Arusha tunarudia kosa lile lile la kutokupanga mji kisasa. Mkuu wa Mkoa shughulikia hili

Upekuzi101

JF-Expert Member
Aug 28, 2020
221
542
Pamoja na Jiji la Arusha kuwa kitovu cha utalii, wengi waliofika wanaweza kukubaliana kuwa mji huu ulikuwa na bahati mbaya ya kutopangiliwa vizuri toka mwanzo.

Mji ni mdogo na huduma nyingi muhimu zinapatikana ndani ya eneo dogo katikati ya mji. Ukishafika stendi ya mabasi, ukapita Clock Tower, na kurudi Soko Kuu, unakuwa umemaliza mji ndani ya saa mbili kwa kutembea kwa miguu.

Hata hivyo, kwa sasa kuna juhudi za kupanua na kuendeleza maeneo mapya kama East Africa na Bondeeni City ili kuipa Arusha hadhi ya kimataifa, hasa kwa kuzingatia uwanja wa kisasa unaojengwa huko ambao unatarajiwa kuwa wenyeji wa michuano ya AFCON.

Kinachotendeka katika ujenzi na uuzaji wa viwanja maeneo hayo ni cha kusikitisha. Viwanja vimekuwa vikiuzwa kiholela, hata kwa vipimo vidogo kama mita 10 kwa 10, bila mpangilio wowote wa maendeleo. Hali hii inaleta hofu ya usalama, hasa endapo majanga kama moto yatatokea, kwani hakutakuwa na njia za dharura. Nyumba zinajengwa kwa kasi lakini bila kuzingatia mpangilio wa miji, hali inayorudia makosa yaliyofanyika katika maeneo mengine nchini.

Ili kuepuka kuifanya Arusha kuwa kama makazi holela, serikali inapaswa kuhakikisha viwanja vinavyouzwa vinakidhi vipimo vya angalau mita 30 kwa 20, na mipango ya ujenzi iwekwe wazi. Ramani bora za mji, njia za barabara, maeneo ya maduka, na huduma za msingi zinapaswa kuanishwa mapema.

Mnunuzi wa kiwanja apewe mwongozo wa matumizi sahihi ya kiwanja chake. Kukosa kuchukua hatua mapema kutaacha Arusha ikiwa na sura mbaya kwa miaka mingi ijayo, hali ambayo si sahihi kwa mji wenye umuhimu wa kimataifa.

#ArushaDeserveBetter
 
Back
Top Bottom