Mioyo ya Watanzania inaumia kwa uchungu mkubwa inaposikia habari za Ubadhirifu wa Fedha za Umma

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,272
9,716
Ndugu zangu Watanzania,

Nimeona hisia kalia sana, maumivu makubwa sana, uchungu mkubwa sana wa Watanzania huku mitaani kwangu wanapoendelea kusikia na kufuatilia kile kinachoendelea katika bunge letu pale Dodoma juu ya ubadhirifu wa pesa za umma.

Wanaongea kwa hisia na uchungu mkubwa, wanaongea huku nyuso zao zikiwa na simanzi, kukata tamaa, kulowa na kuvunjika moyo juu ya Watanzania wenzetu walioamua kutumia ofisi za umma kujitajirisha na kujineemesha huku nyuma kukiwa na kundi la Watanzania wakiteseka hata kupata tu milo mitatu kwa siku moja.

Wakati tunasikia habari za ubadhirifu huo kuna kundi kubwa la vijana waliomaliza vyuo vikuu hawana ajira mpaka muda huu, hawana mbele wala nyuma, wanashindwa kufanya shughuli za kilimo kwa kuwa hata hela ya mbolea ni shida kwao, wamebaki wanahangaika mitaani kufanya vibarua vya kinyonyaji ili tu wapate chochote cha kukimu maisha yao.

Wapo vijana utawakuta wanabeba cement kwa shilingi mia kwa mfuko mmoja wa kilo 50 ili walipe kodi za nyumba, wapo vijana wanabeba zege licha ya kuwa na vyeti safi katika makabati yao, wapo vijana wanadamka alfajiri kwenda kufanya vibarua vya kulima ili wapate fedha za kuendeshea maisha yao.

Sasa iweje mtu aliyepata bahati ya kuajiriwa serikalini na kulipwa mshahara na marupurupu manono na mwenye mtaji wa kutosha ashindwe kuridhika na kipato chake mpaka aanze kuiba? Nani katuroga Watanzania? Kwanini hatuna huruma, aibu wala hofu ya mwenyezi Mungu? Nani atazikwa na pesa? Nani kaburi lake litapambwa kwa pesa?

Unaanzia wapi kutafuna pesa za umma mamilioni kwa mamilioni wakati mpaka sasa kuna wakulima hawaelewi hata watapata wapi pesa za kununulia mbolea? Wakati kuna watu wanakosa hata pesa ya kukata bima ya afya ili wapate matibabu wakiugua? Wakati kuna watoto wa maskini wanashindwa hata kupata uji wa lishe? Wakati kuna watoto yatima wanashindwa hata kununua mavazi na kupata milo mitatu ya chakula iliyo bora?

Inatuma ujumbe gani kwa Watanzania wanyonge na maskini? Inawafundisha nini wanajeshi wanaokesha mipakani wakilinda mipaka ya Taifa letu usiku na mchana huku wakiwa wamesaini kiapo cha kifo kwa ajili ya kupigania, kulinda na kutetea Taifa letu? Inatuma ujumbe gani kwa manesi, wakunga, wauguzi wanaokesha mahospitalini kuokoa maisha ya Watanzania wenzetu katika mazingira ya kujitoa na kujitolea?

Inatoa ujumbe gani kwa walimu huko Mbozi vijijini waliojitolea kufundisha watoto wa kitanzania? Inatuma ujumbe gani kwa vijana waliomaliza vyuo vikuu na hawana ajira? Inatuma ujumbe gani kwa askari polisi wanaokesha katika giza na mvua usiku kucha wakifanya doria na wakipambana na majambazi hatari kwa ajili ya kuyaangamiza ili Watanzania tuwe salama sisi na mali zetu?

