Uchaguzi 2020 Mwelekeo wa kampeni za Uchaguzi Mkuu umedhihirisha umaskini mkubwa uliozalishwa nchini ndani ya miaka 5 ya utawala huu

Na Magufuli akishinda, sehemu ambazo wabunge wa upinzani watakuwa wameshinda, hakuna kulipa Kodi.

Maana hata mkilipa, hamtaletewa maendeleo.

Kodi zote kuanzia mwaka huu, zitalipwa kwenye majimbo yenye CCM ili wapelekewe maendeleo kwa Kodi zao, siyo wapelekewe maendeleo kwa Kodi za waote huku wengine wakibaguliwa, wakati Kodi tunalipa wote.
Usipolipa kodi si ni jela tu
 
Hakuna Sehemu JPM anachemka Kama Kusema Mkichagua Upinzani Sitaleta Maendeleo kama Vile maendeleo ni Hisan Na hela ni zake.

Huu Ubaguzi ndoo Unaleta Chuki dhidi ya CCM yeye aseme Ninaomba Kura na mchague Wabunge na Madiwan wa CCM ila Kuanza Kuwaambia Watu eti hatoleta Maendeleo Binafsi naona Kama Anakosea Mno na Hana washauri.
Ukihitaji kitu kwa kutoka kwa mtu huonyeshi kiburi unaonyesha unyenyekevu.

Magufuli amekosa hekima ya unyenyekevu ambayo kama kiongozi unatakiwa kujua ku balance sehemu ya kuonyesha uongozi na kujiweka katika nafasi ya unaowaongoza.
Mpaka kuwa na guts za kutoa kauli kama hiyo bado anaishi katika mipango iliyokuwa imepangwa ya kumtangaza yeye mshindi no matter what. Hii maanaake wananchi hawana nafasi ya kumchagua kiongozi wao mkuu wa nchi bali wabunge na madiwani. Uchaguzi ulikuwa unachukulika kama kiini macho kuwahadaa wananchi na nchi hisani +mashirika ya kimataifa yanayotaka demokrasia Afrika.
Tundu Lissu anachukuliwa kama tishio la kuzuia mipango hii isiendelee. Akiendelea kukaza na kutoa elimu ya uraia juu ya nguvu ya wananchi katika maamuzi ya mwisho. Mengi yatatokea na yanabashirika mpaka sasa
 
Mpaka kuwa na guts za kutoa kauli kama hiyo bado anaishi katika mipango iliyokuwa imepangwa ya kumtangaza yeye mshindi no matter what. Hii maanaake wananchi hawana nafasi ya kumchagua kiongozi wao mkuu wa nchi bali wabunge na madiwani. Uchaguzi ulikuwa unachukulika kama kiini macho kuwahadaa wananchi na nchi hisani +mashirika ya kimataifa yanayotaka demokrasia Afrika.
Tundu Lissu anachukuliwa kama tishio la kuzuia mipango hii isiendelee. Akiendelea kukaza na kutoa elimu ya uraia juu ya nguvu ya wananchi katika maamuzi ya mwisho. Mengi yatatokea na yanabashirika mpaka sasa
Mungu mbariki Tundu Lissu.
 
Huoni kama utakuwa at disadvantage zaidi zikiwemo harrassment za polisccm
Mara 100 ya hizo harassment, kuliko nitoe Kodi, lakini nitengwe kisa nilichagua upinzani.

Na siku hizi nikienda kununua kitu, hata huwa sidai risti ya EFD. Zamani ilikuwa lazima nidai risti tena ile isiyochakachuliwa.

Si anashindana na wananchi, wacha tumuonyeshe makali.
 
Hujui hayo mango ya ccm ni kodi zetu wananchi, tangu na kua huwa naona mabango ya ccm nchi nzima Tena kipindi hichi sio mengi ka kipindi Cha jakaya
Kwanza nataka kujua maeneo ya umma walimoweka mabango mfano kwenye taa za barabarani kwa mijini wamelipia matangazo kwa manispaa na TRA au ?
 
JPM alidhani maflyover, mareli, ma-ndege ndio vitu vya kuombea kura. Kwa dunia ya leo hivyo vitu sio vya kutishia watu; hata watoto wanaviona kila siku kwenye Tv,simu,games nk
Watu wanataka furaha, amani, haki, heshima, shibe - kuishi bila hofu... wameyakosa haya kwa miaka mi5.
Hata kijijini kwake Chato hakuna wa kutishika na hayo ma vitu,huko ulaya mbali tunasafiri na kuyaona hayo anayodai yeye kwenye nchi nyingi za kiafrika Kama Ghana,Nigeria,Ivory Coast,Kenya,Angola na hata Uganda Wana express road kubwa na nzuri ya njia sita kutoka Entebe Hadi Kampala,sasa anatutisha na kibaha hata hauishi.
Kwa miaka yake yote 5 Tzn inaongoza kwa kuwa na watu wasio na Furaha kwa sababu ya ugumu wa maisha,vijana wanazeeka kabla ya umri wao Hadi ndoa zinayumba kisa uchumi afu uje kuchagua mtu katili asiyejali labda uwe umerogwa.
 
Mwezi mmoja umekatika tangu kampeni za Uchaguzi Mkuu zianze. Hali halisi inaonesha dhahiri Taifa lilivyobugikwa na umaskini uliozalishwa ndani ya miaka 5 ya utawala huu wa awamu ya tano.

