mangosongoo
JF-Expert Member
- Oct 2, 2016
- 257
- 456
Ndugu zanguni, maisha yanakwenda kwa kasi sana, na hatujui ya mbele yetu ni nini, yanaweza yakawa mazuri au mabaya japo katika kanuni ya maisha hatutakiwi kujitabiria mabaya.
Katika mazuri kunakufanikiwa kimaisha, kiuchumi, kifamilia, elimu na afya njema lakini katika mabaya nayakusikitisha kwa mwanadamu kuna magonjwa pamoja na vifo na mengineo.
Tukigeukia kwa upande wa mabaya, kijana umefikisha miaka 35 au zaidi au chini kidogo uwe na fedha au usiwe nazo na huna familia, wewe bado upo upo. Ulishawahi kukaa na kutafakari siku kwa bahati mbaya umeumwa ghafla ndani umezidiwa itakuwaje?
Sawa ndugu zako wa karibu watapata taarifa na watakusaidia lakini itafika mahali wanaweza choka na kujipoteza mmoja moja, kinachobaki ni kuanza kujuliwa hali kwa njia ya simu lakini familia yako, mke na watoto watakuwa hapo na wewe usiku na mchana kukupambania, hawatachoka na wewe. Tumeshuhudia haya katika jamii zetu zinazotuzunguka.
Vile vile unaweza kuwa na fedha nyingi mwisho siku zinaweza zisikusaidie pia ukiwa kitandani. Hili ni jambo la kufikiria sana na kulipa umakini mkubwa. Sisi wanaume kuna namna tunatakiwa tufikirie sana.