Mwanaume bila gari ni aibu kubwa

Mwanaume bila gari ni aibu kubwa

Za leo ndg zangu.

Mwanaume kuishi bila gari inawezekanaje kwa mfano?

Unapanda ngarangara za ngongo la mboto unaning'inia kwenye chuma upo na watoto jamani. Unaenda kanisani mvua inanyesha unakimbia na familia.

Aibu sana.
ngongo la mboto ndo wapi?
 
tatizo la watanzania ndio hili.... unaona usipomiliki gari maisha hayaendi ?

kama naishi kwangu kodi silipi, bills najilipia, familia yangu inasonga vizuri nina shida gani ?

unakuta mtanzania masikini ya Mungu kamshahara ni laki tano, ameunga unga mkopo amechukua ki vitz, mshahara unabaki laki 3, huku anaishi nyumba ya kupanga, mafuta hawezi kuweka zaidi ya elfu 15, tujutathimini upya
Daaaah..acha kabisa.Anza na kilicho cha msingi kwako.Hakuna watu ambao huwa wananiduhi kama kuomba omba umpe tafu ya mafuta.Be forwad ulikuwa mwenyewe,kuna hizi tabia mtu anakuona unatembea mdogo mdogo...ooh ingia tu haina shida.Ukizama mtu anaanza una buku tano hapo nijaze chaap mafuta.
Mmiliki kitu ambacho unaweza kukitendea haki na kwa wakati husika.Sio kuja kuwapa shida watu wengine kwa visingizio kibao.
 
Duu mmetoka kwenye nguvu za kiume hadi sasa hivi magari

Tunaomba mlegeze vigezo jamani mnatuathiri kisaikolojia [emoji23][emoji23]
[emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] ule mkweche wako ulikufaga au
 
Za leo ndg zangu.

Mwanaume kuishi bila gari inawezekanaje kwa mfano?

Unapanda ngarangara za ngongo la mboto unaning'inia kwenye chuma upo na watoto jamani. Unaenda kanisani mvua inanyesha unakimbia na familia.

Aibu sana.

NI AIBU? ungesema ani MUHIMU, ila sio AIBU!!!!! Usikute Baba yako kawalea nyie mlikuwa 8, na kwa sababu ya kuwajali na kuwapa ADA hakuweza kununua gari, sasa umepata kazi na mkopo barclays umenunu VITZ old Model, unasema hata Baba yako ilikuwa kwa aibu yake, ANGENUNU GARI NYIE MNGEENDA SHULE? Kuweni na Shukrani kwa Mungu!
 
Aibu kwenu huko ,miji ya watu wanapanda public transport hata km wana gari 3.
Kwanza kupunguza matumizi yasiyo ya lazima.
Pili magari moshi yanatoa ni effect kwa uhai
Tatu parking mijini rejea no 1
Nne msongamano kila mtu akiendesha gari itakuwaje .
Tano usafiri public mzuri, hakuna mtu anapanda na ndoo la samaki wala kubanana.
Sita hongera tumejua umenunua gari .
 
Mtu kuchukua mkopo kisha ukanunulia gari ya kutembea na ukawa unaulipia kwa mshahara wako basi ni ujinga. Mimi nina gari ila sijawahi kuwaza kununua gari ya kutembelea kwa mkopo! Ni kueneza umasikini mkubwa.
 
Watoto wa Mama utawajua tu!!sasa madaladala sio usafiri?na ukimfuatilia mtoa mada utakuta ana ki-babywalker!!
 
Narrow minded.

Growing OLD is inevitable. Growing UP is optional. Tunawahi kukua ila tunachelewa kukomaa.

So sad.
 
Shukuru Mungu aliekujalia kuwa nalo hill gari na wala ww sio kiumbe bora zaidi ya wengine acha Majivuno hayafai kwenye dunia hii, mm gari ninalo na mkw wangu analo La kwake nimemnunulia ila sioni sababu ya kukejeli wasio nayo.
 
Za leo ndugu zangu,

Mwanaume kuishi bila gari inawezekanaje kwa mfano?

Unapanda ngarangara za Gongo la mboto unaning'inia kwenye chuma upo na watoto jamani. Unaenda kanisani mvua inanyesha unakimbia na familia.

Aibu sana.
Kwa Tanzania sio aibu, uwiano wa magari na idadi ya wanaume bado magari ni machache sana. Hivyo jambo hili kuonekana la ajabu/aibu bado sana, hapa utaonekana mleta mada ni limbukeni.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom