Feleshi sidhani kama atakubali tena kuja kwa mwanasheria mkuu, kwasababu amefanya kazi ktk mazingira magumu sana, na amini usiamini, KIKWETE AMEKUJA KUKIRI KUWA ALIKUWA MISLED KUMWONDOA, amegundua hilo baadaye akajua kuwa yote yalikuwa majungu matupu.
Feleshi alifanya kazi akichukiwa kwa asilimia 100% na Werema na Masaju waliokuwa wanataka kuingiza mambo yao na yeye akawa anashikilia msimamo.
Feleshi amefanya kazi kwa misukosuko na Dr. Hosea ambaye muda wote alikuwa anapeleka ushahidi hafifu kwa dpp ili kunawa mikono wakati kesi ameiharibu asilimia mia. ujue kesi inajengwa na wapelelezi, bila upelelezi hakuna kesi, hivyo pccb wakiharibu ushahidi dpp atapoteza pesa za serikali kushikilia kesi ambayo yeye hakusanyi ushahidi na anaona imepotoshwa. pccb kwa maslahi yao wamekuwa wakila rushwa na watuhumiwa hata mafisadi, halafu wanaleta ushahidi hafifu ili mafisadi wakatokee mbele. ushahidi wa mambo haya ni kesi ya IDI SIMBA NA KINA ROBERT KISENA WA SIMON GROUP a.k.a sakata la UDA.
baada ya kumteua kuwa jeji, taasisi karibia zote za serikali zilisusia, taasisi za nje ya nchi zikamtaka arudishwe, mambo yalivurugika kwasababu dpp alikuwa anafanya kazi zaidi hata ya boss wake werema na masaju, kilichotokea kikwete aliomba arudi tu afanye kazi kama dpp wakati jaji kama tu werema anavyofanya kazi kama AG wakati ni jaji, feleshi akakataa.
wafanyakazi wa hiyo ofisi ndio wanaojua kilichopo, aliyeijenga ofisi hii ni FELESHI, na ndiye anayeijua kuliko wote. mwenye uwezo kichwani, namwenye uwezo wa kuchukua maamuzi magumu ni feleshi.
kwa taarifa yako, kikwete alikuwa mislead kuwa kwa misimamo ya Feleshi ccm itashindwa kushughulikia upinzani mwakani, wakataka kumtoa mapema ili wamuweke mtu atakayetumika. walipokuja kutafuta nani atareplace wakakosa kabisa atakayefit kama alivyokuwa feleshi, mashirika ya kimataifa yakagoma, polisi walishagoma kutoa ushirikiano. werema na kundi lake wakawa wameweka pandikizi lao yule mlarushwa ANSLEM MWAMPOMA ili amsumbue na kumharibia wakifikiri feleshi akitoka yeye ndiye atashika nchi, aliishia kukaimu tu wala hajawa dpp, na aliyepewa udpp ni dogo aliyempokea kazini.
mnachotakiwa kujua, hakuna dpp atakayefit nafasi ya feleshi. kikwete kati ya vitu alivyowahi kupotezwa na hosea, masaju na werema, ni kumtosa feleshi kwa bifu lao la kuona feleshi anakubalika kuliko wao.
hata hivyo, sidhani kama feleshi atakuja kukubali kurudi tena kwenye ofisi ya mwanasheria mkuu, alikokuwa jaji huko anapumsika kwasababu kile kitu alichokuwa amekalia ni kugumu kuliko hata urais, kiti ambacho rais analeta yake, hosea analeta yake, mawaziri wanaleta yake na wewe unatakiwa kuchukua maamuzi magumu...ni nafasi ya hatari na ngumu ambayo kwa yale aliyoyafanya lazima apongezwe. hosea, werema na masaju Mungu atawaengua wenyewe. nilishawahi fanya kazi kwenye hiyo ofisi, ninawajua a-z, na ninamjua feleshi pia.