Ni vipi Watanzania wataelewa neno uzalendo? Watatafsiri vipi maana ya uzalendo? Pesa hizo si zingelipa wafanyabiashara na wakulima walioiuzia serikali mahindi yao? Si ingeiwezesha serikali kununua mahindi kutoka kwa mkulima na hivyo kumuokoa na kupata hasara? Si ingejenga miundombinu ya barabara,vituo vya afya, usambazaji wa maji safi na salama?

Si ingetolewa hata kama Ruzuku kwa nishati ya mafuta ili yashuke zaidi na zaidi na hivyo kupunguza hata kiwango cha Nauli na gharama za usafirishaji? Si ingetolewa kama mikopo kwetu vijana tukapata hata hela ya mbolea pamoja na mbegu bora za mahindi?

Hatujasikia watu wakitelekeza wagonjwa mahospitalini? Hatujasikia watu wakishindwa kukomboa miili ya wapendwa wao waliofariki hospitalini kwa kukosa pesa ya kulipia huduma za matibabu japo matibabu hayakuokoa uhai wa wapendwa wao?

Mnafikiri ni kwanini inatokea hivyo kama siyo umaskini wa watu kushindwa gharama za matibabu mpaka kuamua kutekeleza wagonjwa wao? Unafikiri kwanini watu wanashindwa kulipa gharama za matibabu ili wachukue miili ya wapendwa wao?

Jibu ni kwa kuwa ni umaskini ndio unakuwa umechagia hali hiyo. Unakuta familia imeuza kila kitu na kila rasilimali iliyokuwepo nyumbani mpaka kufikia hatua kukosa cha kuuza na hivyo kushindwa na kuishiwa na pumzi ya kuendelea kugharamia huduma za mgonjwa wao.

Kwanini viongozi wetu na wale waliopewa dhamana mnashindwa kutambua haya kwa kuwa waaminifu kwa pesa za umma? Kwanini hamna huruma katika ofisi za umma kwa kuzitendea haki? Kwanini msifanye kazi kwa uzalendo na upendo kwa Eatanzania? Mnajuwa ni kiasi gani tunaumia watanzania? Mnajuwa ni kiasi gani mnawaumiza na kuwasononesha Watanzania?

Mtu anaiba halafu anaona sawa tu? Sifa tu? Ufahari tu? Hivi mnajua maisha ya Watanzania wanyonge katika kupata milo yao? Mnajua adha za wakulima mashambani? Mnajuwa muda wanaoamka kwenda shambani? Mnajua wengine wanakoswa koswa hadi kung'atwa na nyoka? Mnajuwa wapo vijana wapo tayari kufanya kazi hata kwa elfu tatu kwa siku? Sasa kwanini ninyi hamliziki? Hivi mnaweza kuvaa viatu vya Watanzania wa huku mitaani tukisema tubadilishane viatu? Anayeweza aniambiea.

Kuondoa masikitiko, maumivu, machungu, machozi, kudumisha uzalendo kwa Watanzania ni lazima hatua kali za kisheria na kiuwajibikaji zichukuliwe haraka sana kwa wale wote waliohusika moja kwa moja au kwa kushindwa kuchukua hatua dhidi ya ubadhirifu wa pesa za umma.

Kutokufanya hivyo italeta picha mbaya kwa Watanzania na kuiweka serikali katika wakati mgumu wa kutokuaminika machoni pa Watanzania na kukosa ushirikiano kutoka kwa Watanzania, lakini pia itashusha morali ya kazi kwa watumishi wengine kama vile wanajeshi, manesi, wauguzi, waalimu, nk, wanaofanya kazi kwa uzalendo na kujituma kwa ajili ya Taifa letu.

Tusiwakatishe tamaa Watanzania kwa ajili ya watu wachache walioamua kuwa waroho na wenye kukosa uzalendo kwa Taifa letu. Tuwafute machozi Watanzania kwa kuwachukulia hatua hawa wabadhirifu.

Kazi iendelee, mama ametufikia na kuwafikia Watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya Watanzania wanyonge wasio na sauti.

