(A)Anazirazira:
1.Ashakusoma unamtetemekea sana, akinuna tu unabembeleza mpaka anajisikia raha.Hakuna asiyependa raha, lazima anune kila siku.
2.Anatafuta upenyo wa kukuacha. Siku akizira usipobembeleza ndo hutomuona tena. Kuhakikisha hili, ebu siku moja akizira nawewe chuna umuone kama atatafuta namna ya kujirudi au atachuna.
(B)UKIMYA:
(i)Ni mtu wa kukaa kimya hadi umuongeleshe =ni tabia/haiba yake(personality), siyo muongeaji.Hii ndiyo sababu hata akipiga simu haongei sana.Hebu jaribu kuchunguza kama ni tabia yake au la kwa kuangalia anapokuwa na watu wengine either wanaume au wanawake kama pia huwa wanaanza kumuongelesha tu!
(ii)Anakupigia simu baada ya muda mrefu kupita = Anahitaji umuanze, hauko akilini mwake muda mwingi, anakukumbuka kwa nadra.
(C)"Umetoka kwa bwanako?".... Huku akichekacheka:
1.Hana wivu juu yako, yaani kwake ni kwamba mwanamme yeyote akupitie yeye sawa tu ilimradi na yeye anapata.
2.Hakuamini, kama ulivyokwisha ona.
3.Hatanii, anawasilisha ujumbe wake na hisia zake(vile anavyokufikiria) pasipo kutaka kusababisha ugomvi.
(D)Hakuamini kwa sababu:
1.Unatabia ambazo zinamtia shaka
2.Umewahi muonesha kuwa wewe siyo wa kuaminika, alikuamini lakini aliwahi kukuona ktk hali ambayo hakutegemea.
3.Hajiamini(Inferiority complex), anahisi wewe siyo level yake.
HITIMISHO:
(1)Mapenzi pasipo wivu, Hamna mapenzi hapo ni kusogeza tu siku....ukitaka utolewe roho mguse mke wa mwanamme(utashangaa kwanini nasema mwanamme) ndiyo, mwanamme yeyote hawezi vumilia aone mpenzi wake aliyenaye malengo na anayempenda anatumiwa na mwingine hawezi hata thubutu kukutania upuuzi huo asiopenda kuuona na akiongea "umetoka kwa bwanako" atakuwa ktk hasira na sio ktk kicheko. So, huyo in short hana malengo na wewe!
(2)Mawasiliano ni muhimu sana ktk mahusiano yoyote hasa ya kimapenzi! Ukiona haoni umuhimu wa kuzungumza na wewe basi haoni umuhimu wa kuyajenga na kuyadumisha mapenzi yenu.
(3)Ukimpenda mtu, muda mwingi anakuwa akilini mwako na ukim-miss unatamani hata usikie sauti yake tu....utapiga simu mara kwa mara, hasa mnapokuwa hampo pamoja!
Nimeongea si kama mwenye experience ktk mapenzi tu lakini pia kama psychologist!