Mwanaume mzima unashika shika........!

Mwanaume mzima unashika shika........!

Ulichokifanya umekosea na alichokifanya mkeo amekosea pia, wote mmekosea.
Kivipi?

*Japokuwa ni mke wako na una uhuru nae na vitu vyake, lakini inategemea desturi na utamaduni wa kuishi mliojijengea nyinyi wenyewe. Kumbuka mikoba ya kina mama inabeba vitu vingi tena vingine ni siri(Urembo, Pedi, Nguo, Dawa nk) kwa mwanamke mwenyewe tu, hivyo sio busara sana kuifungua pasipo ridhaa ya mwanamke mwenyewe unless mmeshajenga utamaduni huo!!

*Mkeo pia amefanya makosa sana kwa kuonyesha ukali na hasira kwa jambo ambalo hajaridhia kwanza kufanywa na mume wake, hivyo imepelekea wewe kuhisi vibaya.

Nawewe huna akili, unatetea ushenzi? Mikoba inabeba vitu vya siri? Pedi ni kitu cha siri kwa mume na mke? Mbona akiivaa hiyo pedi anavaa nikimuona? Pumbavu ukioa utajua haya.
 
Nawewe huna akili, unatetea ushenzi? Mikoba inabeba vitu vya siri? Pedi ni kitu cha siri kwa mume na mke? Mbona akiivaa hiyo pedi anavaa nikimuona? Pumbavu ukioa utajua haya.

Afadhali umesema wewe ningesema mimi mngesema nina chuki na jinsia Ke...!!!

we TanganyikaTANU bichwa lako....!!!!
 
Last edited by a moderator:
Huu uzungu sijui unatupeleka wapi wabongo!!!!!! Yaani mwanamume mzima unakuja kuuliza eti ufanye nini, shit????
 
Kama angekuwa ni mke wangu kwanza angechezeya vitasa halafu maelezo yangefuata baadae sana.Mkuu acha kushikwa maskio kiivyo!
 
Hapa tatizo ni huyu mwanamume.... hajijui au bado hajakua na hajui ndoa ni nini anafikiria ni kufuatana na kusindikizana kazini tu!!!! Kuna siri gani kwenye ndoa, labda kama hamjaoana!!!!
 
Nimependa comment yako. Wote wana makosa. Kwani kwa jinsi dada alivyofura ni wazi hawana utamaduni wa uwazi kwenye ndoa yao so alipaswa akubaliwe kwanza. Na mdada naye kuropoka maneno yote hayo, mhm? Sio vizuri.
Wakaongee wasameheane. Ndio misukosuko ya ndoa hiyo.

na ndio mana wakati mwingine haitakiwi kuishi kwa mazoa alicho fanya uyo Dada si cha kistarabu kuhusu mkoba hakuna kitu ambacho anapaswa kuto ona kwenye mkoba wake jamaa chamsingi afanye uchunguzi kunakitu hapo
 
.......mwanaume zima unashika shika mikoba ya wanawake!! we vipi??? Yalikuwa ni maneno yaliyonichoma barabara moyo wangu tena kutoka kwa mwanamke ninayempenda kuliko wote, yaani mke wangu!!!

Ilikuwa hivi, ametoka kazini akanipitia mimi kazini kwangu tukawa tunajirudisha home taratiibu na stori mwanana za kutaniana hivi na vile bora tumekutana tunaopendana!!!

Ugomvi ulianzia nilipopokea simu ya mfanyakazi mwenzangu akinitaarifu kuwa report niliyotuma, attachment haikwenda ambayo ndiyo report yenyewe!!! So nitume tena na kwa haraka sana coz makao makuu wanaisubiri jioni hiyo hiyo!!! Niliwasha laptop yangu nikakuta ina umeme kidogo sana nilichofanya ni kuibeba kwenye flash na nikalazimika kumuomba mke wangu laptop yake ili niitumie kwa muda huo!!!

Ye wife anatumia mini laptop ambayo inaingia kwenye mkoba wake anaoweka na vitu vingine vya kike, kiukweli sikusubiri jibu lolote toka kwake nikafungua mkoba wake na kutoa min laptop yake nikaiwasha na kuanza kutumia, kumbe mwenzangu muda wote huo hakuniona ila alinielewa kuwa nahitaji laptop yake!!!

Aliposimamisha gari na kunigeukia akakuta natumia tayari, daah!!! Yalimtoka maneno ambayo sijawahi kuyasikia kinywani mwake tangu namfahamu (moja wapo ni hayo niliyotumia kama title aya ya kwanza)!! Alikasirika mwanamke mpaka nikashangaa, sikumjibu kitu kwani nilituma niliyoyatuma nikazima laptop yake nikamrudishia!!!

