Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 36,357
- 23,760
Ndugu zangu Watanzania,
Ni lazima tufahamu kama Taifa tuna maadui ambao kila siku wanawaza na kufikiria namna ya kuichafua Nchi na Taifa letu kimataifa,namna ya kuharibu taswira nzuri ya Taifa letu,namna ya kuvuruga amani na utulivu wa Taifa letu,namna ya kuharibu umoja wa kitaifa,namna ya kuchochea machafuko na tggmavurugu hapa Nchini.
Wanawaza haya kwa sababu wanajua palipo na amani ,umoja na mshikamano wa kitaifa kama ilivyo hapa Nchini ni lazma pawepo na maendeleo na Ustawi wa Wananchi. Wanajua Amani na utulivu wetu hapa Nchini imekuwa chachu ya maendeleo yetu tuliyonayo hapa Nchini. Wanajua ndio imekuwa sumaku ya kuwanasa na kupokea maelfu kwa maelfu ya watalii hapa Nchini mpaka kufikia watalii million mbili kwa Mwaka.
Hivyo wanajua ili kuuwa uwekezaji ,biashara na utalii hapa Nchini ni sharti kuchochea machafuko na vurugu kwa kutumia aidha vibaraka wao waliowapandikiza hapa Nchini ambao wamekosa uzalendo kwa Taifa letu au kwa kutumia vitaasisi vyao walivyovipa majina tofauti tofauti ya utetezi wa kitu fulani au harakati fulani ili kutoa maneno ya kichochezi ,uongo na Uzushi usio na ushahidi wa aina yoyote ile.
Hii yote ikiwa ni katika juhudi za kutukwamisha katika juhudi zetu za kujenga uchumi jumuishi na kuondokana na utegemezi na kuomba omba. Kasi ya kukua kwa uchumi wetu ,kuongezeka kwa mapato ya ndani ,kuongezeka kwa shughuli za kibiashara na uwekezaji kumekuwa tishio na kuwapa Homa maadui zetu. Ndio sababu wanatumia kila njia kutaka kujaribu kuharibu amani yetu tuliyonayo hapa Nchini.
Hata hii habari ya kusema kuna mipango ya kumzuru Lissu kwa kumuwekea sumu akiwa gerezani ni habari za uongo,uzushi na uchonganishi tu . Kwa sababu habari hizo hazina ukweli wala ushahidi wa aina yoyote ile na wala hakuna kitu cha namna hiyo kinaweza kufanyika chini ya serikali hii imara ,shupavu na madhubuti ya Rais Wetu Mpendwa Mama Samia Suluhu Hasssan.
Ikumbukwe ya kuwa katika kipindi hiki cha Kuelekea uchaguzi Mkuu. maadui zetu nao wapo kazini kujaribu kuleta mtafaruku na kutuondoa kwenye njia na malengo yetu. Lakini kubwa ni kuwa hawa maadui zetu kwa kushirikiana na vibaraka wao wanajaribu kutaka kumchafua Rais wetu Mpendwa na serikali yake. Wanataka na kujaribu kuleta Mkwamo kwa kuwa wanajua namna anavyokubalika ,kupendwa na kuaminika kwa watanzania ambao wamepania kumrejesha Ikulu kwa kura nyingi za ndio. Wanataka kuondoa Imani ya watanzania kwa Rais wetu, jambo ambalo hata hivyo hawawezi kufanikiwa na kufanikisha.
Hivyo basi watanzania wote tunapaswa kuwa makini na matamko mbalimbali yanayotolewa na vibaraka wa Mabeberu pamoja na mabeberu wenyewe. Tuwe makini na kauli zao na tusiwaunge mkono wala kuwasikiliza. Tushikamane na kuungana kama Taifa kusimama na Rais wetu. Tusikubali na kukaa kimya pale mtu anapotokea kumchafua Rais wetu na serikali yetu pamoja na kuipaka matope nchi yetu. Tulinde amani yetu kwa wivu mkubwa sana na kwa gharama yoyote ile.
Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.