GE2025 Mwenezi BAWACHA, Sigrada Mligo ajiondoa CHADEMA, ahamia CHAUMMA

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Basi fumba mdomo wako kwa sababu sikukuita ukomenti nilichoandika. Hizo habari nazifuatilia hadi leo. Hakuna manyanyaso yoyote labda maneno ya kiccm mnayomezeshwa huko lumumba a kuaminishwa hayo juu ya chadema.
Natumia bamdo langu, nitacomment chochote ninachokitaka..... nyambaaaf. Hamna strategies, mnapigwa asubuhi na mapema na mtu wenu mjuaji huyo.
 
Dah!,
binti alinusurika kunyang'anywa uhai na walinzi katili sana wa heche, kwa amria ya heche, huku heche mwenyewe akishuhudia na kufurahia ukatili ambao binti huyo alikua akifanyiwa.

huenda walinzi wale katili wa heche ndio waliomdhulumu mzee kibao.
Hao wapinzi kwanini wasikamatwe,wainganishwe na waliomuua Kibao na zile silaha walizokuanazo siku wanamchukua Kibao,zichukuliwe?
 
Aliyekuwa Katibu Mwenezi wa Baraza la Wanawake wa CHADEMA (BAWACHA) taifa, Sigrada Mligo, ametangaza kujiondoa rasmi ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) akilalamikia kile alichokiita kauli za kubeza mchango wake na mazingira ya “unyanyasaji wa ndani ya chama.”

Akizungumza na wanahabari siku ya Jumatatu katika makao makuu ya Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), Kinondoni jijini Dar es Salaam, Mligo amesema kuwa ameumizwa na namna anavyotajwa kuwa chanzo cha migogoro, licha ya kuwa mmoja wa waliokibeba chama wakati wa kipindi kigumu.

“Mwaka 2019 tuliendesha CHADEMA Digital ambayo ilikuwa inasajili wanachama na kushughulikia masuala ya uchaguzi. Lakini kwenye uchaguzi wa Januari 2025, CHADEMA ilishindwa kufanya operesheni kwenye majimbo ya Makete, Wang’ing’ombe na Ludewa kwa sababu ya ukosefu wa bajeti. Mimi ndiye nilimpigia Katibu Mkuu Mnyika kuuliza sababu, na yeye akathibitisha kuwa hawana fedha,” amesema Mligo.

Kwa mujibu wa Mligo, aliamua kufadhili operesheni hiyo kwa fedha zake binafsi, akitumia zaidi ya shilingi milioni 15 kuhakikisha kuwa majimbo hayo matatu katika Mkoa wa Njombe yanashiriki mchakato wa uchaguzi wa ndani ya chama.

“Niliigharamia kwa fedha zangu hadi majimbo yanapata uongozi ambao ulipiga kura kwenye uchaguzi mkuu wa chama. Zipo kwenye kumbukumbu rasmi, hawawezi kubisha,” amesisitiza.

Hata hivyo, Sigrada alisema licha ya kujitolea kwake kwa hali na mali, amekuwa akidhihakiwa na baadhi ya wanachama na viongozi wa CHADEMA ambao, kwa maneno yake, wanajifanya kuwa wao ndio waliokifia chama kuliko wengine.

“Sasa unakutana na lugha za kienyeji sana ambazo zinataka kuonesha kwamba kuna watu wameipambania CHADEMA, kuna watu wameifia CHADEMA kuliko watu wengine, kwahiyo sisi watu wengine sio watu wa matangazo na siyo watu wa mitandaoni, ndiyo maana nikasema nikisema niliyoyafanya kwenye chama hiki halafu mtu anakuja na lugha laini kwamba Sigrada anakiua chama, unamshangaa”, ameeleza Sigrada.

Kauli ya Mligo imekuja miezi kadhaa baada ya kuripotiwa kujeruhiwa na mmoja wa walinzi wa CHADEMA wakati wa kikao cha ndani kilichoongozwa na Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, John Heche, Machi 25, 2025, mjini Njombe.
Huyu si ndio alisema kapigwa na mlinzi wa Heche, wanaccm ikiwemo Makala wakawa wanamtembelea hospitali? Yeye huko cdm wala alikuwa hatakiwi.
 
chadema waliobaki aili zao haziwatoshi yaani wanaendeshwa na lissu ambaye siyo mzalendo watahenya sana mwaka huu na uchaguz uko palepale
Wala hatutamani huo upuuzi uitwao uchaguzi.
 