Lucas Hebel mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
 
Kwa hiyo siku hizi umekuwa msemaji wa Watanzania! Juzi ulikuwa msemaji wa Chadema. Kabla ya hapo, umekuwa msemaji wa Samia na Tulia!! Kweli kazi unayo.
Mzalendo hachagui kuusema ukweli na hana mipaka ya kuusema ukweli maana ukweli .ndio maana hata wewe ukikosea nakukosoa na ukifaya vizuri nakupongeza bila kujali wewe ni nani.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Nimeona hisia kalia sana,maumivu makubwa sana,uchungu mkubwa sana wa watanzania huku mitaani kwangu wanapoendelea kusikia na kufuatilia kile kinachoendelea katika bunge letu pale Dodoma juu ya ubadhirifu wa pesa za umma, wanaongea kwa hisia na uchungu mkubwa,wanaongea huku nyuso zao zikiwa na simanzi,kukata Tamaa, kulowa na kuvunjika moyo juu ya watanzania wenzetu walioamua kutumia ofisi za umma kujitajirisha nakujineemesha huku nyuma kukiwa na kundi la watanzania wakiteseka hata kupata tu milo mitatu kwa siku moja.

wakati tunasikia habari za ubadhirifu huo kuna kundi kubwa la vijana waliomaliza vyuo vikuu hawana ajira bado mpaka muda huu,hawana mbele wala nyuma,wanashindwa kufanya shughuli za kilimo kwa kuwa hata hela ya mbolea ni shida kwao,wamebaki wanahangaika mitaani kufanya vibarua vya kinyonyaji ili tu wapate chochote cha kukimu maisha yao.wapo vijana utawakuta wanabeba cement kwa shilingi mia kwa mfuko mmoja wa kilo 50 ili walipe kodi za nyumba,wapo vijana wapo wanabeba zege licha ya kuwa na vyeti safi katika makabati yao,wapo vijana wanadamka alfajiri kwenda kufanya vibarua vya kulima ili wapate fedha za kuendeshea maisha yao.

Sasa iweje mtu aliyepata bahati ya kuajiliwa serikalini na kulipwa mshahara na marupurupu manono na mwenye mtaji wa kutosha ashindwe kuridhika na kipato chake mpaka aanze kuiba? Nani katuroga watanzania? Kwanini hatuna huruma wala aibu wala hofu ya mwenyezi Mungu? Nani atazikwa na pesa? Nani kaburi lake litapambwa kwa pesa?

Unaanzia wapi kutafuna pesa za umma mamilioni kwa mamilioni wakati mpaka sasa kuna wakulima hawaelewi hata watapata wapi pesa za kununulia mbolea? Wakati kuna watu wanakosa hata pesa ya kukata bima ya afya ili wapate matibabu wakiugua? Wakati kuna watoto wa maskini wanashindwa hata kupata uji wa lishe? Wakati kuna watoto yatima wanashindwa hata kununua mavazi na kupata milo mitatu ya chakula iliyo bora?

Inatuma ujumbe gani kwa watanzania wanyonge na maskini? Inawafundisha nini wanajeshi wanaokesha mipakani wakilinda mipaka ya Taifa letu usiku na mchana huku wakiwa wamesaini kiapo cha kifo kwa ajili ya kupigania, kulinda na kutetea Taifa letu? Inatuma ujumbe gani kwa manesi ,wakunga ,wauguzi wanaokesha mahospitalini kuokoa maisha ya watanzania wenzetu katika mazingira ya kujitoa na kujitolea? Inatoa ujumbe gani kwa walimu huko Mbozi vijijini waliojitolea kufundisha watoto wa kitanzania? Inatuma ujumbe gani kwa vijana waliomaliza vyuo vikuu na hawana ajira? Inatuma ujumbe gani kwa askari polisi wanaokesha katika giza na mvua usiku kucha wakifanya doria na wakipambana na majambazi hatari kwa ajili ya kuyaangamiza ili watanzania tuwe salama sisi na mali zetu?