Taifa limeshuhudia wagombea urais kushindwa kufanya kampeni kwa kukosa fedha, kushindwa kuandaa mabango kwa kukosa fedha, kushindwa kutumia media kwa kukosa fedha, na kadhalika.

Nchi nzima anayetamba kwa mabango na media ni Magufuli tu kwa kutumia mali ya umma ikiwemo TBC. Wananchi wanahoji iwapo hata hayo magari ya kifahari yaitwayo maV8 ya kijani kama kweli si ya serikali.

Kwa kifupi, kampeni zinaendeshwa kwa ugumu na umaskini huku CCM pekee ikitanua. Tujitafakari. Hili nalo ni JAMBO LETU.



Kuwachagua tena CCM ni kuwapa jeuri ya kuendelea kutunyanyasa na kutuibia huku tukiwasujudia,kuwaabudu na kuwanyenyekea wezi . Watu waliojiuzia mali zote za umma zikiwemo nyumba ,wanamiliki karibu majengo yote ya kifahari nchini halafu wanatudharau na kuwatumia wakubwa wachache wa Vyombo vya dola kujiweka madarakani. CCM kule zanzibar inatumia Risasi kuwawekea wazanzibar Rais aliyelewa mali nla madaraka tangu baba yake.
Hii sasa ni vita kati ya mabepari wa nchi hii na maskini. Mabepari wengi ambao wanashikilia mafaraka ndani ya CCM wanatumia nguvu kubwa kuendelea kutafuna mali za umma.
Labda tujiulize :Hivi JPM na Hussein Mwinyi wakikosa Kura na wakakubali watapungukiwa nini wao kama wao na familia zao? Wakekosa nini hapa duniani ambacho Mungu hajawapa
Kama ni mali wanazo nyingi sana walizozipata kupitia madaraka na vyeo walivyopata kwa zaidi ya miaka 25 . Je,wanataka nini mpaka watumie dhulma na risasi kusalia kwenye madaraka? Kwa nini wanataka kutumia majeshi ,rushwa , vitisho ,chuki na Tume ya Uchaguzi ili tu waendelee kufaidila Kodi za watanzania wote?
Kwa nini wasiweke mifumo ya haki ili washinde na kutawala kwa Haki ili wapate mema ya dunia hii leo na kule Ahera pia wapate thawabu??
Ama kweli kizazi hiki kimebahatika kuwaona wakina Farao kwa macho.

Dhulma zilizofanyika kwenye serikali za mitaa na kwenye uchaguzi huu kwa kuwaengua wapinzani tuu kwenye uchaguzi ndizo zinaxopelekea watu wawe wanajiandaa kukabiliana na dhulma kuu inayopangwa na Polepole,Mdhulumaji mkuu Bashiru na Tume ya uchaguzi. Hawa watu watatuvurugia nchi yetu kwa sababu ya uroho wao baada ya kuonja ladha ya kujizolea mapesa ya walipa kodi na kuona ladha ya utajiri wa bure bila kupata msoto wa kibiashara na kulipa makodi zaidi ya kudhulumu wapiga kura.
 
Sawa kabisa mkuu hii kweli ni hoja ya mjadala! Tena wakati vyama vingine vinalia ukata huu mkali, CCM inatanua inavyotaka, imetapanya wapiga kampeni nchi nzima wakibebwa kwa misafara mikubwa, huku wengine wakitumia helikopta na mbaya zaidi hali hii ngumu inatokea wakati CCM hiyohiyo na serikali yake wanajinadi kuwa wameifikisha nchi kwenye uchumi wa kati! Nafikiri huu utakuwa ni uchumi wa kati kwa CCM pekeake maana hata mitaani wananchi wanalalamika hali ngumu mno ya maisha! Hebu tuzidishe SARA na MAOMBI ili Mwenyezi Mungu akalikombowe taifa letu hapo October 28 kutoka kwenye kikundi cha watu wachache wanaofaidi peke yao rasimali za nchi yetu!
 
JPM alidhani maflyover, mareli, ma-ndege ndio vitu vya kuombea kura. Kwa dunia ya leo hivyo vitu sio vya kutishia watu; hata watoto wanaviona kila siku kwenye Tv, simu, games nk.

Watu wanataka furaha, amani, haki, heshima, shibe - kuishi bila hofu... wameyakosa haya kwa miaka mi5.
Ungekuwa unawasikia jinsi watu wanavyozungumzia kuhusu hizi barabara sidhani kama ungeandindika hayo uliyoandika,njoo uwasikilize watu huku mitaani.
 
Hakuna Sehemu JPM anachemka Kama Kusema Mkichagua Upinzani Sitaleta Maendeleo kama Vile maendeleo ni Hisan Na hela ni zake.

Huu Ubaguzi ndoo Unaleta Chuki dhidi ya CCM yeye aseme Ninaomba Kura na mchague Wabunge na Madiwan wa CCM ila Kuanza Kuwaambia Watu eti hatoleta Maendeleo Binafsi naona Kama Anakosea Mno na Hana washauri. Ukihitaji kitu kwa kutoka kwa mtu huonyeshi kiburi unaonyesha unyenyekevu.

Magufuli amekosa hekima ya unyenyekevu ambayo kama kiongozi unatakiwa kujua ku balance sehemu ya kuonyesha uongozi na kujiweka katika nafasi ya unaowaongoza.
Hivyo vitu(hekima na unyenyekevu) hata Lissu hana na ndio maana wakati mwengine huwa anaropoka tu kwa kukosa hekima ila nyie mnamsifu kuwa ni msema ukweli ni shujaa.
 
2494093_magu.jpeg
 
Back
Top Bottom