Mwanasiasa bora kijana 2012 Tanzania

Tukiwachambua akina Lema, Lisu, Mnyika na Zito, Filikunjombe na wengine, isiwe kutaja majina tu bila kuwachambua itaonekana JF si wa kiwango tunachotarajia. Kuna mambo kadhaa ambayo yanaweza kumpa mtu nafasi ya kupaa na papo akawa na yanayomteremsha, bora kuwa na mizani ambayo inampa mtu haki yake bila upendeleo. Hii ni kwa wenye upeo wa kuelewa wanaweza nielewa wengine wataishia mipasho lakini wote mmetumia uhuru wenu kuchangia na halijaharibika neno, ila nifanyayo ndiyo njia bora ambayo wasomi, wataalamu na watu makini hutumia kupima uwezo wa mtu.

Lema namtolea nje kwa jambo moja ambalo ni papara, bila kutuliza akili na kuangalia madhara yake. Anafaa kwa uhamasishaji lakini si kuongoza. Lema hatumii zaidi akili na busara. Kuna nafasi ambazo anatakiwa kutumia zaidi akili, na busara lakini yeye anaendekeza zaidi utashi hiyo ndiyo kasoro ambayo anayo. Jambo kama hilo alikuwa nalo pia Mrema enzi zake, kuna mambo na nafasi mtu unatakiwa kupunguza jazba, kufikiri kabla ya kutoa tamko na kuangalia athari zake zinazoweza kutokea na namna gani uongee kwa lugha ambayo haitaleta mtafaruku zaidi kwa walio kinyume cha itikadi yako.

Zitto ni mlipuaji zaidi na anafaa kuwa katika nafasi ya wizara nyeti kwa ajili ya umakini wake. Anaweza kuwa kiongozi mzuri hapo baadaye baada ya mchemko wa ujana kupungua na utu uzima kushika nafasi na hivyo kujenga dhana ya ustahimilivu. Kuna mambo ya kunyooshea vidole kwa nafasi aliyo nayo, lakini kwa mwendo huu kama kiongozi wa nchi afanye hivyo mambo yataharibika, yatakiwa kuwa na hali ya ustahimilivu, busara, hekima na moyo wa subira.

Mnyika anaonekana kukomaa kiakili angali kijana mbichi, anaongea kwa busara, hoja yenye mvuto na ustahimilivu katika ukokotoaji wake. Ustahimilivu alio nao ni hazina nzuri sana kwa siku za usoni kwani akishakomaa zaidi ni chombo cha thamani kubwa.

Lisu ni hazina kubwa sana ya ufumbuzi wa mengi yahusuyo masuala ya kisheria. Hana woga, mwazi na mwelimishaji mzuri. Anahitaji muda zaidi katika kuimarika zaidi katika utumishi wa umma, na ni mmoja ambaye kama Chadema wanaweza kushika dola anafaa kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Deo Filikunjombe ni kijana ambaye anajiamini, anaaminika, ana utashi mkubwa, anajituma na anajitolea. Anamwamko wa kimageuzi, mpole, mvumilivu, mkweli, hana woga na ni mtetezi wa wananchi bila kujali itikadi za chama chake. Ana ushupavu wa pekee kiasi cha kupinga wazi wazi dhuluma na udhalilishaji unaofanywa na viongozi wa Chama chake au serikali yake. Ni jambo la pelee na lisilo la kawaida kwenda kinyume cha chama kilichomdhamini kuingia bungeni. Wengine wayafanyayo nafasi na mazingira yao ndiyo hayo, lakini huyu Deo naweza kumfananisha na Kambona, Edwin Mtei, Kaserabantu, Horace Kolimba, Abdu Jumbe na wengineo kwa kuwataja wachache.
 
