Mwanamalundi
JF-Expert Member
- Aug 30, 2007
- 3,125
- 1,437
.......mwanaume zima unashika shika mikoba ya wanawake!! we vipi??? Yalikuwa ni maneno yaliyonichoma barabara moyo wangu tena kutoka kwa mwanamke ninayempenda kuliko wote, yaani mke wangu!!!
Ilikuwa hivi, ametoka kazini akanipitia mimi kazini kwangu tukawa tunajirudisha home taratiibu na stori mwanana za kutaniana hivi na vile bora tumekutana tunaopendana!!!
Ugomvi ulianzia nilipopokea simu ya mfanyakazi mwenzangu akinitaarifu kuwa report niliyotuma, attachment haikwenda ambayo ndiyo report yenyewe!!! So nitume tena na kwa haraka sana coz makao makuu wanaisubiri jioni hiyo hiyo!!! Niliwasha laptop yangu nikakuta ina umeme kidogo sana nilichofanya ni kuibeba kwenye flash na nikalazimika kumuomba mke wangu laptop yake ili niitumie kwa muda huo!!!
Ye wife anatumia mini laptop ambayo inaingia kwenye mkoba wake anaoweka na vitu vingine vya kike, kiukweli sikusubiri jibu lolote toka kwake nikafungua mkoba wake na kutoa min laptop yake nikaiwasha na kuanza kutumia, kumbe mwenzangu muda wote huo hakuniona ila alinielewa kuwa nahitaji laptop yake!!!
Aliposimamisha gari na kunigeukia akakuta natumia tayari, daah!!! Yalimtoka maneno ambayo sijawahi kuyasikia kinywani mwake tangu namfahamu (moja wapo ni hayo niliyotumia kama title aya ya kwanza)!! Alikasirika mwanamke mpaka nikashangaa, sikumjibu kitu kwani nilituma niliyoyatuma nikazima laptop yake nikamrudishia!!!
Katika kudadisi kwangu niligundua yafuatayo;
1. Alikasirika sababu nimefungua mkoba wake, Je wana JF mimi kama mume mtu siruhusiwi kugusa mkoba wa mke wangu na kuufungua??
2. Alikasirika mimi kuwasha laptop yake kwa madai kwamba ile ni kitu binafsi kama ilivyo simu so nilipaswa kusubiri aniwashie!! Wana JF laptop pia ni restricted kwa mume/mke???
Kifupi mie sijaongea nae kitu mpaka sasa coz mihasira mingi na nimejikuta nina mengi yanazunguka kichwani nataka kwanza nitulie ili nilianzisha tuelewane vizuri!!!
Ila bado najiuliza nilikuwa sahihi ama nimekosea??? Wana JF mnaonaje hili????
Nawasilisha
Hizi ni siri zenu. Si jambo jema kuziweka hadharani. Fikiria kama mkeo ni mwana JF, atajisikia vipi akisoma hapa?