Mwanaume amwoa mwanaume mwenzake bila kujua

Mwanaume amwoa mwanaume mwenzake bila kujua

Mwanaume mmoja mkoani Mtwara amekaa na mwanaume mwenzake miezi minne bila kujua.

Kwa mujibu wa maelezo mahusiano yalianza baada ya kukosea namba wakafahamiana mpaka wakafikia maamuzi ya kuoana huku akijua ni wa kike.

Baada ya kufata taratibu wawili hao wakaoana lakini tatizo likaja wakati wa kujamiiana mwenzake wakawa kilasiku anasema anaumwa ikawa hivyo ndani ya miezi mitatu ndipo akaja gundua kuwa ni mwanaume mwenzake.

Kuhusu mavazi anasema mwenzake huyo huvaa kama mwanamke na kupika pia anajua hata kujiremba anajiremba hali iliyo mpelekea kutogundua.
Uwongo wa wazi kabisa huu.Umbile la mwanaume ni tofauti kabisa na umbile la mwanamke huwezi kukosea.
 
Mh mkwara wa waziri wa mambo ya ndani umewakumbusha adhabu watakayo pata ndio maaana wameamua kuwekana peupe ili ionekane kuna makosa ya kiufundi ktk uhusiano wao

Vipi lakini waliwapeleka hosp.. Kupima kama hawajakoroga kisamvu au ndio kimeungulia tayri.
Bwahahahahahaaaaahaaaa!
 
Hiyo habari wameitoa humu, ishawahi kuletwa hiyo taarifa
 
Mwanaume mmoja mkoani Mtwara amekaa na mwanaume mwenzake miezi minne bila kujua.

Kwa mujibu wa maelezo mahusiano yalianza baada ya kukosea namba wakafahamiana mpaka wakafikia maamuzi ya kuoana huku akijua ni wa kike.

Baada ya kufata taratibu wawili hao wakaoana lakini tatizo likaja wakati wa kujamiiana mwenzake wakawa kilasiku anasema anaumwa ikawa hivyo ndani ya miezi mitatu ndipo akaja gundua kuwa ni mwanaume mwenzake.

Kuhusu mavazi anasema mwenzake huyo huvaa kama mwanamke na kupika pia anajua hata kujiremba anajiremba hali iliyo mpelekea kutogundua.
inamaana analala na baibui au gauni au vipi

unaanzaje kuoa bila kula
 
Miezi 4 unaishi na mtu bila kujua jinsi yake? Haingii akilini katika hali ya kawaida.
 
Muongo huyo watakuwa walioana kama mashoga sasa baada ya kushtukiwa ndo anajifanya hakujua wala kushiriki nae tendo la ndoa
 
Aseme tu ametumia kakinaii
Hivi hata kama anaumwa anapobadili nguo kwenda kuoga hamuoni ?
 
eti anadai mdada( shoga) alimkatalia ngono kwa kisingizio cha kuumwa mgongo[emoji3][emoji3] na uyo kaka alikaa hadi kwa mamamkwe hakushtukiwa walijua ni nke[emoji3] nendeni yotube ya geahabibu kama ameiweka iyo hekaheka ya jana Mbeki/ tegeta na leo mtwara zote za mashoga
 
Kuna vitu unaweza kuvisikiliza hata sikio likagoma kuupokea huo ujinga. Miezi 4 hata kama ulifungiwa ya mkeka, je hukuwa hata na ham kidogo tu naye?? Ka alikuambia anaumwa mgongoni si unambeba hata kwa machela hadi kwa dokta?? Miezi 4 unakodolea mimacho tuuu siamini. Labda basi alipokuambia anaumwa akakuelekeza uani nawe ukajiliwazia humo. Huyo ni punga kabisaaa anataka kuhalalisha upuuzi wake huo
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom