Mwanyika aongea...

Nilivyomsikiliza inaonekana ana point fulani (kama si politics). nampa benefit of doubt kwanza kabla sijamhukumu
Kuna mtu alikuwa ananambia siku hizi IGP ni kama cheo cha kisiasa kwakuwa ni waongeaji sana na utendaji mdogo!

BTW: Mi nilimsikiliza kwa umakini nikaona NI HERI ya yeye IGP kuliko AG ambaye kusema kweli naona hana jipya! Muhimu ni kushikilia hivi hivi mpaka kieleweke.
 
Posted Date::3/12/2008

Timu ya EPA yaita wahariri

* Kikao kuongozwa na Mwanyika
* Kufafanua utata wa marejesho ya fedha
* Wadau wahoji ziliko Sh50bn zilizorudi
* Wataka wamiliki kampuni wajulikane

Na Ramadhan Semtawa
Mwananchi

SIKU tatu baada ya Timu Maalumu ya kuchunguza ufisadi katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA), ndani Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kutoa taarifa kwa umma kuwa haiwafahamu watuhumiwa wa fedha hizo na kupata lawama kutoka kwa wananchi, sasa imeamua kukutana na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari nchini.

Uamuzi wa timu hiyo kukutana na wahariri umekuja huku bado kuna maswali mengi ambayo hayajapata majibu kuhusu watuhumiwa waliochota fedha za EPA.

Timu hiyo (Task Force) inayoongozwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Johnson Mwanyika, itakutana saa 5:00 asubuhi na wahariri hao katika Ukumbi wa Mikutano uliopo katika Majengo ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora jijini Dar es Salaam.

Awali, timu hiyo ilikuwa ikitoa taarifa nyepesi na fupi kupitia tovuti za vyombo vya habari au kutuma fax, ambazo hata hivyo, hazikuwa na majibu ya msingi ambayo yamekuwa yakihojiwa na umma, huku waandishi wakikosa fursa ya kuhoji kwa kina kuhusu mchakato huo.

Kwa mujibu wa taarifa ya Afisa Habari, Wizara ya Sheria na Katiba, Omega Ngole, Mwanyika anatarajia kufanya mkutano na wahariri wa vyombo vya habari kufafanua mambo mbalimbali kuhusu mchakato huo.

"Mwenyekiti wa Timu ya Rais ya Uchunguzi wa Fedha za EPA, Johnson Mwanyika anatarajia kufanya mkutano na wahariri wa vyombo vya habari ili kufafanua masuala kadhaa yanayohusu kazi inayoendelea ya timu hiyo," alisema Ngole kwa niaba ya Mwanyika.

Iwapo Mwanyika atazungumza na wahariri leo, itakuwa ni hatua moja ya kwanza kwa timu hiyo kuondoa urasimu na kukutana ana kwa ana na wawakilishi wa vyombo vya habari.

Mkutano huo unafanyika wakati wingu zito likiwa limetanda kuhusiana na mchakato mzima, huku maswali ya msingi yakikosa majibu hadi sasa na hasa ni akina nani hao waliorejesha fedha za EPA.

Hoja ambazo hazijajibiwa

Miongoni mwa maswali hayo, kubwa linahusu ni nani hasa ambao hadi sasa wamerejesha fedha Sh50 bilioni ambazo Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkullo, alitangaza kuwa zimerejeshwa.

Kutokana na kauli ya Mkullo, wanaharakati wanahoji ni nani hasa waliorejesha fedha hizo na vipi wasikamatwe na kufunguliwa kesi ya uhujumu uchumi na ni makampuni gani ambayo yamerejesha fedha hizo?

Swali jingine ambalo hadi sasa halijajibiwa ni pamoja na kwamba, hadi sasa ni makampuni mangapi kati ya 22 yaliyochota zaidi ya Sh133 bilioni za EPA, ambayo yamesharejesha fedha hizo. Je, fedha zinazorejeshwa zinawekwa katika benki gani?

Katika mchakato huo, pia kunajitokeza swali la fedha hizo kuwa zipo katika akaunti ipi, BoT au akaunti maalumu kwingineko?

Maswali hayo hadi sasa hayajapata majibu, licha ya timu hiyo chini ya Mwanyika kutoa taarifa tatu katika vipindi tofauti.

Kauli zenye utata

Taarifa ya mwisho iliyotolewa Jumapili wiki iliyopita ilihusu kauli ya Mwanyika kwamba hadi sasa timu hiyo imeweza kubaini makampuni tu na si wahusika.

