Mwanaume Vs Mwanamke: Uchambuzi wa Ubongo wa Mwanadamu

Arnold Kalikawe

Senior Member
Sep 28, 2016
145
334
Tafiti nyingi zimepambanua utofauti wa namna akili ya mwanaume na mwanamke; majibu ni kama yafuatavyo.

1. KUFANYA KAZI NYINGI.
Wanawake wana Ubongo wenye michakato mingi. Akili za wanawake iliyoundwa ili kuzingatia kazi nyingi kwa wakati mmoja. Wanawake wanaweza Kutazama TV na Kuzungumza kupitia simu na kupika.

Wanaume wana Ubongo wenye Mchakato Mmoja. Akili za wanaume zimeundwa kuzingatia kazi moja tu kwa wakati mmoja. Wanaume hawawezi kutazama TV na kuzungumza kwa simu kwa wakati mmoja. Wanasimamisha, kupunguza Sauti au kuzima TV huku wakiongea. Wanaweza kufanya kimoja kati ya kutazama TV au kuzungumza kwa simu au kupika, lakini sio vyote kwa mkupuo.

2. LUGHA
Wanawake wanaweza kujifunza lugha nyingi kwa urahisi na kwa haraka. Lakini hawezi kupata ufumbuzi wa matatizo kwa urahisi.

Wanaume hawawezi kujifunza lugha kwa urahisi lakini wanaweza kutatua matatizo kwa urahisi. Ndio maana kwa wastani msichana wa miaka 3 anaweza kufahamu msamiati mingi mara tatu kuliko mvulana wa miaka 3.

3. UJUZI WA UCHAMBUZI
Ubongo wa wanaume una maeneo mengi ya kushughulikia mchakato wa uchambuzi. Wanaweza kuchanganua na kutafuta suluhisho la mchakato mfano kubuni ramani tata ya jengo kwa urahisi. Lakini ikiwa ramani hiyo hiyo itatazamwa na wanawake, hawawezi kuielewa. Wanawake hawawezi kuelewa na kutafsiri maelezo ya ramani kwa urahisi, Kwao ni wataona kama mistari tu imechorwa kwenye karatasi.

4. KUENDESHA GARI.
Wakati wa kuendesha gari, nafasi mbalimbali za uchambuzi hutumiwa kwenye ubongo wa mwanaume, na kumfanya aweze kufanya maamuzi ya haraka. Anaweza kuendesha gari kwa kasi. Ikiwa anaona kitu kwa umbali mrefu, mara moja ubongo wake utambua na huainisha kitu mfano aina ya gari, mwelekeo wa gari, na kasi ya hilo gari na basi anaendesha ipasavyo kwa mujibu wa vitu atakavyokutana navyo barabarani. Ambapo mwanamke huchukua muda mrefu kutambua mwelekeo wa kitu / kasi. Ubongo wa mwanaume wenye mchakato mmoja husimamisha sauti kwenye gari (kama ipo) au jambo lolote linaloendelea kwenye gari, kisha huzingatia kuendesha gari pekee.

5. KUSEMA UONGO
Wanaume wanapowadanganya wanawake uso kwa uso, wanakamatwa kwa urahisi. Ubongo wa asili wa wanawake unaona na kutafsiri ishara za uso kwa 70%, lugha ya mwili kwa 20% na maneno kutoka kinywani kwa 10%, mwanamke hazingatii tu maneno ya mdomoni bali huzingatia zaidi kwenye ishara za uso na lugha za mwili. Ubongo wa wanaume hauna hii. Wanawake hudanganya kwa urahisi kwa wanaume endapo watakutana uso kwa uso. Kwa hivyo nyie wanaume, msiseme uongo uso kwa uso, inatakiwa uwe Mafia hasa maneno yako yaendane na ishara za uso na lugha ya mwili kuweza kufanikiwa kudanganya. Unaweza kumdanganya akakubali ila moyoni akajua umemdanya ila akapuuzia.

6. KUTATUA MATATIZO
Ikiwa mwanaume ana matatizo mengi, ubongo wake huainisha kwa uwazi matatizo hayo na kuyaweka katika mpangilio binafsi katika ubongo na kisha kutafuta suluhisho la jambo moja moja mpaka yote yaishe. Unaweza kuona watu wengi wakitazama angani kwa muda mrefu. Ikiwa mwanamke ana matatizo mengi, ubongo wake hauwezi kuainisha matatizo kwa ajili ya ufumbuzi, bali atataka amuelezee mtu mwingine. Baada ya kumuelezea kila kitu mtu, basi anaenda kitandani kwa furaha na kulala, bila ya kuwa na wasiwasi kuhusu matatizo kutatuliwa au la. Wanachukulia matatizo kwa uwepesi.

7. WANACHOTAKA
Wanaume wanataka hadhi, mafanikio, suluhu, maendeleo mkubwa, nk... Lakini Wanawake wanataka uhusiano, marafiki, familia, nk...

8. KUTOKUWA NA FURAHA
Ikiwa wanawake hawana furaha na mahusiano yao, hawawezi kuzingatia kazi zao. Ikiwa wanaume hawana furaha na kazi zao, hawawezi kuzingatia mahusiano. Kwa mwanaume Kazi ni kipaumbele kuliko mahusiano, ila kwa mwanamke mahusiano ni kipaumbele kuliko kazi. Ni rahisi kumshawishi mwanamke kuacha kazi kisa mahusiano mfano aolewe, ila ni ngumu kumshawishi mwanaume aache kazi kisa mahusiano.

9. HOTUBA
Wanawake hutumia lugha isiyo ya moja kwa moja katika hotuba. Lakini Wanaume hutumia lugha ya moja kwa moja. Kwa kifupi mwanamke atafumba fumba vitu au kuzunguka sana anapotaka kuwasilisha jambo lake, ila mwanaume ni mtu wa kunyoosha maelezo.

10. KUSHUGHULIKIA HISIA
Wanawake wanaongea sana bila kufikiria. Wanaume hutenda sana bila kufikiria. Mfano: Mwanamke ni rahisi kusambaza Uongo na umbea bila kufikiria athari zitakazotokea, na mwanaume ni rahisi kuonga sana pesa bila kufikiria athari za kiuchumi.
 
Back
Top Bottom