Wanasiasa bora wa muda wote toka upinzani

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Mar 29, 2012
10,233
22,317
Nionavyo mimi wafuatao ni wanasiasa bora wa muda wote kwa upande wa upinzani. Orodha hii itaanza na yule bora zaidi kushuka chini.

1. Hayati Maalim Seif
Kila mmoja anakumbuka vizuri balaa la Maalim Seif kwenye siasa za nchi hii kutokea upinzani. Huwa najiuliza huyu dingi aliwapaga nini wazenji kiasi cha kumpenda na kumwamini kiasi kile hadi mauti yanamkuta? Kasoro pekee ambayo nimeona inatajwa sana ni kashfa ya Maalim Seif kuwasaliti wenzake walipotaka kwenda mahakamani kuhoji kuhusu Muungano. Sikuwahi kumsikia akijibu hili.

2. Hayati Lyatonga Mrema

Nilitaka nimweke Mzee wa Kiraracha namba moja ila nikakumbuka huyu dingi hakudumu kwenye msimamo wake kwa muda mrefu. Hakuwa consistent. Nikimtoa Lowasa naweza sema Lyatonga ni mgombea mwingine wa upinzani aliyetupa wakati mgumu sana mwaka 1995 kwenye kinyang'anyiro cha kumpata rais wa JMT. Huyu mwamba ndo kama alitengeneza njia ya upinzani. Ni legend. Kasoro yake ni tuhuma za usaliti na migogoro kwenye vyama alivyopita.

3. Dr Wilbroad Slaa
Mzee Slaa kaacha alama nyingi sana kwenye siasa za nchi kwa ujumla. Kama sio kukatwa jina lake mwaka 1995 basi Slaa angekuwa mbunge wa CCM. Alihamia CHADEMA kwa kuona hajatendewa haki. Lilikuwa pigo ambalo CCM hatutakaa tusahau. Kama bahati mbaya tena mwaka 2015 jina lake likakatwa tena kama mgombea urais kwa tiketi ya CHADEMA na nafasi yake akapewa mtu aliyetuhumiwa na CHADEMA kwa miaka mingi kuwa ni fisadi. Kama kawaida Dr akaona isiwe akajitoa CHADEMA na kumsapoti mgombea wa CCM. Nadhani kilichomuuma zaidi Dr ni pale anapokumbuka hawara wake alivyopigwa na polisi kwasababu ya CHADEMA lakini baadae yeye na hawara wake wakaishia kusalitiwa na CHADEMA.

4. Zitto Kabwe
Huyu mwamba toka Kigoma ndo alifungua njia kwa vijana wengi kujiingiza kwenye siasa na kugombea nyadhifa mbalimbali kwa tiketi za vyama vya upinzani. Kwa lugha ya mjini ni kuwa alichangamsha game. Hoja zake za kisomi bungeni zilikuwa zinatikisa nchi. Atakumbukwa kwa ishu ya Buzwagi. Kwa mujibu wa katiba ya ACT huyu ni kiongozi mkuu wa chama. Binafsi namwona kama mmiliki wa chama kwasababu mwenyekiti wa chama hana kauli ya mwisho mbele ya Zitto Kabwe. Kwenye siasa za unafiki Zitto ni brand kubwa. Kimsingi pamoja na mazuri yake ana kashfa za usaliti.

5. Hayati Mchungaji Christopher Mtikila
Mchungaji Mtikila hawezi kukosekana kwenye hii orodha kwa kuwa mtu aliyeshinda kesi mahakamani akitaka uwepo wa mgombea binafsi kwenye chaguzi. Ana mazuri mengi ila kasoro yake ni ubaguzi wake dhidi ya watanzania wenye asili ya kiasia.

6. Halima Mdee
Mwanamama huyu kutoka CHADEMA hawezi kosa kwenye hii list akiwa namba 6 kwasababu ya ukubwa wake kisiasa huko upinzani. Bado hajapatikana mwanasiasa mwanamke kutoka upinzani apiyefikia rekodi za Halima. Huyu ni miongoni mwa wabunge wachache wanawake waliowahi kushinda viti vya ubunge kwa kupigiwa kura na sio viti maalum. Ikumbukwe alikuwa akishinda kwenye jimbo gumu mno la Kawe. Mdee ni mwanasiasa bora kabisa ila vijana wengi wa hovyo wameonyesha kuwa na mashaka juu ya ukaribu uliopo kati wa Mdee na mbunge mwenzake aitwaye Esther.

7. Abdul Nondo
Huyu mwenyekiti wa ngome ya vijana namwingiza kwenye hii list kwasababu akiwa bado kinda kapitia misukosuko mingi lakini hakukata tamaa hadi sasa no boss mkubwa kwenye idara ya vijana ya chama chake. Watu wengi wenye utaaalamu na siasa za upinzani wamekuwa wakidai kuwa Nondo ni mkubwa kisiasa kuliko aliyekuwa mgombea urais wa CHADEMA 2020. Mimi nakubaliana nao. Huyu Nondo ana kashfa ya kujiteka na kusingizia dola.

8. Tundu Lissu
Mtaalamu wa sheria Lissu hawezi kusahaulika hapa kama mwanasiasa jasiri aliyesimamia misimamo yake katika nyakati ngumu kidemokrasia kuwahi kutokea hapa nchini. Kisiasa Lissu bado ni mdogo hata kwa kijana Abdul Nondo. Kimsingi Lissu hana haiba ya kisiasa na huwa hajui aongee nini kwa wakati gani. Ni mtu ambaye yuko tayari kuona nchi yake inawekewa vikwazo kwa maslahi yake ya kisiasa.

9. Hawa Bananga
Mwanamama huyu wa shoka ambaye ni mbunge viti maalum kwa tiketi ya CHADEMA akiwakilisha mkoa wa Tabora ni akili kubwa sana iliyowezesha CHADEMA kupata nguvu kubwa mno kupitia kina mama. Hawa Bananga aliibeba BAWACHA mabegani. Mimi niko CCM ila kama Hawa Bananga atagombea ubunge kwenye jimbo ambalo nipo basi nitampigia kura. Sijawahi sikia kashfa yoyote ya Hawa Bananga.

10. Freeman Aikael Mbowe

Kwa kifupi Mbowe ni mwenyekiti bora zaidi wa chama kinachokufa CHADEMA. Hata kwa hizi nyakati za mwisho wa uhai wa CHADEMA bado Mbowe anafaa kuendelea kuwa mwenyekiti hadi atakapochoka. Ni namba kumi kwa ubora kwenye hii orodha tukufu. Kama Mwalimu Nyerere angekua hai nadhani angemkemea sana Mbowe kwa kauli zake za kibaguzi dhidi ya watanzania.
 
Huu uchambuzi wako uko biased na umejaa utoto mwingi!
 
No 2, 4 na 6 hebu tuondolee hao kwanza kisha tuendelee na mchakato.
 
Back
Top Bottom