Mwanaume kuzirazira sababu yake nini?

miss charming

JF-Expert Member
Dec 3, 2016
910
904
Habari za usiku,

Kuna mwanaume nimedumu nae kwa takribani miezi 5 mpaka sasa lakini kitu kinachonikera ni mtu wa kuzirazira na kususa susa sana mpaka najiuliza huyu ana mapenzi ya dhati kweli maana mimi najua mwanaume hasusi na hasa kwa mwanamke ampendae na pia huwa sio mtu wa story.

Yaani anaweza mkakaa hapo kimya mpaka uanze wewe kuongea na wakati mwingine simu anaweza akakaa siku nzima asipige au akipiga anaongea maneno mawili tu keshakata.

Kitu kingine haniamini kabisa yaani haamini kama yuko peke yake, kama labda umetoka utasikia ulikuwa wapi au ulikuwa kwa bwanako nini yaani saa zingine anaongea huku anacheka kana kwamba hanionei wivu.

Naomba wenye experience na mapenzi hii ikoje hasa katika mahusiano.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom