Mjumbe wa Halmashauri Kuu CCM Taifa, Khamis Hamza Chilo, Amewataka wana CCM Wilaya ya Ilala Kuondoa Makandokando na Kujenga Mshikamano.

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,898
942
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM Taifa, Khamis Hamza Chilo, amewataka wana CCM Wilaya ya Ilala kuondoa makando kando na kujenga mshikamano kuakikisha CCM inashika dola.

MNEC Khamis Hamza Chilo alisema hayo kata ya Ilala katika mkutano mkuu wa Jumuiya ya Wazazi ya chama cha Mapinduzi ulioandaliwa na kamati ya Utekelezaji kata ya Ilala.

"Nawaomba wan CCM wezangu muondoe makundi na Mkanganyiko ndani ya chama chetu kiweze kushinda na kushika dola hivyo tuache makundi na makando kando "alisema MNEC Khamis .

MNEC Khamis Hamza Chilo alisema chama cha Mapinduzi uhai wake ni wanachama, CCM ina wenyewe na wenyewe ndio sisi kwa ushirikiano wa umoja wetu katika kujenga chama na jumuiya zake.

Aliagiza umoja na mshikamano uendelezwe ili CCM iweze kusonga mbele na kushinda kwa kujenga umoja na mshikamano itashinda katika chaguzi za Serikali za mitaa.

Alisema uongozi anapanga Mwenyezi Mungu hivyo amewataka wana Ilala kumpa ushirikiano Mbunge wa jimbo la Ilala ambaye ni Naibu Spika Mussa Zungu na Diwani wa Ilala Saady Khimji kwa utekelezaji wa Ilani ya CCM vizuri ambapo kata ya Ilala utekelezaji umefanyika vizuri wa miradi ya maendeleo vikiwemo vituo vya afya,Barabara, na sekta ya Elimu

MNEC Khamis Hamza Chilo akizungumzia Jumuiya ya Wazazi ya CCM kata ya Ilala ina jukumu kubwa la kumsaidia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan katika utekelezaji wa Ilani ya chama cha Mapinduzi CCM katika kusimamia miradi ya maendeleo.

Alipongeza Jumuiya ya Wazazi kata ya Ilala kwa kuandaa mkutano mkuu pamoja na kufanya kazi kubwa ikiwemo kusaidia jamii ya eneo la kata ya Ilala

Aliagiza Jumuiya ya Wazazi kata ya Ilala kulinda watoto na kusimamia maadili ikiwemo kufatilia matokeo yao kitaaluma shuleni kwa kushirikiana na walimu .

Aliwataka Wazazi kwenda kusimamia sekta ya Elimu ili waweze kupata viongozi bora wa Taifa la kesho ambalo litaibua mawaziri na Rais waje kusaidia chama cha Mapinduzi.

Wakati huohuo MNEC Khamis Hamza Chilo aliwataka Jumuiya ya wazazi wajiandaae kwa ziara maalum ya kwenda Zanzibar ambayo anatarajia kuwapa mwaliko rasmi hivi karibuni kwenda kujifunza.
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2024-01-03 at 22.26.03.jpeg
    WhatsApp Image 2024-01-03 at 22.26.03.jpeg
    46 KB · Views: 5
  • WhatsApp Image 2024-01-03 at 22.26.03(1).jpeg
    WhatsApp Image 2024-01-03 at 22.26.03(1).jpeg
    60.3 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2024-01-03 at 22.26.02.jpeg
    WhatsApp Image 2024-01-03 at 22.26.02.jpeg
    53.2 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2024-01-03 at 22.26.02(1).jpeg
    WhatsApp Image 2024-01-03 at 22.26.02(1).jpeg
    42.3 KB · Views: 3
Back
Top Bottom