Mwenendo wa siasa za CHADEMA na Rais samia kupitia CCM. Nani anapoteza nani anapata kati ya CDM na CCM?

system hacker

JF-Expert Member
Mar 13, 2022
426
706
Simple sana.

Anayepatia ni CDM, anayepoteza ni machawa wa CCM wala sio CCM.

Hii ni kama kusema mwenendo wa siasa hizi ni CDM vs Machawa wa CCM.

Kuna uzi humu nimeandika kwamba, adui mkubwa wa CDM ni Polisi na wala sio CCM.

Polisi kwa namna nyingine tunaweza kuwaita ni machawa wa CCM. Wapinzani huenda mbali na kuwaita PolisiCCM kwa namna wanavyotumika kufanikisha maswala ya CCM na kuwaumiza wapinzani.

Kwa mwenendo huu ni kama wanakosa ile nguvu radical waliyokuwa nayo wakati wa zile siasa za Magufuli. Watajiona sasa ni wanyonge kuwabughudhi wapinzani hasa CDM kwa kuamini kwamba viongozi wao wapo karibu sana na CCM.

Unadhani nani yupo nyuma ya siasa hizi mpya Tanzania?

Watu wawili: J. Kikwete & Abdulrahaman Kinana.

Kwanini?

1. Soma signals anazorusha Lema, Soma signals alizowahi kurusha Lissu akiwa Belgium, n.k.

2. Hao watajwa wote hapo juu ni waasisi wa siasa za mwenendo huu. Ndio kuna wakati J.K. aliitwa Rais dhaifu na wala hakumaindi hadi leo.

Ni wakati wa J.K. na Kinana ndiko upinzani iliimarika zaidi hapa nchini kuliko nyakati zote.

Je, ina maana CCM kama chama hawapotezi?

CCM wanapoteza. Kwa sababu ndani ya mfumo wa utawala na siasa nchini wapinzani ni wengi mno, lakini wanaogopa kuwa front.

Hivyo, kwa hali hii walau watapata 'relief' kwa kiasi chake na kuwa kidogo huru kutokandamiza upinzani kama ilivyozoeleka.

Kitu gani kimepangwa kwa mbali sana ambacho watu wengi hawakioni?

Hiki:

Siasa za CCM ziwe karibu na nguvu sawa na za upinzani. Ili ikitokea Kiongozi aina ya Magufuli akitwaa madaraka basi aweze kuthibitiwa ipasavyo na mfumo ulio huru wa kisiasa hasa kutoka upinzani.

Kwa maana kwamba, ujio wa aina ya urais wa Magufuli uliwatisha mno the 'senior citizens' na kuwafanya wawe wanyonge kulikopitiliza wasiamini kwamba waliwahi kuwa viongozi wakuu hapa nchini. Ilikuwa ni fedheha sana.

Swali linalowasumbua:

Je, tutafanyaje siasa za nchi yetu ili kusiwepo tena room ya marais wa aina ya Magufuli kuibuka na kuendesha nchi kwa mfumo ule?

Jibu rahisi:

Wanaamini hivi. Ni kujitahidi kuimarisha mifumo ya kisiasa ili vyama vya upinzani hususan CDM kiwe na nguvu imara kiasi kwamba akitokea Kiongozi wa juu kukengeuka basi wapinzani waweze kushughulika naye.

Hii ni kwa sababu hata kipindi cha ubabe wa Magufuli at least wapinzani walijitahidi kumkabili ingawa walikuwa na mazingira magumu zaidi. Ilhali wana CCM waliendelea kumtetea na kumpigania badala ya kumfunga speed governor. Take note of this!

Inaonekana kwamba this time around CDM itavuna wabunge wengi zaidi kuliko kipindi chochote kile.

All the best
 
Katiba Mpya ndiyo suluhisho itazaa mifumo mipya itayoiletea nchi heshima badala ya kutegemea utashi wa mtu binafsi kuongoza.Hilo ni muhimu kuliko utashi binafsi wa Rais kuongoza. CCM watakuwa wamefankiwa sana wakiruhusu Katiba mpya na kuondoa yaliyotokea nyuma maana wote CCM na CDM waliumia sana awamu ya tano.
 
Katiba Mpya itazaa mifumo mipya itayoiletea nchi heshima badala ya kutegemea utashi wa mtu binafsi kuongoza.Hilo ni muhimu kuliko utashi binafsi wa Rais. CCM watakuwa wamefankiwa sana na kuondoa yaliyotokea nyuma maana wote CCM na CDM waliumia kipindi cha tano.
Hivi hiyo Katiba mpya itakuwaje kias mnadhani itatua yote? Yapo yatakayatokana na utashi wa mtu ata zije katiba mpya 100! Kenya hapo Odinga wala hataman ata kumpa mkono Ruto ila wana Katiba mpya, kule South kuna Malema! Siasa za kinafiki kama zakina Mbowe na Zitto wala hana na wana Katiba nzuri tu!

Siasa ni itikadi, ishi katika itikadi/ iman yako sio hawa wanasiasa wetu ambao siasa nzuri na pale waahidi viti bungen then waache wale! Umewafunga midomo ila usipowapa hiv vitu mezan bas watakutangaza kuwa mbaya mpaka bas, na hapa ndipo tulipokosea kuchanganya wanasiasa na wafanyabiashara, maana watalinda biashara zao kupitia siasa, bora Azimio la Arusha lirudi maana sioni atakaebaki katika siasa.
 