Aliyekuwa Katibu Mwenezi wa Baraza la Wanawake wa CHADEMA (BAWACHA) taifa, Sigrada Mligo, ametangaza kujiondoa rasmi ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) akilalamikia kile alichokiita kauli za kubeza mchango wake na mazingira ya “unyanyasaji wa ndani ya chama.”

Akizungumza na wanahabari siku ya Jumatatu katika makao makuu ya Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), Kinondoni jijini Dar es Salaam, Mligo amesema kuwa ameumizwa na namna anavyotajwa kuwa chanzo cha migogoro, licha ya kuwa mmoja wa waliokibeba chama wakati wa kipindi kigumu.

“Mwaka 2019 tuliendesha CHADEMA Digital ambayo ilikuwa inasajili wanachama na kushughulikia masuala ya uchaguzi. Lakini kwenye uchaguzi wa Januari 2025, CHADEMA ilishindwa kufanya operesheni kwenye majimbo ya Makete, Wang’ing’ombe na Ludewa kwa sababu ya ukosefu wa bajeti. Mimi ndiye nilimpigia Katibu Mkuu Mnyika kuuliza sababu, na yeye akathibitisha kuwa hawana fedha,” amesema Mligo.

Kwa mujibu wa Mligo, aliamua kufadhili operesheni hiyo kwa fedha zake binafsi, akitumia zaidi ya shilingi milioni 15 kuhakikisha kuwa majimbo hayo matatu katika Mkoa wa Njombe yanashiriki mchakato wa uchaguzi wa ndani ya chama.

“Niliigharamia kwa fedha zangu hadi majimbo yanapata uongozi ambao ulipiga kura kwenye uchaguzi mkuu wa chama. Zipo kwenye kumbukumbu rasmi, hawawezi kubisha,” amesisitiza.

Hata hivyo, Sigrada alisema licha ya kujitolea kwake kwa hali na mali, amekuwa akidhihakiwa na baadhi ya wanachama na viongozi wa CHADEMA ambao, kwa maneno yake, wanajifanya kuwa wao ndio waliokifia chama kuliko wengine.

“Sasa unakutana na lugha za kienyeji sana ambazo zinataka kuonesha kwamba kuna watu wameipambania CHADEMA, kuna watu wameifia CHADEMA kuliko watu wengine, kwahiyo sisi watu wengine sio watu wa matangazo na siyo watu wa mitandaoni, ndiyo maana nikasema nikisema niliyoyafanya kwenye chama hiki halafu mtu anakuja na lugha laini kwamba Sigrada anakiua chama, unamshangaa”, ameeleza Sigrada.

Kauli ya Mligo imekuja miezi kadhaa baada ya kuripotiwa kujeruhiwa na mmoja wa walinzi wa CHADEMA wakati wa kikao cha ndani kilichoongozwa na Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, John Heche, Machi 25, 2025, mjini Njombe.

Nenda ila ujue hamna bunge wa kupewa... Liccm mnalotegemea linahemea icu.... Yaani kifupi wewe ushakufa kisasa... Nenda kalime parachichi huna jipya!
 
Wacha shobo zako. Ukubwa wa chadema sio wakutegemea dola ili wakubalike. Hebu jaribuni kuufanya mchezo sawa mwone ukubwa wa chadema. Mbona mnaogopa reforms za uchaguzi kama mnsukubwa wa wawanachama.
Reform zianze kwanza kwenye Chama chenu huko.
 
Zitsae hizo reforms ambazo zilikuwa hazaajanza kufanywa huko chadema baadaye mkamkamata Lissu kisa ashindwe nikukiendeleza chama.

Sasa hapo kwenye Katiba na sheria za achuguzi zinahitajika reforms ambazo zinanufaisha kila chama na mwananchi kiujumla. Reforms na taratibu za chama kila mmoja wanazao ndio maana ccm juzi walibadilisha ili Samia asipingwe na yoyote. Huu ni udikteta asiweze ushindani kwenye chama chama chake.
 
Huyu tangu lile sakata la kutengenezwa kuwa alijeruhiwa, lilikuwa ni suala la wakati. Kuondoka kwake kutakuwa ni nafuu kwa CHADEMA maana adui wa ndani ni mbaya kuliko wa nje.
Kumbe ndiye😂😂😂😊
 
Back
Top Bottom