Ni vipi watanzania wataelewa neno uzalendo? Watatafsiri vipi maana ya uzalendo? Pesa hizo si zingelipa wafanyabiashara na wakulima walioiuzia serikali mahindi yao? Si ingeiwezesha serikali kununua mahindi kutoka kwa mkulima na hivyo kumuokoa na kupata hasara? Si ingejenga miundombinu ya barabara,vituo vya afya, usambazaji wa maji safi na salama? Si ingetolewa hata kama Ruzuku kwa nishati ya mafuta ili yashuke zaidi na zaidi na hivyo kupunguza hata kiwango cha Nauli na gharama za usafirishaji? Si ingetolewa kama mikopo kwetu vijana tukapata hata hela ya mbolea pamoja na mbegu bora za mahindi?

Hatujasikia watu wakitelekeza wagonjwa mahospitalini? Hatujasikia watu wakishindwa kukomboa miili ya wapendwa wao waliofariki hospitalini kwa kukosa pesa ya kulipia huduma za matibabu japo matibabu hayakuokoa uhai wa wapendwa wao? Mnafikiri ni kwanini inatokea hivyo kama siyo umaskini wa watu kushindwa gharama za matibabu mpaka kuamua kutekeleza wagonjwa wao? Unafikiri kwanini watu wanashindwa kulipa gharama za matibabu ili wachukue miili ya wapendwa wao? Jibu ni kwa kuwa ni umaskini ndio unakuwa umechagia hali hiyo.unakuta familia imeuza kila kitu na kila rasilimali iliyokuwepo nyumbani mpaka kufikia hatua kukosa cha kuuza na hivyo kushindwa na kuishiwa na pumzi ya kuendelea kugharamia huduma za mgonjwa wao.

Kwanini viongozi wetu na wale waliopewa dhamana mnashindwa kutambua haya kwa kuwa waaminifu kwa pesa za umma? Kwanini hamna huruma katika ofisi za umma kwa kuzitendea haki? Kwanini msifanye kazi kwa uzalendo na upendo kwa watanzania? Mnajuwa ni kiasi gani tunaumia watanzania? Mnajuwa ni kiasi gani mnawaumiza na kuwa sononesha watanzania? Mtu anaiba halafu anaona sawa tu? Sifa tu? Ufahari tu? Hivi mnajuwa maisha ya watanzania wanyonge katika kupata milo yao? Mnajuwa adha za wakulima mashambani? Mnajuwa muda wanaoamka kwenda shambani? Mnajuwa wengine wanakoswa koswa hadi kung'atwa na nyoka? Mnajuwa wapo vijana wapo tayari kufanya kazi hata kwa elfu tatu kwa siku? Sasa kwanini ninyi hamliziki? Hivi mnaweza kuvaa viatu vya watanzania wa huku mitaani tukisema tubadilishane viatu? Anayeweza aniambiea.

Kuondoa masikitiko,maumivu,machungu, machozi,kudumisha uzalendo kwa watanzania ni lazima hatua kali za kisheria na kiuwajibikaji zichukuliwe haraka sana kwa wale wote waliohusika moja kwa moja au kwa kushindwa kuchukua hatua dhidi ya ubadhirifu wa pesa za umma .kutokufanya hivyo italeta picha mbaya kwa watanzania na kuiweka serikali katika wakati mgumu wa kutokuaminika machoni pa watanzania na kukosa ushirikiano kutoka kwa watanzania ,lakini pia itashusha morali ya kazi kwa watumishi wengine kama vile wanajeshi,manesi,wauguzi,waalimu n.k wanaofanya kazi kwa uzalendo na kujituma kwa ajili ya Taifa letu.tusiwakatishe Tamaa watanzania kwa ajili ya watu wachache walioamua kuwa waroho na wenye kukosa uzalendo kwa Taifa letu. Tuwafute machozi watanzania kwa kuwachukulia hatua hawa wabadhirifu.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
Huko chamani kuanzia mwenyekiti wenu na mawaziri wake wote wezi wa pesa za walipa kodi...jpm alimfukuza mpka CAG kuficha ufisadi wake,waliokula hela za sgr ni awamu ya jpm,huyu mama yeye nae kaja kumalizia kula mpka kuuza bandari.
Hicho chama chakavu ni ukoo wa panya
 
