ndege JOHN
JF-Expert Member
- Aug 5, 2015
- 19,579
- 44,821
Maisha yenyewe ya sasa ukijichanganya ukaishi maisha fake ya kuigiza lazima u collapse tu kuna mpangaji mwenzangu single mother aliforce kumpeleka mtoto shule hizi za mamilion sasa hata baba mtoto amegoma kulipa ada mambo magumu Leo hii kafikisha miezi Sita anadaiwa tu kodi ila baba mwenye nyumba wetu mvumilivu sana anapigwa tu sound ametulia kuna mwingine yeye alidaiwa kodi ya mwaka mzima hadi akakimbia chumba kaacha kitanda na vyombo mwenye nyumba na mjumbe wamevunja mlango Mwenyenyumba kachukua Mali hizo.Mimi binafsi sijawahi kupitisha miezi miwili bila kulipa yaani bora nidaiwe kausha damu huko kuliko kodi ya chumba nacholala.