Naamini kipimo cha huu urafiki ni baada ya uchaguzi, hasa utakapofika ule wakati wa kuhesabu kura, na kutangaza washindi.

Hapo kama yule mwenye polisi hatakuwa tayari kuweka mbele interest za chama chake kwa manufaa yao, basi kweli patakuwepo na urafiki usio na mashaka baina yao.

Hivyo kama hilo litatokea, pia naamini wote wawili watakuwa wamefaidi, kwasababu haki kati yao itaachwa ichukue mkondo wake, yule anayeistahili ndie atakayeipata.

Lakini kama itatokea mmojawapo akaendelea kukandamizwa na polisi, basi hapo Chadema watakuwa wamepoteza, na CCM watakuwa wamepata lakini isivyo haki.
 
Katiba mpya ije na mfumo wa serikali ya mseto kama hakuna majority bungeni.
 
Simple sana.

Anayepatia ni CDM, anayepoteza ni machawa wa CCM wala sio CCM.

Hii ni kama kusema mwenendo wa siasa hizi ni CDM vs Machawa wa CCM.

Kuna uzi humu nimeandika kwamba, adui mkubwa wa CDM ni Polisi na wala sio CCM.

Polisi kwa namna nyingine tunaweza kuwaita ni machawa wa CCM. Wapinzani huenda mbali na kuwaita PolisiCCM kwa namna wanavyotumika kufanikisha maswala ya CCM na kuwaumiza wapinzani.

Kwa mwenendo huu ni kama wanakosa ile nguvu radical waliyokuwa nayo wakati wa zile siasa za Magufuli. Watajiona sasa ni wanyonge kuwabughudhi wapinzani hasa CDM kwa kuamini kwamba viongozi wao wapo karibu sana na CCM.

Unadhani nani yupo nyuma ya siasa hizi mpya Tanzania?

Watu wawili: J. Kikwete & Abdulrahaman Kinana.

Kwanini?

1. Soma signals anazorusha Lema, Soma signals alizowahi kurusha Lissu akiwa Belgium, n.k.

2. Hao watajwa wote hapo juu ni waasisi wa siasa za mwenendo huu. Ndio kuna wakati J.K. aliitwa Rais dhaifu na wala hakumaindi hadi leo.

Ni wakati wa J.K. na Kinana ndiko upinzani iliimarika zaidi hapa nchini kuliko nyakati zote.

Je, ina maana CCM kama chama hawapotezi?

CCM wanapoteza. Kwa sababu ndani ya mfumo wa utawala na siasa nchini wapinzani ni wengi mno, lakini wanaogopa kuwa front.

Hivyo, kwa hali hii walau watapata 'relief' kwa kiasi chake na kuwa kidogo huru kutokandamiza upinzani kama ilivyozoeleka.

Kitu gani kimepangwa kwa mbali sana ambacho watu wengi hawakioni?

Hiki:

Siasa za CCM ziwe karibu na nguvu sawa na za upinzani. Ili ikitokea Kiongozi aina ya Magufuli akitwaa madaraka basi aweze kuthibitiwa ipasavyo na mfumo ulio huru wa kisiasa hasa kutoka upinzani.

Kwa maana kwamba, ujio wa aina ya urais wa Magufuli uliwatisha mno the 'senior citizens' na kuwafanya wawe wanyonge kulikopitiliza wasiamini kwamba waliwahi kuwa viongozi wakuu hapa nchini. Ilikuwa ni fedheha sana.

Swali linalowasumbua:

Je, tutafanyaje siasa za nchi yetu ili kusiwepo tena room ya marais wa aina ya Magufuli kuibuka na kuendesha nchi kwa mfumo ule?

Jibu rahisi:

Wanaamini hivi. Ni kujitahidi kuimarisha mifumo ya kisiasa ili vyama vya upinzani hususan CDM kiwe na nguvu imara kiasi kwamba akitokea Kiongozi wa juu kukengeuka basi wapinzani waweze kushughulika naye.

Hii ni kwa sababu hata kipindi cha ubabe wa Magufuli at least wapinzani walijitahidi kumkabili ingawa walikuwa na mazingira magumu zaidi. Ilhali wana CCM waliendelea kumtetea na kumpigania badala ya kumfunga speed governor. Take note of this!

Inaonekana kwamba this time around CDM itavuna wabunge wengi zaidi kuliko kipindi chochote kile.

All the best
Give and take rule is really applying but during the jpm regime, the take by force was applying
 
Tatizo kubwa ni wateuliwa na watumishi wa Umma waliopewa dhamana vyama vya upinzani vitatumia ubovu wa huduma ingawa hakuna uhakika kama wao wakipata Mamlaka watafanya nini
 
Mpaka Sasa CCM 3-0 Chadema, maana magoli yote Chadema wamejifunga.
 
CCM wanajua sana siasa. 2025 ni kama wapinzani wameamua kusiwe na uchaguzi wa rais. Ni Samia bila shaka yoyote
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom