Mpasuaji wa Manesi
JF-Expert Member
- Mar 13, 2016
- 299
- 1,372
Mwanaume,
NDOA ikishafeli, na Wakati tu mgogoro wa kugombania watoto utapoanza na wewe ukakomaa nao, hapo kaa ukijua tayari umeshindwa kabla hujaanza. Yaani hapo Mwanamke tayari anakuwa amekushinda.
Mkienda Mahakamani, utashindwa.
Ukienda Kanisani, huko pia utashindwa.
Ukienda Ustawi wa jamii, utashindwa pia.
Na hata ukija Jamiiforums pia, bado utashindwa (members watakukaanga).
Hivyo nisikilize Mpasuaji wa Manesi,
Tenganisha Hisia zako na watoto wako, mambo ya hisia achia Wanawake, hao tayari ni watoto wako na jamii inalifahamu hilo. Na hata watoto wako pia wanafahamu kuwa wewe ni Baba yao, hivyo huna sababu ya kuleta visirani.
Kama Mama yao anahitaji kubakia na watoto, ni sawa. Muache abaki nao. Huna sababu ya kuchukua wanao kinguvu na kuwapitisha watoto kwenye migogoro itakayoharibu fikra zao na kuwaachia kumbukumbu mbaya.
Kama kweli unajali watoto wako, basi jiepushe na migogoro na malumbano isiyo vya lazima. IKIWEZEKANA, Jitahidi kuwafanya hata watoto wako wasijue nini kinaendelea.
Wewe Ondoka kwa amani na fanya majukumu yako inavyopaswa.
Watoto sio wajinga, wanaona kila kitu na watafahamu kinachoendelea. Wakati wao utakapofika watakutafuta.
LAKINI ukiendelea kuwa wa migogoro, mara uibe mtoto, mara ugomvi, mara vikao kila siku, hata watoto wako nao watakuona wewe ni PUMBAVU na hawatakuheshimu.
"Mimi siwezi kuacha damu yangu", "Lazima niwapambanie wanangu", Hizi ni kauli za Wanaume wajinga. Mitazamo yao kuhusu ndoa ni ile ya kwenye drama na kwenye Movie.
Be a Man, Stay taliban.
EDITED, Tar 4 August 2023:
Nimesoma Comment za wale wale mnaoendeshwa na hisia, "My child is my everything", "nipo tayari kwa lolote kwa ajili yao", "I love them and they love me so much and other bla bla bla."
Mpo SAHIHI pia, endeleeni kupambana na hio migogoro huko Ustawi wa jamii, vikao kila siku na Mahakamani, hakuna aliyewazuia.
Mtu isipomfaa akili yake, basi utamdhuru ujinga wake.

- Wafungulie watoto account ya Bank.
- Weka pesa humo kila mwezi.
- Weka kiwango maalumu kinachoweza kutoka kwa mwezi mtu atakapotoa.
- Lipa ada moja kwa moja kwenye Shule husika.