Uchaguzi 2020 Mwelekeo wa kampeni za Uchaguzi Mkuu umedhihirisha umaskini mkubwa uliozalishwa nchini ndani ya miaka 5 ya utawala huu

share

JF-Expert Member
Nov 22, 2008
6,062
10,461
Mwezi mmoja umekatika tangu kampeni za Uchaguzi Mkuu zianze. Hali halisi inaonesha dhahiri Taifa lilivyobugikwa na umaskini uliozalishwa ndani ya miaka 5 ya utawala huu wa awamu ya tano.

Taifa limeshuhudia wagombea urais kushindwa kufanya kampeni kwa kukosa fedha, kushindwa kuandaa mabango kwa kukosa fedha, kushindwa kutumia media kwa kukosa fedha, na kadhalika.

Nchi nzima anayetamba kwa mabango na media ni Magufuli tu kwa kutumia mali ya umma ikiwemo TBC. Wananchi wanahoji iwapo hata hayo magari ya kifahari yaitwayo maV8 ya kijani kama kweli si ya serikali.

Kwa kifupi, kampeni zinaendeshwa kwa ugumu na umaskini huku CCM pekee ikitanua. Tujitafakari. Hili nalo ni JAMBO LETU.
 
JPM alidhani maflyover, mareli, ma-ndege ndio vitu vya kuombea kura. Kwa dunia ya leo hivyo vitu sio vya kutishia watu; hata watoto wanaviona kila siku kwenye Tv, simu, games nk.

Watu wanataka furaha, amani, haki, heshima, shibe - kuishi bila hofu... wameyakosa haya kwa miaka mi5.
 
Hujui hayo mango ya ccm ni kodi zetu wananchi, tangu na kua huwa naona mabango ya ccm nchi nzima Tena kipindi hichi sio mengi ka kipindi Cha jakaya
 
Hakuna Sehemu JPM anachemka Kama Kusema Mkichagua Upinzani Sitaleta Maendeleo kama Vile maendeleo ni Hisan Na hela ni zake.

Huu Ubaguzi ndoo Unaleta Chuki dhidi ya CCM yeye aseme Ninaomba Kura na mchague Wabunge na Madiwan wa CCM ila Kuanza Kuwaambia Watu eti hatoleta Maendeleo Binafsi naona Kama Anakosea Mno na Hana washauri. Ukihitaji kitu kwa kutoka kwa mtu huonyeshi kiburi unaonyesha unyenyekevu.

Magufuli amekosa hekima ya unyenyekevu ambayo kama kiongozi unatakiwa kujua ku balance sehemu ya kuonyesha uongozi na kujiweka katika nafasi ya unaowaongoza.
 
Hujui hayo mango ya ccm ni kodi zetu wananchi, tangu na kua huwa naona mabango ya ccm nchi nzima Tena kipindi hichi sio mengi ka kipindi Cha jakaya
Kuchapisha bango moja ni sh 5000 fikiria tu ni mabango mangapi yamechapishwa.
 
Na Magufuli akishinda, sehemu ambazo wabunge wa upinzani watakuwa wameshinda, hakuna kulipa Kodi.

Maana hata mkilipa, hamtaletewa maendeleo.

Kodi zote kuanzia mwaka huu, zitalipwa kwenye majimbo yenye CCM ili wapelekewe maendeleo kwa Kodi zao, siyo wapelekewe maendeleo kwa Kodi za waote huku wengine wakibaguliwa, wakati Kodi tunalipa wote.
 
Na Magufuli akishinda, sehemu ambazo wabunge wa upinzani watakuwa wameshinda, hakuna kulipa Kodi.

Maana hata mkilipa, hamtaletewa maendeleo.

Kodi zote kuanzia mwaka huu, zitalipwa kwenye majimbo yenye CCM ili wapelekewe maendeleo kwa Kodi zao, siyo wapelekewe maendeleo kwa Kodi za waote huku wengine wakibaguliwa, wakati Kodi tunalipa wote.
Kongwa na Misungwi hayajawahi kuwa majimbo ya upinzani lakini hayana maendeleo.
 
Hakuna Sehemu JPM anachemka Kama Kusema Mkichagua Upinzani Sitaleta Maendeleo kama Vile maendeleo ni Hisan Na hela ni zake.

Huu Ubaguzi ndoo Unaleta Chuki dhidi ya CCM yeye aseme Ninaomba Kura na mchague Wabunge na Madiwan wa CCM ila Kuanza Kuwaambia Watu eti hatoleta Maendeleo Binafsi naona Kama Anakosea Mno na Hana washauri.
Ukihitaji kitu kwa kutoka kwa mtu huonyeshi kiburi unaonyesha unyenyekevu.

Magufuli amekosa hekima ya unyenyekevu ambayo kama kiongozi unatakiwa kujua ku balance sehemu ya kuonyesha uongozi na kujiweka katika nafasi ya unaowaongoza.
Umeniwahi Mkuu, halafu Leo nimeanza kukuelewa, Naomba tukutane PM. Please.
 
Wewe ni mjinga!
.
Mlikuwa mnachukua fedha chafu toka kwa vibeberu vyenu!

