Kwanza kabisa ni kutoijua jiografia ndio maana baadhi ya watu wanashabikia bila kutathmin.
1: Ni kweli serikali iliyopita ilipita bila hat a kufanya lolote, mfano, kuna majengo ya Nyamagana council pale mkolani PM Pinda aliweka jiwe la msingi 2008, baada ya hapo hadi leo popo wanaishi mle. Ni la ghorofa moja.
kuna barabara ya usagara kisesa ilikuwa iishe 2008, hadi leo hamna kitu. Mkandarasi Nyanza roads ashafungasha virago maana hawajalipwa
Uwanja was ndege Mwanza miaka mingi umekuwa ukitajwa na tuliskia kuna pesa Ilihamishwa ikaenda jenga kwingine.
Hayo ni kwa uchache, hebu tembeeni Mwanza licha ya kwamba iko juu ya arusha kuna vyuo vingapi vyenye campus ya kueleweka mwanza, chuo gani cha serkali kinatoa degree ukitoka Dodoma hadi kanda ya Ziwa?
Watu mnatia hasira sasa ngoja nirap
Mwanza airport sasa itajengwa na itaisha mwakani 2017, kwa kuwa ni chini ya saamoja kufika Serengeti national park, unapata picha gani kuhusu watalii, mtalii gani unadhani atataka ashukie KIA atembee 8hours kufika Serengeti? Mtaisoma tu nakushaurini msome bajeti ya 2016/7 na ten a itakuwa poa ikaitwa Serengeti int airport
DIKKM hii ni SGR, awamu ya kwanza ni Dar_Isaka_Mwanza. Mwanza itakuwa na logistic hub nendeni fb gongeni "mwanza 2035" mtayaona haya, Eneo la fela litakuwa linapokea mizigo yote ya kanda ya ziwa na kupakuliwa pale. Sina hakika kama TPA na TRA watakuwa na ofisi ndogo kwa clearance.hii fursa nayo itaipa kick Mwanza
Mwanza inazungukwa na Mara,Simiyu,Shinyanga,Geita na Kagera eneo hili lina wakazi kama 17million, na wote wanatamka kuwa Mwanza ni kwao, kwa mtaji huu wa idadi kubwa ya watu jirani haitatokea hata chembe ya siku moja ilingane mji unaozungukwa na watu wa wanapenda kuishi porini kama wafugaji. Mtaimport hadi mtachemsha.
Bomba la mafuta litapitia Kagera Geita Shinyanga vyote hivi vitastimulate uchumi was mwanza maana safari zote za ndege ni mwanza
Mna vijitabia flan vya kibaguzi vinauzi sana, kuanzia kwenye ajira hadi kwenye Miradi
Chuo kama cha Nelson Mandela kudaadek kilikuwa kijengwe Mbeya nacho mmepora.
Hata ktk baadhi maofis hata ya gov unakuta mkurugenzi hadi msaidiz wake wote huko huko unajua napata machungu hata kuandika, pita airport huko pita pita Tanesco, Pita pita crdb mnakera nk