Mgogoro wainuka kati ya Wananchi na TANROAD Njombe

Munjombe

JF-Expert Member
Dec 10, 2018
1,941
2,640
Kumekuwa na msuguano mkali kati ya wananchi wa Kitulila na Uongozi wa wakala wa Barabara mkoa wa Njombe.

Wananchi wanapinga kusudio la Tanroad kuchepusha Barabara ya Njombe Ludewa kwenye mradi wa Itoni-Lusitu wanadai Barabara hiyo inakwenda kuharibu mito kwa itapita kwenye vilima ambavyo ndio chanzo cha mito hiyo.

Baadhi ya wananchi wameenda mbali na kulaumu viongozi wa kijiji kwa kuwa wamekuwa vigeugeu kuwa upande wa mkandarasi na Tanroad bila kujali athari za baadae.

Wananchi walipohoji sababu za kuchepusha Barabara maafisa Tanroad wamekuwa na dharau na kuwàambia wananchi hao hawajasoma hivyo wao kama wataalamu wanajua wanachofanya.

Pia wananchi hao wameomba mbunge wao Ndugu Deo Mwanyika afike haraka kusikiliza kero hiyo kwani maisha na shughuli zao za kiuchumi zipo hatarini kutokana Barabara hiyo kuelekezwa kwenye vyanzo vya maji bila sababu ya msingi.
 
Back
Top Bottom