Kauli hiyo ambayo inatafsiriwa kwamba mafisadi hawashikiki, imewafanya Watanzania wa kada mbalimbali kuanza kuwa na wasiwasi na mchakato mzima wa kuwafichua mafisadi hao.

Timu hiyo ambayo inaongozwa na Mwanyika na wajumbe wengine akiwemo Mkuu wa Jeshi la Polisi, Inspekta Jenerali (IGP) Said Mwema na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Edward Hosea, iliundwa na Rais Kikwete, mapema Januari, mwaka huu, baada ya kubainika kwa ufisadi huo wa fedha za umma na kisha kumwachisha kazi aliyekuwa Gavana wa BoT, Daud Ballali na nafasi yake kuchukuliwa na Profesa Benno Ndulu.

Hata hivyo, hadi sasa timu hiyo haijamkamata mtuhumiwa hata mmoja licha ya kusema fedha zimeshaanza kurejeshwa na kutambulika kwa makampuni yaliyorejesha fedha hizo kwa hundi, bila wamiliki wake kujulikana.
 
Fedha za EPA zimerejeshwa na majini?

Machi 12, 2008
Raia Mwema

Wahenga walisema, “Ukishangaa ya Musa utayaona ya Firauni.” Na kweli. Hivi sasa tunaambiwa na tume ya Rais ya kuchunguza wizi unaohusu Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) ndani ya Benki Kuu ya Tanzania (BOT) kwamba watu waliohusika na wizi huo hawashikiki kwa sababu kinachojulikana ni makampuni, siyo watu.

Kabla ya hapo tulikwisha kuambiwa kwamba baadhi ya watuhumiwa katika kashfa hiyo walikuwa wameanza kurejesha fedha na kwamba Serikali ilikuwa imekwisha kustakabadhi shilingi bilioni 50. Hayo yalisemwa na Waziri wa Fedha, Mustafa Mkullo na Mwenyekiti wa Tume ya Rais, Johnson Mwanyika.

Mtu akisema kwamba kauli kama hizi zinamchanganya atakuwa na haki ya kusema hivyo. Maswali kadhaa yanamjia mtu moja kwa moja, bila hata kufikiri. Je, ni kweli kwamba hizo fedha zimerejeshwa? Kama zimerejeshwa, nani kazirejesha? Makampuni? Je, makampuni hayo yana wamiliki, na hao wamiliki ndio wamezirejesha, au fedha hizo zimetembea zenyewe na kujiingiza katika akaunti fulani ya Serikali?

Au kuna majini wanaobeba mikoba ya fedha usiku wa manane na kutumbukiza fedha hizo katika akaunti hiyo wakati nchi nzima imelala? Kama ni hivyo, si tungekwenda Mlingotini tukashauriana na “mafundi” badala ya kuteua tume ya kutubabaisha?

Tunaamini kwamba wazito waliomo ndani ya tume ya Rais wanaelewa kwamba kila mtu anajua kwamba kampuni iliyorajisiwa lazima iwe na wakurugenzi na anwani inayoeleweka. Iweje washindwe kujua wamiliki wa makampuni hayo ni akina nani? Au wanawajua lakini kuna vipengele vya sheria vinavyoizuia tume kuamuru wakamatwe angalau hao wanaorejesha fedha?

Mwizi akibainika kwamba kaiba, hawezi kurejesha mali aliyoiba kisha akaachiwa huru. Haki ya kwanza ya mwizi ni kukamatwa na kupelekwa mbele ya vyombo vya sheria. Kurejesha alichoiba, au kufilisiwa pale inapopasa, ni hatua ya pili. Au, labda, hawa watuhumiwa hawakuiba bali ‘walikopa’ tu?

Na kama walikopa kwa nini Serikali imelifanya suala hili liwe kubwa kiasi hiki? Si wangeambiwa warejeshe mikopo hiyo kwa wakati uliokubaliwa ndani ya mkataba wa mkopo, wakiwa wamelipa riba mwafaka?

Watu wana haki ya kuendelea kusaili busara ya kuwatumia maofisa wa Serikali katika uchunguzi kama huu. Kwa nini isingeundwa kamati ya Bunge? Maofisa wa Serikali na vyombo vyake ndio watu wa kwanza kuhusika na uchafu unaofanywa katika idara za Serikali, na silika yao ni kufanya kila kitu ni siri. Je, hapa hatujapeleka kesi ya nyani iamuliwe na tumbili?

Chacha, chichi tucheme nini?
 
MKUU wa Jeshi la Polisi nchini Inspekta Jenerali (IGP) Said Mwema akizungumza katika mkutano huo amewafafanisha watuhumiwa wa ufisadi katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT), sawa na watuhumiwa wa ugaidi ambao wanaweza kuilipua nchi.