Katika kudadisi kwangu niligundua yafuatayo;
1. Alikasirika sababu nimefungua mkoba wake, Je wana JF mimi kama mume mtu siruhusiwi kugusa mkoba wa mke wangu na kuufungua??
2. Alikasirika mimi kuwasha laptop yake kwa madai kwamba ile ni kitu binafsi kama ilivyo simu so nilipaswa kusubiri aniwashie!! Wana JF laptop pia ni restricted kwa mume/mke???

Kifupi mie sijaongea nae kitu mpaka sasa coz mihasira mingi na nimejikuta nina mengi yanazunguka kichwani nataka kwanza nitulie ili nilianzisha tuelewane vizuri!!!

Ila bado najiuliza nilikuwa sahihi ama nimekosea??? Wana JF mnaonaje hili????

Nawasilisha

Mkuu, kwanza nianze kwa kukupa pole kwa huo mtafaruku uliojitokeza baina yako na mkeo, kimsingi hapa kitu kikubwa kilichomfanya mkeo kuwa na gadhabu na kukueleza hayo aliyo kueleza, ni usiri alio uifadhi ndani ya mkoba wake, wenda kwenye hiyo mini laptop au kwenye mkoba wenyewe.

Sasa unapokuwa unafungua kitu ambacho mtu amekiifadhi kwa ajili yake tu, hapo lazima mtu awe mbogo, ila kama hakuna usiri basi kama amechukizwa, angekueleza kwa utaratibu na kamwe asinge tumia lugha ya kukufedhehesha kama aliyo tumia.

Mi nadhani labda alikuwa na vidonge vya ugonjwa ambao hataki wewe uujue, alikuwa na picha au kitu kingine chochote cha jembe lingine, au kwenye hiyo laptop yake, kama una mazoea ya kuiwasha na kuitumia basi haitakuwa na shida, ila kama anaificha na kamwe hataki uiguse, basi hapo kuna kitu. haya ni baadhi tu ya mambo ambayo mkeo anaweza akawa anakuficha kuhusu yeye. It is your job to find out, what exactly is it.
 
Yan nshashikaga mkoba wa mamito nae acha agombe,nikiwa nae road anangangania kunibebea briefcase yangu ila wa kwake ndo hataki hata niguse
 
Ukiona mkeo anakutamkia hayo maneno ujue kabisa anajua udhaifu wako, anajua humfanyi kitu na utaacha mara moja kurukia mkoba wake. Yani anakujua A-Z ndo mana hata wewe umeshindwa kumuuliza unakuja kutuuliza sisi wanaMMU, vile vile siku hizi hakuna wanaume kuna vianaume. Mwanaume lazima ujue kutumia maneno why, where, how etc.
 
1.Ulifanya ghafla coz uliweweseka kutokana na report kutofika,ilibidi umfahamishe unatumia laptop yake kuna issue iko tight kwako.
2. Umetumia lazima akupe na ungeafanya tu kazi yako mkuu.
3.kakosea sana kukumaind kiasi hiki sio heshima hata kidogo haswa kwa mume na mke na hii inashilia kuna jambo lipo zaidi ya laptop lifanyie kazi.
3. busara sana kutumia na kumrudishia kisha kukaa kaumyaa na kutafakari kunanini? ni laptop tu au kuan lingine?
4.kaa nae na muulize tatizo nini? na hujapendezewa na aliichokifanya last time na akuelize kwanini na kunanini?
4.kama kauliza zake hazieleweki, anza kumfuatilia kwa ukaribu nyendo zake.
hawa watu unatakiwa uishi nao kwa hekima sana mkuu, somtimes unawaka kinoma, sometimes unakuwa muungwana usiwe defined sana!
 
nivea nimependa ujumbe wako natumia simu aise ningekupa like ya nguvu.
Haya mapenzi ya tamthilia yanatucost sana vijana aise maana mambo mengine sio ya kufanywa baina ya mke na Mume kwa kauli yake hiyo ni mbaya sana na haikustahili. Hebu kaa nae chini uongee nae umuulize maana ya kauli yake hiyo ya ukali ambayo haikustahili kabisa.
 
Last edited by a moderator:
Yeah Nivea the guy has got something manly of us are sill looking...............lkn nchi inakuaga na majeshi,usalama wa taifa na mambo kibao lkn huwa zinapindulia saa huyu moja nitashindwa kumpindua,noooo,nahitaji mwanamke wa hivyo,lazima apinduliwe
for sure he is really lucky and happy endeed.hua mimi sio msaliti wa moyo wangu na siishi maisha ya pretending hata siku moja.
 
.......mwanaume zima unashika shika mikoba ya wanawake!! we vipi??? Yalikuwa ni maneno yaliyonichoma barabara moyo wangu tena kutoka kwa mwanamke ninayempenda kuliko wote, yaani mke wangu!!!

Ilikuwa hivi, ametoka kazini akanipitia mimi kazini kwangu tukawa tunajirudisha home taratiibu na stori mwanana za kutaniana hivi na vile bora tumekutana tunaopendana!!!

