Haya kazi kwenu!
Wameshatuangalia na kugundua kuwa watanzania wote ni watiifu kwa viongozi wao ndio maana wanatuchezea kama mpira,unyonge wetu ndio uliotufikisha hapa,na ipo siku watakuja kutushika hata naniliu zetu na tutabaki kuwasujudia tu. na huku tukiimba mapambio ya kuwasifu,lakini wakitoka tu tunarudi kwenye ile korasi ya ufisadi,ufisadi ufisadi oye oye oye,na mwisho usiku tunalala,kesho yake tena mwimbo ni ule ule.
source: mzee wa sumo (Mpoki Bukuku)
Mwenyekiti wa Timu Maalumu (Task Force) ya Rais ya kuchunguza wizi wa mabilioni ya shilingi Benki Kuu katika kashfa ya ufisadi, Johnson Mwanyika (kushoto), ameshindwa kutoa hesabu kamili ya pesa wanayodai kukusanya na hakuwa na jipya la kueleza badala yake alishindwa kutoa majibu ya msingi ya maswali ambayo yamekuwa yakiulizwa.
Mwanyika akionekana dhahiri kushindwa kujieleza huku akijikanyaga katika kauli zake, alisema hadi sasa fedha hizo zinarejeshwa katika akaunti maalumu ambayo alisita kusema imefunguliwa katika benki gani na mafisadi wanaorejesha pesa wameijuaje?
Huku akionekana kukosa taarifa mpya za kutoa kwa vyombo vya habari, Mwanyika alishindwa kueleza kwa dhati kiasi cha fedha kilichokusanywa hadi jana badala yake alikisia kwamba ilitarajiwa kuwa sh 60 bilioni hadi asubuhi alipoondioka kazini.
Kwa kuonyesha Mwanyika hakuwa amejiandaa vya kutosha kuzungumza na vyombo vya habari, taarifa yake imepingana na taarifa yya maandishi iliyotolewa jana na Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM), ambayo ilimukuu taarifa ya timu hiyo na kusema zilikuwa zimekusanywa sh 64 bilioni.
Alirudia maeneo yake ya kusihi Watanzania kuwa na subira huku akishindwa kueleza pia kwamba, katika fedha hizo thamani ya mali ni kiasi gani na fedha taslimu.
MKUU wa Jeshi la Polisi nchini Inspekta Jenerali (IGP) Said Mwema akizungumza katika mkutano huo amewafafanisha watuhumiwa wa ufisadi katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT), sawa na watuhumiwa wa ugaidi ambao wanaweza kuilipua nchi.
alisema mchakato unaondelea katika urejeshaji wa fedha za umma zaidi ya sh 133 bilioni zilizoibwa EPA, alisema watu hao wanaweza kuilipua nchi iwapo watatafutwa kwa pupa.
IGP Mwema alisema timu inafahamu kwa kina jinsi Watanzania wanavyokerwa na kuhoji vipi, watuhumiwa hawakamatwi kitu ambacho hata wao (timu) kinawaumiza roho.
Alisema kuna mashaka makubwa miongoni mwa Watanzania kwamba, watu waliotajwa katika ufisadi huo wanapita mijini huku wakitamba lakini hawakamatwi hali ambayo inawafanya wananchi wahoji kazi ya timu hiyo.
"Kuna mashaka makubwa, watu waliotajwa wanaonekana kupita mijini, wanatamba, watu sasa wanaohoji hii timu kazi yake nini, hili jambo linawakera wengi na sisi pia tunajisikia hivyo hivyo," alisema IGP Mwema na kuongeza:,
"Tunaulizwa tunawaogopa, hata sisi inatusikitisha kwanini hatuwakamati, kila mtu anajua na kila mtu anataka wakamatwe, lakini hili suala linahitaji upepelezi mtambuka."
"Suala hili si dogo, linagusa watu wengi na maeneo mengi, tunachofanya ni kulishughulikia kwa umakini, watuhumiwa waliochukua fedha ni sawa na magaidi, tukiwafuata kwa pupa wanaweza kuilipua nchi.