KAMA NI HIVYO MBONA WAKO MITAANI WAKITANUA HII SELF CONFIDENT WANAPATA WAPI?

alisema mchakato unaondelea katika urejeshaji wa fedha za umma zaidi ya sh 133 bilioni zilizoibwa EPA, alisema watu hao wanaweza kuilipua nchi iwapo watatafutwa kwa pupa.

WATATAFUTWA? wepi tena hao

IGP Mwema alisema timu inafahamu kwa kina jinsi Watanzania wanavyokerwa na kuhoji vipi, watuhumiwa hawakamatwi kitu ambacho hata wao (timu) kinawaumiza roho.

Kweli? au ni lugha ya daganya toto

Alisema kuna mashaka makubwa miongoni mwa Watanzania kwamba, watu waliotajwa katika ufisadi huo wanapita mijini huku wakitamba lakini hawakamatwi hali ambayo inawafanya wananchi wahoji kazi ya timu hiyo.

B*******

"Kuna mashaka makubwa, watu waliotajwa wanaonekana kupita mijini, wanatamba, watu sasa wanaohoji hii timu kazi yake nini, hili jambo linawakera wengi na sisi pia tunajisikia hivyo hivyo," alisema IGP Mwema na kuongeza:,

"Tunaulizwa tunawaogopa, hata sisi inatusikitisha kwanini hatuwakamati, kila mtu anajua na kila mtu anataka wakamatwe, lakini hili suala linahitaji upepelezi mtambuka."

KICHEFU CHEFFU
 
source: mzee wa sumo (Mpoki Bukuku)

Tunaulizwa tunawaogopa, hata sisi inatusikitisha kwanini hatuwakamati, kila mtu anajua na kila mtu anataka wakamatwe, lakini hili suala linahitaji upepelezi mtambuka."

"Suala hili si dogo, linagusa watu wengi na maeneo mengi, tunachofanya ni kulishughulikia kwa umakini, watuhumiwa waliochukua fedha ni sawa na magaidi, tukiwafuata kwa pupa wanaweza kuilipua nchi
.


...hii ni balaa kama anawalinganisha hawa jamaa na magaidi hivi si ndo wanapaswa wewe keko ili kuinusuru nchi isilipuliwe...mimi nasikitika saaaaana tena nalia kilio kama cha koana aliyebanwa na ndoana....tunadanganywa saaaaaaana....hakuna sababu za msingi kwa nini hawa watu wasikamatwe....inasikitisha sana na inauma...
 
Mafisadi wa EPA kutajwa bungeni

  • Ni kutokana na shinikizo la wananchi
  • Ahadi ya Spika yasubiriwa kwa hamu
na mwandishi wetu

SHINIKIZO la wananchi la kutaka kujua watuhumiwa walioiba fedha za Mfuko wa Madeni ya Nje (EPA), limeifanya Serikali ifikie uamuzi wa kupeleka bungeni taarifa ya Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali.

Vyanzo vya habari vimeidokeza MTANZANIA kwamba awali, Serikali ilikuwa na mpango wa kukiuka ahadi yake iliyotolewa bungeni, ya kuhakikisha taarifa ya uchunguzi, haifikishwi kwenye chombo hicho cha uwakilishi.

Aliyekuwa Waziri wa Fedha, Zakia Meghji, alishaahidi bungeni kwamba taarifa ya uchunguzi huo ingefikishwa na kujadiliwa bungeni.

Hata hivyo, kashfa ya kampuni hewa ya Richmond, ambayo iliibuliwa na Kamati Teule ya Bunge, ilizima kabisa mjadala wa fedha za EPA.

Habari zilizopatikana wiki hii zilisema, baada ya mjadala huo ‘kukwepwa’ katika Mkutano uliopita, sasa utaibuka katika Mkutano utakaoanza mwanzoni mwa mwezi ujao.

“Kulikuwa na mpango wa kulimaliza suala hili nje ya Bunge. Uamuzi huo ulitokana na kile kilichoonekana kwenye Richmond, Serikali haikuwa tayari kuona tena ikiumbuliwa.

“Lakini baada ya shinikizo la wananchi, na kwa kuzingatia kuwa Serikali ilishatoa ahadi bungeni ya kujadiliwa kwa ripoti hiyo, Serikali imejikuta haina namna yoyote ya kukwepa,” kimesema chanzo chetu cha habari.

