GE2025 Mwenezi BAWACHA, Sigrada Mligo ajiondoa CHADEMA, ahamia CHAUMMA

GE2025 Mwenezi BAWACHA, Sigrada Mligo ajiondoa CHADEMA, ahamia CHAUMMA

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
4,481
Reaction score
14,856
Aliyekuwa Katibu Mwenezi wa Baraza la Wanawake wa CHADEMA (BAWACHA) taifa, Sigrada Mligo, ametangaza kujiondoa rasmi ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) akilalamikia kile alichokiita kauli za kubeza mchango wake na mazingira ya “unyanyasaji wa ndani ya chama.”

Akizungumza na wanahabari siku ya Jumatatu katika makao makuu ya Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), Kinondoni jijini Dar es Salaam, Mligo amesema kuwa ameumizwa na namna anavyotajwa kuwa chanzo cha migogoro, licha ya kuwa mmoja wa waliokibeba chama wakati wa kipindi kigumu.

“Mwaka 2019 tuliendesha CHADEMA Digital ambayo ilikuwa inasajili wanachama na kushughulikia masuala ya uchaguzi. Lakini kwenye uchaguzi wa Januari 2025, CHADEMA ilishindwa kufanya operesheni kwenye majimbo ya Makete, Wang’ing’ombe na Ludewa kwa sababu ya ukosefu wa bajeti. Mimi ndiye nilimpigia Katibu Mkuu Mnyika kuuliza sababu, na yeye akathibitisha kuwa hawana fedha,” amesema Mligo.

Kwa mujibu wa Mligo, aliamua kufadhili operesheni hiyo kwa fedha zake binafsi, akitumia zaidi ya shilingi milioni 15 kuhakikisha kuwa majimbo hayo matatu katika Mkoa wa Njombe yanashiriki mchakato wa uchaguzi wa ndani ya chama.

“Niliigharamia kwa fedha zangu hadi majimbo yanapata uongozi ambao ulipiga kura kwenye uchaguzi mkuu wa chama. Zipo kwenye kumbukumbu rasmi, hawawezi kubisha,” amesisitiza.

Hata hivyo, Sigrada alisema licha ya kujitolea kwake kwa hali na mali, amekuwa akidhihakiwa na baadhi ya wanachama na viongozi wa CHADEMA ambao, kwa maneno yake, wanajifanya kuwa wao ndio waliokifia chama kuliko wengine.

“Sasa unakutana na lugha za kienyeji sana ambazo zinataka kuonesha kwamba kuna watu wameipambania CHADEMA, kuna watu wameifia CHADEMA kuliko watu wengine, kwahiyo sisi watu wengine sio watu wa matangazo na siyo watu wa mitandaoni, ndiyo maana nikasema nikisema niliyoyafanya kwenye chama hiki halafu mtu anakuja na lugha laini kwamba Sigrada anakiua chama, unamshangaa”, ameeleza Sigrada.

Kauli ya Mligo imekuja miezi kadhaa baada ya kuripotiwa kujeruhiwa na mmoja wa walinzi wa CHADEMA wakati wa kikao cha ndani kilichoongozwa na Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, John Heche, Machi 25, 2025, mjini Njombe.

Aliyekuwa Katibu Mwenezi wa Baraza la Wanawake wa CHADEMA (BAWACHA)taifa, Bi. Sigrada Mligo, am.jpg
 
Hakuna mwanachama anaenyanyaswa hata mmoja hizo ni kauli za kujitia ujinga tu kichwani ionekane hawafurahishwi ila toka uongozi mpya ulipochaguliwa unapata misukosuko kutoka chama dola hadi sasa na kila kitu kimezuiwa kwahiyo wakisema hawafurahishwi ni ujinga wao kwa vile wameshafikia bei ya kwenda huko.
 
chadema waliobaki aili zao haziwatoshi yaani wanaendeshwa na lissu ambaye siyo mzalendo watahenya sana mwaka huu na uchaguz uko palepale
 
Kumbe bado hawajaisha.... nadhani itangazwe siku moja ya wote waliobaki waondoke kama wana Israel walivyoondoka Misri
 
Hakuna mwanachama anaenyanyaswa hata mmoja hizo ni kauli za kujitia ujinga tu kichwani ionekane hawafurahishwi ila toka uongozi mpya ulipochaguliwa unapata misukosuko kutoka chama dola hadi sasa na kila kitu kimezuiwa kwahiyo wakisema hawafurahishwi ni ujinga wao kwa vile wameshafikia bei ya kwenda huko.
Anaevaa kiatu ndie anaejua kinako mbana.

Amandla...
 
Hakuna mwanachama anaenyanyaswa hata mmoja hizo ni kauli za kujitia ujinga tu kichwani ionekane hawafurahishwi ila toka uongozi mpya ulipochaguliwa unapata misukosuko kutoka chama dola hadi sasa na kila kitu kimezuiwa kwahiyo wakisema hawafurahishwi ni ujinga wao kwa vile wameshafikia bei ya kwenda huko.
Hilo unasema wewe mtumwa usiyejua kunyanyaswa ni nini Wala upeo wa kuelewa hilo.
 
Back
Top Bottom