Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Frederick Werema ajiuzulu

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema amejiuzulu nafasi yake hiyo kuanzia leo, Jumanne, Desemba 16, 2014 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amekubali ombi hilo la kujiuzulu.

Katika barua yake kwa Mhe. Rais Kikwete, Jaji Werema amesema kuwa ameomba kujiuzulu kwa sababu ushauri wake kuhusiana na suala ya Akaunti ya Tegeta Escrow hakueleweka na umechafua hali ya hewa.

Mhe. Rais Kikwete amemshukuru Jaji Werema kwa utumishi wake ulioongozwa na uaminifu na uadilifu.

Mwenye akili kasha jua, pimbi ni nani kati yake Chacha na yule mbunge huko mwisho wa reli.
 
Alikua muadilifu na muaminifu jamani,sasa JK,sijui ana maanisha nini hapo kwamba hajui haamini au anawaona watanzania kwa ni waapuzi sana,jitu limekwiba tena limeibia watanzania walio masikini leo unaliita eti ni kiongozi alie tukuka muadilifu na muaminifu kweli baba Riz,tumekuweka hapo magogoni utudhihaki na kutufanya wajinga.
 
.

Mhe. Rais Kikwete amemshukuru Jaji Werema kwa utumishi wake ulioongozwa na uaminifu na uadilifu.

Jamani,kweli huyu mtu anastahili sifa hizi wakati ametutia hasara?ningekuwa mimi ndio mwajiri wake,wala nisingemjibu
 
Asante kwa taarifa. Najiuliza maswali machache, yeyote mwenye majibu anaweza kunisaidia, tafadhali.
  • Inawezekana Kajiwahi ku-resign kabla hajawajibishwa na Rais au ni makubaliano yamefanywa ili aonekane ka-resign mwenyewe?
  • Kipindi chote tangu issue hiyo inaanza kuwa gumzo hadi report inasomwa bungeni na yeye na Muhongo wakiwa wanatetea na kusema ni uongo, alikuwa hajagundua kwamba ushauri wake umechafua hali ya hewa hadi leo ndo kagundua?
  • Kwa vile sasa kagundua kosa, inawezekana ukawa wakati mzuri sasa wa kumwomba radhi kafulila kwa matusi aliyomtolea na hata ikiwezekana akaomba radhi bunge zima? (yeyote anayemfahamu vizuri kwa tabia anaweza kunijibu hili)
  • Kwa vile yeye ni mwanasheria kitaaluma, anaweza kuliambia taifa, kutokana na kosa lake la "ushauri wake kuchafua hali ya hewa" katika sheria za nchi, ni adhabu gani anayopaswa kupewa?
 
Nani Tumbiliiii? chezea wanamageuzi UKAWA ni noma tutawakumbuka kwa mengi sana katika historia ya siasa ya Tanzania
 
Mwenye akili kasha jua, pimbi ni nani kati yake Chacha na yule mbunge huko mwisho wa reli.

Mkuu sahihisho, sio pimbi ni "tumbili". Huyu kijana Kafulila inabidi awe makini la sivyo mafisadi walioguswa watamtanguliza kuzimu kabla hajafaidi ndoa yake.

Tiba
 
Alikua muadilifu na muaminifu jamani,sasa JK,sijui ana maanisha nini hapo kwamba hajui haamini au anawaona watanzania kwa ni waapuzi sana,jitu limekwiba tena limeibia watanzania walio masikini leo unaliita eti ni kiongozi alie tukuka muadilifu na muaminifu kweli baba Riz,tumekuweka hapo magogoni utudhihaki na kutufanya wajinga.
mwache,ameanza kuona rasharasha kwenye uchaguzi wa Serkali za mitaa.ngoja akimalizie chama tu
 
Unajiita Jaji,AG na Msomi alafu unajidhalilisha kwa kushiriki wizi na wanasiasa wezi hata kama ni Boss wako! Yule AG wa Zanzibar ataendelea kuheshimiwa siku zote siyo huyu mwizi wa pesa za umma aliye shiriki kuchakachua maoni ya Watanzania ktk BMK. Siku zaja yeye na walio mtuma kutuibia na kuchakachua maoni yetu tutawafanyia kitu mbaya!
 
Hvi unadhani CAG kuna baya alilolifanya kwa JK? Kila alichokifanya alifanya kwa matakwa ya JK hata hilo la Escrow. Ndio maana anaambiwa alikuwa maminifu na mtiifu. Kumtosa ni vile tu imebidi. Utamsikia akimsifu hata mpuuzi kama Muhongo na Maswi.
 
Huyu bwana alilewa madaraka, mahaba na chama tawala yakamtia upofu hakupata tambua dhamana na cheo alicho nacho ni kwa ajili ya watanzania wote bila kujali chama. Nampa pole na hongera kwa maamuzi magumu kwani madaraka ni matamu.
 
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema amejiuzulu nafasi yake hiyo kuanzia leo, Jumanne, Desemba 16, 2014 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amekubali ombi hilo la kujiuzulu.

Katika barua yake kwa Mhe. Rais Kikwete, Jaji Werema amesema kuwa ameomba kujiuzulu kwa sababu ushauri wake kuhusiana na suala ya Akaunti ya Tegeta Escrow hakueleweka na umechafua hali ya hewa.

Mhe. Rais Kikwete amemshukuru Jaji Werema kwa utumishi wake ulioongozwa na uaminifu na uadilifu.

Muhongo vipi? anasubiria nini? ama anavuta vuta mda uluwa mtamu
 
Hvi unadhani CAG kuna baya alilolifanya kwa JK? Kila alichokifanya alifanya kwa matakwa ya JK hata hilo la Escrow. Ndio maana anaambiwa alikuwa maminifu na mtiifu. Kumtosa ni vile tu imebidi. Utamsikia akimsifu hata mpuuzi kama Muhongo na Maswi.

Mkuu you have said it all. Anasifiwa kwa kuwa ushauri wake ilikuwa ni baada ya kupokea maelekezo kutoka magogoni.

Shame on them.

Tiba
 
Back
Top Bottom