Hofu ya Serikali, ambayo ilishaanza kuonyeshwa na Meghji, inatokana na ukweli kwamba ripoti ya EPA imesheheni majina ya viongozi wadogo kwa wakubwa, wafanyabiashara na watu wengine maarufu.

“Tumetafakari na kuona hatuna ujanja katika suala hili, lazima suala hili lifikishwe bungeni. Lakini inawezekana isiwe kwenye Bunge la Aprili, inaweza ikawa kwenye Bunge la Bajeti.

“Lakini vyovyote iwavyo, Bunge lazima lipewe taarifa kamili ya uchunguzi. Sasa ni wazi kuwa taarifa ya EPA, itapelekwa kusomwa na kuchambuliwa bungeni,” kimesema chanzo chetu.

Katika Mkutano wa 10 wa Bunge uliomalizika, Spika Samuel Sitta, alikuwa mkali kuhusu ufisadi katika EPA, na akaitaka Serikali iwasilishe taarifa kamili ya uchunguzi.

Msimamo wa Spika ulitokana na taarifa isiyo ya kina, iliyowasilishwa na Meghji kwa wabunge.Waziri wa Fedha aliwasilisha bungeni mjini Dodoma, taarifa isiyo ya kina, inayofanana na iliyowahi kutolewa kwa waandishi wa habari.

Matarajio ya wabunge ni kwamba ingewasilishwa taarifa kamili ya uchunguzi, na si taarifa iliyokwishachujwa.

Baada ya Meghji kusoma taarifa hiyo, wabunge wawili walisimama wakitaka mwongozo wa Spika. Wabunge hao ni John Cheyo wa Bariadi Mashariki (UDP) na Christopher ole Sendeka (Simanjiro).

“Mheshimiwa Spika naomba mwongozo wako. Kwamba taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali imekwishafika katika meza yako na kama itajadiliwa kama taarifa nyingine. Na kama haijafika…itafikishwa lini ili tuweze kuijadili?” Alihoji Cheyo.

Sendeka, ambaye naye alikuwa mkali dhidi ya Meghji, alisimama na kusema: “Mheshimwa Spika, kwa kuwa Waziri amewasilisha summary (muhtasari) kuhusu uchunguzi wa BoT, je, itakubalika uielekeze Serikali watuletee taarifa rasmi ya ukaguzi, na si hii iliyokwishakuwa extracted (iliyochujwa) ili Bunge lichukue nafasi yake kama mhimili…ikiwezekana iwepo Kamati Teule ya Bunge…ili ukweli ubainike?” Alihoji Sendeka.

Katika kutoa mwongozi, Spika alisema: “Masuala haya yote (kuleta taarifa hiyo bungeni) yalikuwa katika mchakato wa mashauriano kati ya Bunge na Serikali. Wiki hii tutawapa taarifa hiyo. “Pengine kwa kumbukumbu tu ni kwamba, nilikwishakubali katika Mkutano wa Tisa wa Bunge hili kuwa ripoti italetwa hapa na kujadiliwa, baada ya Mbunge Lucy Mayenga kuomba taarifa hiyo ipangiwe muda maalumu wa kujadiliwa,” alisema Spika.

Aliendelea kusema: “Hata kama Serikali haitataka, ombi hilo lipo ‘live’. Tutaanzia hapo…hizi ni zama za uwazi na ukweli, nadhani tutaafikiana tu,” alisema Sitta, bila kufafanua zaidi wataafikiana na nani na katika jambo gani.

Julai 2, mwaka jana, Edward Lowassa, akiwa Waziri Mkuu, aliahidi kuwa ripoti ya uchunguzi wa ufisadi BoT, baada ya kukamilika itawasilishwa bungeni.

Lowassa alisema: “Tumechukizwa na kushtushwa na taarifa kwamba kuna fedha zimepotea ndani ya Benki (BoT), kwa hiyo, baada ya kuchukizwa na jambo lenyewe, tumemwagiza CAG, tunamwamini ni mtu shupavu, ashirikiane na audit za kimataifa wakague benki wajue imekuwaje jambo hili kama ni kweli.

“Je, ni kweli? Nani anahusika? Ni kina nani na tuchukue hatua gani ili jambo hili lisije likatokea tena kama kweli limetokea? Kwa hiyo, Serikali tumechukua hatua kabla ya kuja hapa. Baada ya taarifa hiyo kupatikana tutachukua hatua zinazopasa na Bunge hili litaarifiwa.”

Rais Jakaya Kikwete aliteua timu inayoundwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini na Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU). Timu hiyo, hadi jana, ilikuwa imefanikiwa kuokoa Sh bilioni 64.

Source: Mtanzania
 
Back
Top Bottom