Mwanaume ambaye hana pesa asioe

Kambi ya Fisi

JF-Expert Member
Feb 3, 2018
13,625
22,278
Nimeona wanaume wengi kwenye mitandao ya kijamii wakilalamika jinsi wanawake wa siku hizi wanavyopenda pesa, ukiwachunguza hao walalamikaji utagundua hawana hela Ila wanatamani kuoa. Hivi umewahi kuchunguza - ni katika tamaduni gani mwanaume asiye na kitu alipewa mke?

Kwa maoni yangu binafsi, haijalishi una mali kiasi gani. Ikiwa mwanaume unamudu kulipia nyumba hata ya chumba kimoja - na unaweza kujilisha - basi unaweza kumtunza mke...... na mtakuwa pamoja, oa.

Lakini ikiwa unaishi kwa kula chakula kutoka katika sifuria ya mama yako na unalala ndani ya chumba chako cha tangu utotoni nyumbani kwa mama yako, ni dhahiri haupo tayari kwa ndoa usithubutu kuoa.

Bili hazilipwi kwa busu - bili hulipwa kwa pesa tasilimu. Hama kwa mama yako uende ukatafute hela kwa jasho lako ukisha pata hela oa na uishi na mkeo kwako na sio kwa mama yako.

Pesa hujibu mambo yote (Mhubiri 10:19)

Ubarikiwe.
 
FB_IMG_1713377159803.jpg
 
Tena ukiwa na HELA ndio usithubutu kuoa..

Kipimo cha Ndoa ya kweli ni wakati ukiwa MASKINI.

refer Case study nyingi za KUGAWANA MALI
Na wanawake wa siku hizi nao hawataki kuanza na wanaume from the scratch, sababu wanajua mkizipata hakuna rangi wataacha kuona, kwahiyo ninyi tafuteni tu pesa kisha oeni hayo mengine ya kuachana sijui kugawana mali ni matokeo tu
 
Back
Top Bottom