Huko chamani kuanzia mwenyekiti wenu na mawaziri wake wote wezi wa pesa za walipa kodi...jpm alimfukuza mpka CAG kuficha ufisadi wake,waliokula hela za sgr ni awamu ya jpm,huyu mama yeye nae kaja kumalizia kula mpka kuuza bandari.
Hicho chama chakavu ni ukoo wa panya
Rais samia ni msafi na mwenye kuendesha serikali yake kwa uwazi,ndio maana unaona hata ripoti ya CAG ikiweka wazi kila kitu kichofanyika ili kila mtu abebe msalaba wake mwenyewe kulingana na matendo yake .
 
Angalao leo umejitutumua,lakini kaa ukijua hizo Buku tatu leo hawatumi.
Mimi huwa siandiki hapa jukwaani kwa malipo kutoka kwa mtu yeyote yule na wala silipwi na mtu yeyote yule kwa ajili ya kuandika hapa jukwaani. Mimi ni mtu huru mwenye kuzungumza ukweli bila kujali ukweli huo utapokelewa vipi na watu .
 
Ccm wote ni wale wale. Lao ni moja tu. Hapo watapiga piga kelele,kuwazuga wananchi,lakini baadae wanapongezana kuwazuga wananchi. Lakini nani wa kumwajibisha mwenzie ambae ni msafi?. Hapo wananchi tu ndio waamke watafute namna ya kuwawajibisha hawa. Vinginevyo tusitegemee chochote,kila mwaka utakuja na report ya ukwapuaji mpya. Hapo ndipo tulipofikia kama nchi. Nchi inaliwa
 
Ccm wote ni wale wale. Lao ni moja tu. Hapo watapiga piga kelele,kuwazuga wananchi,lakini baadae wanapongezana kuwazuga wananchi. Lakini nani wa kumwajibisha mwenzie ambae ni msafi?. Hapo wananchi tu ndio waamke watafute namna ya kuwawajibisha hawa. Vinginevyo tusitegemee chochote,kila mwaka utakuja na report ya ukwapuaji mpya. Hapo ndipo tulipofikia kama nchi. Nchi inaliwa
Tuwe na imani na tuiamini serikali kuwa itachukua hatua kali kwa wahusika wote waliofanya ubadhirifu wa pesa za umma.
 
Mzalendo hachagui kuusema ukweli na hana mipaka ya kuusema ukweli maana ukweli .ndio maana hata wewe ukikosea nakukosoa na ukifaya vizuri nakupongeza bila kujali wewe ni nani.
Siku utakapo fanikiwa kulitofautisha neno uzalendo dhidi ya maneno mengine mfano uchumia tumbo, unafiki, uchawa, ujinga, nk hakika utanishukuru sana.
 
Ccm ipo siku isiyo na jina kutakuwa na anguko lenu kubwa sana halafu hayo mapesa yenu ya wizi hayatawasidia. Kama mti mbichi ulitendwa vile, sijui ninyi mti mkavu kama mtayavumlia hayo MAPIGO.
 
Tuwe na imani na tuiamini serikali kuwa itachukua hatua kali kwa wahusika wote waliofanya ubadhirifu wa pesa za umma.
Kuna serikali ya kuwa na Imani nayo hapo? Wananchi wa leo sio wale wa siku za miaka ya nyuma. Hawa wanajua kila kitu. Ni vile tu hawana uwezo wafanyeje?.
 
Back
Top Bottom