya uchumi inayoendelea kutekelezwa na Jumuiya ya Wazazi nchi nzima ikigusa viwanda, hospitali, ufugaji na shule.

Mpaka sasa Jumuiya ya Wazazi imeshapata eneo la kujenga miradi mikubwa ya hospitali maalum kwa kupata eneo Kahama, Iringa na Pemba na kote mipango ya ujenzi na utekelezaji wa miradi hiyo inaendelea.
 
Wana jenga jengo la biashara pale sababa - Dodoma

Hiki chama kingine hakina ata radio lakini mwenyekiti ana radio pale machame😂🤣😂
 
Wana jenga jengo la biashara pale sababa - Dodoma

Hiki chama kingine hakina ata radio lakini mwenyekiti ana radio pale machame😂🤣😂
Hivi kinaweza kujenga kiwanda atakaeruhusu usajili nani???afrika ukiwa mpinzanzi funga mkanda kuna siku utaletewa tuhuma kuwa hizo korodani sio zako umezipata kwa njia haramu🤣🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom