Mwekezaji na Mbunge wamliza bibi ni kuhusu ghorofa lililopo Kariakoo, aomba Serikali Kuu imsaidie apate haki yake

Mwekezaji na Mbunge wamliza bibi ni kuhusu ghorofa lililopo Kariakoo, aomba Serikali Kuu imsaidie apate haki yake

Kayugumis

Senior Member
Joined
Jun 6, 2022
Posts
140
Reaction score
126
BIBI kikongwe Khadija Isihaka (84), amemwangukia Rais Samia Suluhu Hassan,akimsihi aingilie kati mgogoro wake na mwekezaji Munir Harbesh, anayelalamikiwa kuvunja mkataba wao wa kumiliki jengo la ghorofa kwa ubia.

Bibi Khadija anasema wakati akihangaika kusaka haki yake kwenye uwekezaji huo wa ubia, aliunganishwa na mbunge wa zamani wa jimbo la Kijini, mkoa wa Kaskazini Unguja, Yahya Ali Khamis (CCM), akiamini atamsaidia kutatua changamoto hiyo, badala yake aliishia kutapeliwa sh milioni 22.

Akizungumza kwa uchungu huku akitokwa machozi, kikongwe huyo alimwomba Rais Samia kuingilia kati mgogoro wake na mwekezaji huyo pamoja na utapeli anaodai kufanyiwa na mbunge huyo wa zamani.

Anasema umri wake umeenda sana na anakabiliwa na maradhi, lakini anashindwa hata kupata Bima ya afya na hata kununua gari la kumpeleka hospitali wakati kitega uchumi chake kinamnufaisha raia huyo wa Yemen, hivyo anaomba Rais Samia aingilie kati.

"Awamu ya kwanza tulikubaliana ajenge ghorofa saba , mimi nipewe ghorofa tatu na yeye apate ghorofa nne, tulikubalibaliana nipewe fremu tatu za maduka na chumba cha stoo, nilipwe sh 300, 000 za kujikimu kila mwezi, lakini nimeambulia kupewa ghorofa moja tu tena ya juu hata lifti haina, makubaliano mengine yote hakuna".

Kuhusu mbunge huyo wa zamani wa Kijini, anasema alijigamba kuwa anaweza kumsaidia kupata haki yake, lakini aliishia kutapeliwa sh milioni 22, hivyo anataka fedha zake zirejeshwe mara moja.

Alisisitiza kumlilia Rais Samia angilie kati kwani ni mtetezi wa wanyonge wanaonewa kama yeye na anajua hana muda mrefu wa kuishi duniani, hivyo anataka kuacha urithi kwa watoto wake.

Mbunge huyo wa zamani alipoulizwa alikiri kupokea kiasi hicho cha fedha lakini alidai zilitumika kwa kazi ya kufuatilia haki za Bibi Khadija na kazi hiyo bado inaendelea ikiwemo kutaka kufungua kesi.

Mwekezaji kwa upande wake, amesema hataki kufuatiliwa na hana muda wa kuzungumzia malalammiko ya Khadija huku akitoa maneno ya kejeli na dharau.

CHANZO: RAIA MWEMA
 
Tatizo watu wengi hawana Elimu katika maswala ya uwekezaji hawataki kupitia kwenye njia sahihi matokeo yake ndiyo hayo, kwani hakukuwa na mkataba wa maandishi?
 
Tatizo watu wengi hawana Elimu katika maswala ya uwekezaji hawataki kupitia kwenye njia sahihi matokeo yake ndiyo hayo, kwani hakukuwa na mkataba wa maandishi? Cha pili bibi wakati wenzako wananunua uchawi wewe ulikuwa wapi? Leo hii ungempiga na kitu adabu imshike
 
Kwa mkataba huo ulitakiwa uwe na mwanasheria/wanasheria imara. Huwezi kufanya makubaliano kizembe kizembe kwenye property kama hiyo!
 
Anasema umri wake umeenda sana na anakabiliwa na maradhi, lakini anashindwa hata kupata Bima ya afya na hata kununua gari la kumpeleka hospitali wakati kitega uchumi chake kinamnufaisha raia huyo wa Yemen, hivyo anaomba Rais Samia aingilie kati.
Si ujombani huko Yemen?

Still atasimama na wajomba hakuna kitu atasaidia hapo,yeye anajihesabia siyo mwafrika kwanza.
 
nimeuliza,huyo mama ana watoto ?????

ova
 
nimeuliza,huyo mama ana watoto ?????

ova
Swali halijakaa kiinterogative hili, bali limekaa kistatement, hapo hakuna swali bali ni maelezo!

Lilitakiwa kuwa: ... 'huyo mama hana watoto? '
 
Si ujombani huko Yemen?

Still atasimama na wajomba hakuna kitu atasaidia hapo,yeye anajihesabia siyo mwafrika kwanza.
Wanavyoabudu waarabu hawa watu sidhani kama huyu bibi atasaidiwa. Hawa dhulumati miaka ya 2015-21 walirudi kwemye mashimo yao wote k!@#$%%%^&&e zao.
 
Back
Top Bottom