Mwanaume jitahidi kujua msimamo wako kiimani na usimame nao kabla hujaingia kwenye ndoa

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Mar 29, 2012
10,224
22,303
Mambo mengi sana yamezungumzwa kuhusu mapenzi na ndoa kwa ujumla. Hata hili ninaloandika ni kama kukazia tu. Wakuu kama kichwa cha habari kinavyosema ni kuwa mwanaume yeyote kama kichwa cha familia ndo huamua familia yake iweje. Mwanaume ndo kabeba taswira nzima ya familia yake. Mimi leo nakumbusha jambo muhimu sana. Ishu za imani.

Kabla hujaingia kwenye ndoa hakikisha unajua unasimamia wapi. Uwe mkristo, mwislamu au mwabudu mizimu hakikisha unasimama na hiyo imani na ili familia yako ifuate unachofanya. Sijamaanisha ndo uwe mfia dini... nimemaanisha uonyeshe mwelekeo kwa vitendo kwamba familia yako ni waamini wa imani hii na sio vinginevyo. Mke na watoto wajue kabisa HILO NI SUALA LISILOHOJIKA.

Hii nimesema kwasababu siku hizi hasa kwa sisi wakristo kumekuwa na udhaifu mkubwa katika hili hadi kupelekea ndoa nyingi kuvunjika. Kina mama wamebeba hili jukumu na kuishia kuleta mambo ya kiwaki mengi sana. Wanawake wengi wana hawa wanaoitwa mababa wa kiroho. Huwa wanasikilizwa kuliko waume zao. Mwanaume usiposimama imara katika hili utaivuruga familia.
 
kwa wakristo wanaume wengi hawashiki dini ndo maana hao mababa wa kiroho wanazingatiwa, na wanawake wanashika dini haswa, mwanaume wa kawaida hawezi kuendana na hayo mapigo.
Hakuna dini, sasa unaishikaje dini?

Kuna mfumo tu maisha wa jamii Fulani watu wanaufuata kwa kurithi na kuogopa kutengwa tu na jamii, lakini ukweli hakuna dini ni Utapeli mtupu, Si Uislamu wala Christian, ila Yesu anaokoa.
 
Dini na mapenzi nivitu viwili tofauti na havipaswi kuingiliana. Kunao Uhuru wa kuabudu kila nafsi inaweza kuchagua mahali pa kuabudu
Ndo maana wachungaji wa kilokole wanavunja sana ndoa za watu kutokana na wanaume kutokuwa na msimamo. Watu wanakuja kuandika nyuzi za kulialia wakati tayari mambo yameshaharibika.
 
Wanaume wapo bize kuhakikisha familia unapata matunzo.

Dini ni miradi ya wajanja wachache, mtaji wao ni uwepo wa wajinga wengi.
Dini ni hekima za maisha popote duniani wala si kama mlivyokariri katika Ukristo na Uislamu ninyi wafia dini.

Nawaelewa sana Rastafarians na baadhi ya Wapagani wasio na unafki na huthamini Kiumbe chochote hai.

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
 
Ndo maana wachungaji wa kilokole wanavunja sana ndoa za watu kutokana na wanaume kutokuwa na msimamo. Watu wanakuja kuandika nyuzi za kulialia wakati tayari mambo yameshaharibika.
Mapenzi yalikuwepo kabla ya hizo dini unazotaja , mapenzi na dini nivitu viwili tofauti kabisa
 
Hakuna dini, sasa unaishikaje dini?

Kuna mfumo tu maisha wa jamii Fulani watu wanaufuata kwa kurithi na kuogopa kutengwa tu na jamii, lakini ukweli hakuna dini ni Utapeli mtupu, Si Uislamu wala Christian, ila Yesu anaokoa.
Wewe una mawazo kama yangu kabisa yani... Hakuna dini si uislam wala ukristo ila yesu anaokoa.... Watu hawajui kuwa unaweza ukawa huabudu dini yoyote na ukawa mtu wa Mungu
 
Wewe una mawazo kama yangu kabisa yani... Hakuna dini si uislam wala ukristo ila yesu anaokoa.... Watu hawajui kuwa unaweza ukawa huabudu dini yoyote na ukawa mtu wa Mungu
" Mkutanikapo wawili au watatu nami ni pamoja nanyi ''

Kama mwenzio au wenzio wanaamini unachokiamini kwanini msiabudu pamoja na kuwa Dini moja?
 
Back
Top Bottom