Ugomvi ulianzia nilipopokea simu ya mfanyakazi mwenzangu akinitaarifu kuwa report niliyotuma, attachment haikwenda ambayo ndiyo report yenyewe!!! So nitume tena na kwa haraka sana coz makao makuu wanaisubiri jioni hiyo hiyo!!! Niliwasha laptop yangu nikakuta ina umeme kidogo sana nilichofanya ni kuibeba kwenye flash na nikalazimika kumuomba mke wangu laptop yake ili niitumie kwa muda huo!!!

Ye wife anatumia mini laptop ambayo inaingia kwenye mkoba wake anaoweka na vitu vingine vya kike, kiukweli sikusubiri jibu lolote toka kwake nikafungua mkoba wake na kutoa min laptop yake nikaiwasha na kuanza kutumia, kumbe mwenzangu muda wote huo hakuniona ila alinielewa kuwa nahitaji laptop yake!!!

Aliposimamisha gari na kunigeukia akakuta natumia tayari, daah!!! Yalimtoka maneno ambayo sijawahi kuyasikia kinywani mwake tangu namfahamu (moja wapo ni hayo niliyotumia kama title aya ya kwanza)!! Alikasirika mwanamke mpaka nikashangaa, sikumjibu kitu kwani nilituma niliyoyatuma nikazima laptop yake nikamrudishia!!!

Katika kudadisi kwangu niligundua yafuatayo;
1. Alikasirika sababu nimefungua mkoba wake, Je wana JF mimi kama mume mtu siruhusiwi kugusa mkoba wa mke wangu na kuufungua??
2. Alikasirika mimi kuwasha laptop yake kwa madai kwamba ile ni kitu binafsi kama ilivyo simu so nilipaswa kusubiri aniwashie!! Wana JF laptop pia ni restricted kwa mume/mke???

Kifupi mie sijaongea nae kitu mpaka sasa coz mihasira mingi na nimejikuta nina mengi yanazunguka kichwani nataka kwanza nitulie ili nilianzisha tuelewane vizuri!!!

Ila bado najiuliza nilikuwa sahihi ama nimekosea??? Wana JF mnaonaje hili????

Nawasilisha
Aisee hapo hakuna true love! Mchunguze vizuri!
 
Nadhani tuangalie pia upande wa pili, kama mwanamke ndio ananguvu kiuchumi ni rahisi kuwa na jeuri hiyo. Vinginevyo jamaa ana sauti nyororo au ndio wanaume kama mabinti? Komaa maana hapo kuna namna. Ukicheka na Kima utavuna mabua.
 
Mmmmh. Ebwana pole lkn ukumbuke ndoa yako pindi mnafunga jf hawakuwepo jitahidi busara zaidi, huenda alichukia kwakuwa alitegemea baada ya kumwomba utasubili akupe sasa alivyoona umechukua akahisi lbda kuna ki2 unataka kumchunguza sio kweli eti atakuwa na vi2 za siri huenda hapendi kuingiliwa katika mambo yake bila idhini, hebu geuza picha ije kwako ungejickiaje, kakuomba cm hujatoa jibu anayo, na kwa bahati mbaya hukufuta ka sms ka yule dada pale kazin alikokukaribisha chai kwa mbwembwe za mitego!!!!!?
 
Mimi ni signature yako imenikosha. Tafadhali nikumbushe kidogo hiyo ni Orchestre Makassy au Toma Toma?
Dah !! Wakongwe.

Hii Ilikuwa Orchestre makassy, wakati huo niko Darasa la tatu, tukitoka shule inasikia inaimba, na wakati huo ni radio Tanzania tu
 
Hapo kuna kitu zaid ya laptop ili ujue mengi kua mpole kwanza chunguza kimyakimya utapata jibu baada ya hapo chukua hatua
 
wanajua sana na wanawake wengi wanaelewa ,wanawake wako so curious tofauti wanaume, kitu cha kwanza mwanamke akikutana na mwanaume yeye hutafuta kuyajua madhaifu yake tu ili aweze kuishi nawe kupitia madhaifu yako na pale ndipo anapokutawala kirahs tofauti na wanaume husoma mke /gf anapenda nini what ever ili akuridhishe sasa nafikiri umejifunza kitu hapa .this is the way women are ni watu wa kupima sana maji na mguu na akikupata kama huyo bwana hapo juu na ndio kitakuwa chanzo cha kifo chake .jiulize ni kwanini wanaume asilimia kubwa hutangulia kufa kabla ya wake zao kma sio ajali? jibu rahisi sana (hapa sizungumzii gf/bf)

yaan leo umenambia kitu alichoniambia my dad miaka 12 hivi iliyopita...hapo kwenye bold/blue hapo...
he said, ina maana mungu ana upendeleo na kuchukua wababa tu na kuacha kina mama?sikuelewa coz by that time i was too young for that...
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom