Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Frederick Werema ajiuzulu

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Frederick Werema ajiuzulu

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema amejiuzulu nafasi yake hiyo kuanzia leo, Jumanne, Desemba 16, 2014 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amekubali ombi hilo la kujiuzulu.

Katika barua yake kwa Mhe. Rais Kikwete, Jaji Werema amesema kuwa ameomba kujiuzulu kwa sababu ushauri wake kuhusiana na suala ya Akaunti ya Tegeta Escrow hakueleweka na umechafua hali ya hewa.

Mhe. Rais Kikwete amemshukuru Jaji Werema kwa utumishi wake ulioongozwa na uaminifu na uadilifu.

Kwa mantiki hiyo Tumbili kashinda 😄
 
jk kamshukuru kwa uaminifu na uadilifu mtu aliyelitia taifa hasara!!!inatia shaka sana
 
Siyo aibu kiwese, Ni umbumbu wa viongozi wetu. Kwa matendo kama haya ndo tunapaswa kupima uwezo wa viongozi wetu. huyu bwana hawezi kabisa. Sema ni kwamba jamii ya kitanzania bado uelewa ni mdogo na kufuata ushabiki tu. Labda kwa sababu nayeye ni mhusika wa wizi ndo maana kampongeza mwizi mwenzake kwa kazi nzuri waliyofanya kuwakomoa watanzania.
 
Khe Khe Khe Khe Khe siku ya kufa tumbili miti yote huteleza.
 
Bado sasa mharibifu wa uchaguzi serikali za Mta a. Bi GHASIA naye afatilie humohumo KUJIUZULU

Yeah Huyu asiruhusiwe kujiuzulu afukuzwe aambiwe"Nimeipata barua yako ya kujiuzulu ila nakufukuza kazi kwa hasara na kudhalilisha ofisi ya waziri mkuu na taifa.Kama haondolewi basi mkubwa wao ndo ajitoe mana atasamehewa mangapi? amtose mtu au ajitose mwenyewe huyu PM.wANAWEZA KUWA WANAMHARIBIA KWA KUTANGAZA KUWANIA URAISI
 
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema amejiuzulu nafasi yake hiyo kuanzia leo, Jumanne, Desemba 16, 2014 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amekubali ombi hilo la kujiuzulu.
Katika barua yake kwa Mhe. Rais Kikwete, Jaji Werema amesema kuwa ameomba kujiuzulu kwa sababu ushauri wake kuhusiana na suala ya Akaunti ya Tegeta Escrow haukueleweka na umechafua hali ya hewa.
Mhe. Rais Kikwete amemshukuru Jaji Werema kwa utumishi wake ulioongozwa na uaminifu na uadilifu.

UAMINIFU NA UADILIFU?
 
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema amejiuzulu nafasi yake hiyo kuanzia leo, Jumanne, Desemba 16, 2014 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amekubali ombi hilo la kujiuzulu.

Katika barua yake kwa Mhe. Rais Kikwete, Jaji Werema amesema kuwa ameomba kujiuzulu kwa sababu ushauri wake kuhusiana na suala ya Akaunti ya Tegeta Escrow hakueleweka na umechafua hali ya hewa.

Mhe. Rais Kikwete amemshukuru Jaji Werema kwa utumishi wake ulioongozwa na uaminifu na uadilifu.

Ehuuuu!!! Hatimaye mwizi aliyekamatwa na Tumbili amekubali kiishe!! Mijitu mingine bwana Mpaka iumbuliwe ndio isalimu amri! good riddance muraa wetu, your shelf life was indeed too short, a first in Tanzania kama Tumbili kukamata mwizi, a milestone in Tanzania.
 
kujiuzulu tu haitoshi.afilisiwe na achukuliwe hatua kali za kisheria.kama hiyo haitoshi ahukumiwe vilevile.wapo wengi waliofungwa jela kwa tuhuma za wizi wa kuku mitaani.je?leo mwizi mkubwa kama huyu watamuacha vipi?
 
"Tumbili" Kamfukuza mwizi. Tumbili tunaomba umnyang'anye hadi mahindi aliyochuma arudishe maana hayakuwa yake ni yetu sisi tumbili..

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema amejiuzulu nafasi yake hiyo kuanzia leo, Jumanne, Desemba 16, 2014 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amekubali ombi hilo la kujiuzulu.

Katika barua yake kwa Mhe. Rais Kikwete, Jaji Werema amesema kuwa ameomba kujiuzulu kwa sababu ushauri wake kuhusiana na suala ya Akaunti ya Tegeta Escrow hakueleweka na umechafua hali ya hewa.

Mhe. Rais Kikwete amemshukuru Jaji Werema kwa utumishi wake ulioongozwa na uaminifu na uadilifu.
 
Unaweza kusema viongozi tulionao hawapo kuwatumikia wananchi bali kujinufaisha wao wenyewe, ikitokea mmoja wao kashtukiwa na umma na kujiuzuru, wenzao humsifia na kumshukuru kwa utumishi bora na uadilifu.....Hapa, najisikia vibaya sana. iweje mtu aliyesababisha hasara kubwa kama kwenye mchezo wa ESCROW, anapojiuzuru anasifiwa kwa uadilifu? ni uadilifu upi hapo unaozungumzwa? kwanini hatujifunzi kwa wenzetu kusema ukweli, kama kaharibu aambiwe ukweli. nilitegemea kwa mtu kama AG anapojiuzuru, unakubali ila pia unamwambia anataka kuwajibika kwa matendo yake, na hii nizidi ya kuvua cheo pekee bali vyombo vingine vimchukulie hatua zaidi. kwa maoni yangu kusifiana wakati mtu katuingizia hasara, ni utamaduni usiofaa kabisa. tatizo letu tunaoneana aibu mno, au labda katika madili hayo wamepiga wote, sasa inakuwa vigumu kuwajibishana. THIS IS MY CONCLUSION, "YANAMWISHO HAYA"

Mapumbafu siku zote huwa yanasifiana hawajui kingine mtu barabara inatengezwa kwa kodi ya na deni bado unadaiwa halafu utashanga mijitu unashangilia na kusifiana sifa za kijinga wakati unakuta una deni mpaka kiumbe kilicho tumboni kinadaiwa kweli mzazi mrisishe mwanao elimu fuko la hela ujinga.
 
Bila kufunguliwa mashtaka kwa kuingizia hasara serikali na kuchafua taswira ya Taifa kimataifa, mamlaka ya uteuzi itakuwa bado haijafanya la maana.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Tatizo ni nini we mama,mbn unatoa povu. Jamaa kajiuzulu,issue ya kupongezwa haina maana kama hatua zaidi za kisheria hazitachukuliwa. Jamaa amekiri mwenyewe kwamba kajiuzulu kutokana na uzembe aliousababisha,kwa nini asiwajibishwe???
 
alishajiuzulu siku nyingi siku alipojiuzulu mle bungeni alisema hivi"Msimhukumu Maswi nihukumuni mimi yeye anlifuata maagizo yangu"Nilijua tu huyu yupo tayari kujiuzulu isipokuwa kuna masuala ya makubaliano flaniflani ili mambo flaniflani wayaweke sawa kwanza .Lengo asiwaathiri wenzake wenye lengo la kungangana na kufuta ushahidi flaniflani hata kiomgozi ajaye asikute mabaki.Alihisi pia uhatari kama wataondoka wote ghafla na maswi hali ingeharibika zaidi hivyo mmoja abaki a control mambo.
 
Kwa kweli kikwete anatufanya wa Tanzania kama mazuzu...huyu baba na amalize muda wake ajiondokee hatumtaki
 
Ahsanteni UKAWA,,,
SINTAMSAHAU KIKWETE MAISHANI...

DAH..!!

Ni chanzo cha yote haya.
 
Mwanasheria Mkuu wa Serikali ajiuzulu

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick
Werema amejiuzulu nafasi yake hiyo kuanzia
leo, Jumanne, Desemba 16, 2014 na Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amekubali
ombi hilo la kujiuzulu.

Katika barua yake kwa Mhe. Rais Kikwete,
Jaji Werema amesema kuwa ameomba
kujiuzulu kwa sababu ushauri wake kuhusiana
na suala ya Akaunti ya Tegeta Escrow
hakueleweka na umechafua hali ya hewa.

Mhe. Rais Kikwete amemshukuru Jaji Werema
kwa utumishi wake ulioongozwa na uaminifu
na uadilifu.

Na aombe radhi kwa kutukana wabunge kisha ashtakiwe...Muhongo yeye kavimba mpaka afukuzwe kama Yau!!
 
Mwizi wa kuku anauliwa. Je ukiiba billioni moja, unaweza kununua kuku wangapi wa wizi?
 
Nukuu "Peresedor kamshukuru jaji kwa utumishi wake ulioongozwa na UAMINIFU NA UADILIFU" mwisho wa kunukuu...

Asee haya mambo yanawezekana tz pekee, mean kuwa maelekezo yote yalitoka juu na kutafsirika tofauti, ki ukweli kuna viongozi walisha wafanya watz kama mashabiki wa ngoma...

Hyo kauli haikupaswa kutolewa na mkuu wa kaya kama yy, means anataka kutuambia kuwa asinge jiuzuru ikulu isingemuajibisha??

Tanzania bila ........ inawezekana.
 
Back
Top Bottom