Zitto Kabwe anavyoitazama Tanzania ya 2050 Kiuchumi

ACT Wazalendo

JF-Expert Member
May 5, 2014
610
1,540
Anaandika Zitto Kabwe, Kiongozi wa ACT-Wazalendo.

Katika mazungumzo yangu na Maafisa Mipango na Wachumi wa Wizara, Idara, Mashirika ya Umma, Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa Nchi nzima wanaokutana hapa Arusha nimewaeleza kuwa Tanzania ya Mwaka 2050 itakuwa na Watu takribani milioni 130. Tukiweka lengo la kuwa na Pato la Mtu mmoja mmoja la USD 3,500 kwa Mwaka ifikapo 2050 ( zaidi ya mara mbili ya GDP/capita ya sasa ya USD 1200) tunahitaji Uchumi wa Tanzania uongezeke mara 6.5 hadi kufikia USD 455B.

Nimewaambia kuwa inawezekana kwani kati ya Mwaka 2000 na Mwaka 2022 GDP iliongezeka mara 5.8 kutoka USD 13B mpaka USD 75B.

Hivyo, kasi ya kukua kwa Uchumi inapaswa kuwa Wastani wa 8% kwa Mwaka kwa Miaka 10 ya mwanzo 2026-2036, na kasi hiyo isishuke 6% kwa Miaka mingine 15 mpaka Mwaka 2050.

Kasi hiyo ya ukuaji wa Uchumi itapaswa kuongozwa na sekta ya Kilimo, 6-8% kwa Mwaka. Nimesisitiza sana kuwa tunapaswa kuweka nguvu kubwa katika TIJA kwenye Kilimo ( angalau tuongeze mavuno mara mbili ( doubling ) ya sasa katika kila Ekari ya mazao ya Kilimo.

Nimewapa mfano wa zao la Pamba ambapo ilhali mkulima wa Tanzania anapata kilo 250-300 kwa kila ekari ya Pamba, mkulima wa Benin anapata kilo 800 na mkulima wa Burkinafaso anapata kilo 1500.

Hali ni mbaya zaidi kwenye Mahindi na Mpunga ambapo wakulima wetu wanapata gunia chache zaidi kutoka kila ekari 1!

Mambo ya kufanya wakati tunaandaa Dira mpya ya Maendeleo niliyopendekeza kwa wana mipango na wachumi;

1. Lazima tuwe na mjadala wa ukweli miongoni mwetu Watanzania bila ubaguzi wa kisiasa kuhusu Miaka 25 iliyopita. Je tulikuwa na mwafaka wa kitaifa kuhusu DIRA? Je tulikuwa na nidhamu ya kutosha kutekeleza DIRA 2025? Kwanini ilichukua Miaka 10 kuanza kutekeleza DIRA?
Tuwe tayari kukubali matobo na kuweka mikakati ya kuziba matobo hayo.

2. Baada ya tathmini ya hapo juu ( HONEST CONVERSATION), tujenge MWAFAKA WA KITAIFA kuhusu tunapotaka kuipeleka Tanzania. Lazima na ni muhimu kwa Watu wenye kufanya maamuzi na wenye ushawishi wa kimaamuzi ( viongozi wa Serikali, Watumishi wa Serikali, wanasiasa wa Upinzani, Wafanyabiashara, Watendaji wa Mashirika ya Umma, wakulima, wafugaji, Wavuvi, Wanafunzi etc) - Elite bargain, kukubaliana mwafaka wa kitaifa ( commitment to growth and development). Hii bargain
  • ijenge makubaliano ya uhakika kuhusu Maendeleo
  • kujenga dola lenye utayari wa kusaidia Maendeleo na sio predatory state
  • ikubali kujifunza na kurekebisha makosa kila wakati yakitokea ( error correction).

3. Nimesisitiza kuhusu utekelezaji wa mipango ya Maendeleo kufikia DIRA.
  • vipaumbele
  • sequencing ( nini kinaanza na nini kinafuata)
  • nidhamu ya utekelezaji

Nimewakumbusha kuwa Jiografua yetu pekee inaweza kuifanya Nchi yetu kuwa na mapato ya kigeni ya zaidi ya USD 12B kwa Mwaka na makusanyo ya kodi ya USD 10B kila Mwaka kutoka katika Forodha peke yake. Hivyo ufanisi wa Bandari utumike kusaidia sekta nyengine.

4. Nimewakumbusha kuwa Tanzania inahitaji kujenga uwezo wa ndani wa mitaji ili sekta Binafsi ipate mitaji ya kuwekeza katika kukuza Uchumi. Uwezo wetu wa ndani wa kuweka akiba ni mdogo. Savings - GDP ratio ni chini ya 16%. Hivyo nimeshauri kujenga mfumo madhubuti wa Hifadhi ya Jamii ( social security) ili kujenga uwezo wa Watu wetu kuweka Akiba.

Nimewakumbusha kuwa Watanzania wengi ni masikini na wengi wao wanazunguka Mstari wa umasikini. Walio juu wakipata shock kidogo wanadondoka, waliochini wakipata boost kidogo wanapanda. Wajibu wa Uongozi ni kuwapandisha waliochini na kuwahami waliojuu wasidondoke. Hifadhi ya Jamii kwa wote ndio jawabu ya hilo.

NIMESISITIZA
  • pale ambapo sekta Binafsi inafanya vizuri, Serikali isiingilie. Serikali iweke sera nzuri na kutekeleza Sheria.
  • uwiano kati ya Uchumi na siasa uzingatiwe. Tukishajenga mwafaka wa Maendeleo Basi Vyama vya siasa Bisho sane kuhusu mikakati ya utekelezaji ili kufikia DIRA.

#ACTWazalendo #TaifaLaWote #MaslahiYaWote
20231129_093109.jpg
 
#ACTWazalendo #TaifaLaWote #MaslahiYaWoteView attachment 2828268

Mambo ya hovyo, jitu nafiki hili kuzidi Kabudi.
 
Back
Top Bottom