Safari hii njia hizo zilipozibwa mkaishia kulia.
 
Daah za nini sasa wakati anaona biashara ya usafiri imedorola Duniani na mashirika mengi yatasaidiwa na serikali kuyainua huyu jamaa ni adhabu kwa Watanzania nadhani tumezidi unafiki sana
Hata sina la kusema tunamhitaji Mungu atuunganishe tumkatae wote.
 
Mkuu hali hii uionayo ni mpango madhubuti ambao ulipangwa ili kufanikisha lengo la mgombea wa ccm kupita bila kupingwa/kushinda kwa kishindo kwa zaidi ya 90%. Kufanikisha hili mipango ilikuwa;
1. Bunge kutooneshwa live
2. Kuvibana/kuvicontrol vyombo vya habari kutorusha habari za upinzani
3. Kununua wapinzani
4. Kuwaeliminate wapinzani wenye misimamo isiyoyumba
5. Kumcontrol CAG (taarifa zitolewe on favor of serikali na vyama pinzani kupokea hati chafu mfululizo)
6. Kuvinyima pesa za ndani vyama pinzani na kuzuia uingizaji wa misaada/ fedha kutoka nje kwa vyama rafiki
7. Mzee atangazwe kwa ushindi wa kishindo

Kudhihirisha hayo angalia ambayo yaliyokwisha fanyika mpaka sasa, kulikontro bunge kupitisha sheria on favor of serikali na chama tawala (hapa mifano ipo mingi ila mpango mkubwa kabisa ni kuongezewa muda wa kutawala).

Vyama vilivyoonesha msimamo ambavyo ni Chadema na AcT kukosa pesa na misaada kwaajili ya kampeni na kubwa kuliko yote ni KUPONA NA KURUDI KWA TUNDU LISSU na uungwaji mkono anaoupata toka kwa wananchi. Hili halikutegemewa kabisa na ndilo linalowaumiza kichwa watu maana walijua watakuwa na uwezo wa kumdhibiti.

Mambo ni mengi muda ni mchache, wenye kuelewa walishaelewa mpango w kuirudisha nchi kwenye chama kimoja kwakupitia mgongo fake wa demokrasia (Vyama vya upinzani vingekuwa vkle tu ambavyo vimepandikizwa na CCM tu) Usiidharau ile kauli ya CCM ITATAWALA MILELE 😀😀

Wenye kuona mbali walishaona ila kulikuwa hakuna kwa kuyasemea. Tuvute pumzi kwanza
I love you my country
 
JPM alidhani maflyover, mareli, ma-ndege ndio vitu vya kuombea kura. Kwa dunia ya leo hivyo vitu sio vya kutishia watu; hata watoto wanaviona kila siku kwenye Tv,simu,games nk
Watu wanataka furaha, amani, haki, heshima, shibe - kuishi bila hofu... wameyakosa haya kwa miaka mi5.
Wewe mjinga sana na kuchangia hoja hujui na ni mshamba sana. Yaani kwa akili yako ilivyo ndogo unathuburu kuchanhia hoja kwa kusema nakunukuu " hata watoto wanavio na kila siku kwenye TV, simu, games nk..."

Nikuambia kitu kimoja ambacho unatakiwa kukijua. Kuviona kwenye TV na Media au divices nyingine hiyo ni fictive na sio real. Hivi sasa watoto wanaviona real na live. Wana vif-eel na kuvishudua.

Nakumbuka kabla sijaanza kujifunza neno snow shuleni kwenye Geography, tayari nilikuwa najua kinadharia nini maana ya snow na faida na hasara zake, kwa sababu baba yangu nikiwa kijana mdogo alipata bahati ya kwenda nchini Sweeden kusoma.

Alipo rudi alituonyesha picha nyingi za slides akiwa kwenye snow na mambo mengine mengi yaliyo husu snow akiwa huko. Pamoja na hayo yote kuyajua nakuambia kuwa nilikuwa sija i-feel snow mpaka mimi mwenyewe nilipo pata bahaati ya kwenda Ulaya.

Maelezo yote mzee wangu aliyo nieleza kuhusu snow sio kabisa na hali ile ambayo mimi personally niliishuhudia. Ilikuwa kitu kingine kabisa.

Kwa hiyo acha kufanganya watu hapa. Mambo kama hayo nenda ukamweleze nyanya yako ndiye atakuelewa, lakini sio watu tuliopata exposure kama sisi.

Kwenye fikra zangu unaonyesha jinsi gani wewe ulivyo kuwa na elimu ya ngumbaru. Mtu ambaye inaonekana hujui kitu na hujui kuwaza na kupima kama unalo lisema lina maana au la hasha.

Kusema ukweli huna maana na inaonyesha hujaenda shule. Na kama unawadanganya marwfiki zako kuwa ulienda shule basi ulie da kuyaangali majengo na kuta za darasani kwako. Wewe ama kwa hakika ni ZERO BRAIN!

Nibhekushuri ufute ulixho kiandika maana unajiaibisha mwenyewe.
 
Back
Top Bottom