Zitto ni makini,shupavu na uwezo wake wa uelewa ni wa hali ya juu,anaweza kujenga hoja na kuwa na strategy zenye kueleweka
2.january Makamba
3.DEO FIRIKUNJOMBE
4.JOHN MNYIKA
5.BARUHANI
6.MHONGA RUHWANYA
7.HALIMA MDEE
8.ESTER BULAYA
9.MOHAMED DEWJI
!0.mwigulu Nchemba
 
Zitto ni makini,shupavu na uwezo wake wa uelewa ni wa hali ya juu,anaweza kujenga hoja na kuwa na strategy zenye kueleweka
2.january Makamba
3.DEO FIRIKUNJOMBE
4.JOHN MNYIKA
5.BARUHANI
6.MHONGA RUHWANYA
7.HALIMA MDEE
8.ESTER BULAYA
9.MOHAMED DEWJI
!0.mwigulu Nchemba


Tatizo la Zito akiona pagumu hukwepa. Viognozi wengi wa juu chadema wamejituma hadi kuwa na kesi kadhaa mahakamani, lakini nafasi zote hizo Zito alikwepa kwa sababu anazojua mwenyewe. Ni dalili tosha akishika madaraka hayuko tayari kupamana na magumu, la sivyo aanze sasa kujizoesha.
 
Zitto Zuberi Kabwe Mb) Kigoma North; young, smart, ambitious, famous (probably than most of young MPs), shrewd, he knows politics and what he is doing, and furthermore what he wants (goal oriented)
 
Leo ni tarh 2/6/2012, na kwa serkali ni mwaka mpya 2013.
Naomba upige kura yako kwa kutaja jina la mwanasiasa kijana ambaye ni bora ktk kipindi hiki cha miez 6 (nusu mwaka) mpaka sasa.

Karibu kwa kura maana kura yako itamotivate viongozi kutekeleza majukumu yao na itatoa tathmini ya jinsi wanavyokubalika ktk jamii mpaka sasa.


Hapo pekundu, Ubora upi? Maana hata LUSINDE ni bora katika Matusi.
389ea4fb-b878-4364-ad90-4499e3e4ac7b.jpg
 
Hii thread ni nzuri sana lakini ina pungufu moja.Kichwa cha Thread kinasema mwanasiasa bora kijana 2012 wakati ukiingia kwa ndani inasema mwanasiasa bora kijana ndani ya miezi sita.Napendekeza tuwe tunachagua kwa Interval ya mwaka mzima hasa ukizingatia Mwaka wa Kiserikali unaanzia julai na kuisha juni mwaka ufuatao.Hii ya kutuletea miezi sita mimi naona ni kama ujanjaujanja tu.Mtu anavizia mwanasiasa ampendaye amefanya jambo moja kubwa na zuri then anapost hii thread ili kumpublicize.Hello Great thinkers twendeni na uhalisia mambo ya ujanjaujanja tuache.Hili tukio lilipaswa lizingatie harakati za mwaka mzima.Pia hatuna mgombea binafsi sasa wanasiasa kama Zitto Kabwe ambaye hana mapenzi na chama chake zaidi ya kutafuta Umaarufu binafsi hawafai.Zitto hata akiongoza najua Magamba ndiyo yamemchagua coz yanamtumia kuibomoa CDM.Zitto anatafuta umaarufu binafsi HAFAI
 
Mwaka wa serikali gani?au mwaka wa serikali ya ukoo wenu ndio unaanza leo??!!!!!
 
Jamani Wana CDM ni wagumu kuelewa kuliko ata wale wanaccm walioko kule lindi na mtwara wasiojua kusoma wala kuandika na ndio maana hamtaweza kuchuka nchi hii kamwe labda waTz wote wafe wabakie wachaga ambao ni wakenya we umeambiwa taja mwanasiasa bora kijana 2012 unamtaja Lema nani kakwambia saiv lema ni mwanasiasa wakati hana ata cheo cha ubalozi wa nyumba1 mwenzako mfanyabiashara yule kibaka,mlevi...
 
Jamani Wana CDM ni wagumu kuelewa kuliko ata wale wanaccm walioko kule lindi na mtwara wasiojua kusoma wala kuandika na ndio maana hamtaweza kuchuka nchi hii kamwe labda waTz wote wafe wabakie wachaga ambao ni wakenya we umeambiwa taja mwanasiasa bora kijana 2012 unamtaja Lema nani kakwambia saiv lema ni mwanasiasa wakati hana ata cheo cha ubalozi wa nyumba1 mwenzako mfanyabiashara yule kibaka,mlevi...
Watake radhi watu wa Mtwara na Lindi uliowatusi. Wana CCM wasiojua kusoma na kuandika unaowajua wewe wapo Mtwara na lindi tu? Si ungewafananisha wana CCM wasiojua kusoma na kuandika wa huko uliko? Pima kabla hujaandika.
 
Back
Top Bottom