Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Frederick Werema ajiuzulu

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Frederick Werema ajiuzulu

U..DPP tu ulikua ni sheeedah

Alikua anatupiana mpira na takukuro kuhusu kesi za ufisadi

Akiwa ag atatupiana mpira na PM...
Feleshi sidhani kama atakubali tena kuja kwa mwanasheria mkuu, kwasababu amefanya kazi ktk mazingira magumu sana, na amini usiamini, KIKWETE AMEKUJA KUKIRI KUWA ALIKUWA MISLED KUMWONDOA, amegundua hilo baadaye akajua kuwa yote yalikuwa majungu matupu.

Feleshi alifanya kazi akichukiwa kwa asilimia 100% na Werema na Masaju waliokuwa wanataka kuingiza mambo yao na yeye akawa anashikilia msimamo.

Feleshi amefanya kazi kwa misukosuko na Dr. Hosea ambaye muda wote alikuwa anapeleka ushahidi hafifu kwa dpp ili kunawa mikono wakati kesi ameiharibu asilimia mia. ujue kesi inajengwa na wapelelezi, bila upelelezi hakuna kesi, hivyo pccb wakiharibu ushahidi dpp atapoteza pesa za serikali kushikilia kesi ambayo yeye hakusanyi ushahidi na anaona imepotoshwa. pccb kwa maslahi yao wamekuwa wakila rushwa na watuhumiwa hata mafisadi, halafu wanaleta ushahidi hafifu ili mafisadi wakatokee mbele. ushahidi wa mambo haya ni kesi ya IDI SIMBA NA KINA ROBERT KISENA WA SIMON GROUP a.k.a sakata la UDA.

baada ya kumteua kuwa jeji, taasisi karibia zote za serikali zilisusia, taasisi za nje ya nchi zikamtaka arudishwe, mambo yalivurugika kwasababu dpp alikuwa anafanya kazi zaidi hata ya boss wake werema na masaju, kilichotokea kikwete aliomba arudi tu afanye kazi kama dpp wakati jaji kama tu werema anavyofanya kazi kama AG wakati ni jaji, feleshi akakataa.

wafanyakazi wa hiyo ofisi ndio wanaojua kilichopo, aliyeijenga ofisi hii ni FELESHI, na ndiye anayeijua kuliko wote. mwenye uwezo kichwani, namwenye uwezo wa kuchukua maamuzi magumu ni feleshi.

kwa taarifa yako, kikwete alikuwa mislead kuwa kwa misimamo ya Feleshi ccm itashindwa kushughulikia upinzani mwakani, wakataka kumtoa mapema ili wamuweke mtu atakayetumika. walipokuja kutafuta nani atareplace wakakosa kabisa atakayefit kama alivyokuwa feleshi, mashirika ya kimataifa yakagoma, polisi walishagoma kutoa ushirikiano. werema na kundi lake wakawa wameweka pandikizi lao yule mlarushwa ANSLEM MWAMPOMA ili amsumbue na kumharibia wakifikiri feleshi akitoka yeye ndiye atashika nchi, aliishia kukaimu tu wala hajawa dpp, na aliyepewa udpp ni dogo aliyempokea kazini.

mnachotakiwa kujua, hakuna dpp atakayefit nafasi ya feleshi. kikwete kati ya vitu alivyowahi kupotezwa na hosea, masaju na werema, ni kumtosa feleshi kwa bifu lao la kuona feleshi anakubalika kuliko wao.

hata hivyo, sidhani kama feleshi atakuja kukubali kurudi tena kwenye ofisi ya mwanasheria mkuu, alikokuwa jaji huko anapumsika kwasababu kile kitu alichokuwa amekalia ni kugumu kuliko hata urais, kiti ambacho rais analeta yake, hosea analeta yake, mawaziri wanaleta yake na wewe unatakiwa kuchukua maamuzi magumu...ni nafasi ya hatari na ngumu ambayo kwa yale aliyoyafanya lazima apongezwe. hosea, werema na masaju Mungu atawaengua wenyewe. nilishawahi fanya kazi kwenye hiyo ofisi, ninawajua a-z, na ninamjua feleshi pia.
 
Mimi ninayemshangaa ni waziri wa nishati na madini prof. sospeter muhongo yeye ndo anatumia baadhi ya watu kulazimisha kujisafisha. si jambo zuri kidogo yule prof. anahitaji kujitambua kuwa amerisababishia. hasara taifa kwa wizi huo na yeye amenukuliwa akitetea na kuratibu vikao vya kuidhinisha uchotwaji wa fedha hizo. pamoja na kwamba ameonakana ni msomi muhimu lakini kwa mchezo wa siasa ya Tanzania nawahakikishia watanzania kama wataweka imani kwa muhongo tutarajie wizi mkubwa sana kupitia gesi na mafuta. Binafsi ni bora awajibike kwa makosa yake. Tunawasomi wengi sana si lazima tumtegemee yeye kwanza anakibuli sana.
 
aliye staafu anaweza kujiuzuru kweli? au watanzania woote ni wajinga kiasi hicho?
 
NA RAIS NI MWIZI

ILIBIDI ACHUKUE HATUA YA KUKATAA OMBI LAKE KAMA ALIVYOFANYA KWA BALALI THEN AKAFANYE MAAMUZI YA KUMFUKUZA NA KUMFIKISHA MAHAKAMANI


TUNA RAISI LEGELEGE sijawai kuona
Amekuzaa na kukulea halafu leo ndiyo unajifanya kumbeza kumbuka bila yeye huwezi kula story hii mzazi wako wa kike anaijua vema muulize.
 
Werema sio tu kwamba amechafua hali ya hewa, yeye ni mshiriki wa ufisadi and should be jailed

I hope taratibu zote za kumfungulia mashtaka zitakamilik

Siasa mbaya sana, Juzi aliita watu tumbiri, leo yuko uraiani na tumbiri wenzake
Kama mimi tumbili wewe ni mwizi.. kafulila...
 
Amekuzaa na kukulea halafu leo ndiyo unajifanya kumbeza kumbuka bila yeye huwezi kula story hii mzazi wako wa kike anaijua vema muulize.

Na hakika hii ni id yako nyingine.....kwa maneno hayo ndio kweli unataka tukupe nchi......
 
Huyu hafai kabisa. Ni bora kumweka Simbachawene. Nasikia naye ni mwanasheria.
simba cha wene sio mwanasheria, hajui kitu, alisoma open university sheria, hajawahi kupractice, hajui system na utendaji wa ofisi hiyo, kwenye ofisi hiyo unatakiwa kumweka mtu ambaye alishafanya kazi kwenye ofisi hiyo na anajua ofisi inavyofanya kazi, sio kumleta kila mtu tu. la sivyo, mtajuta.
 
... Nasikia Werema Alistaafu Tangu Novemba, Hili Ni Changa La Macho
 
Mengi naye katoa taarifa kwa vyombo vya habari kukanusha kuhusishwa kwako kuhonga wabunge ili waunge mkono taarifa ya PAC, mwenye access atupie humu
 
simba cha wene sio mwanasheria, hajui kitu, alisoma open university sheria, hajawahi kupractice, hajui system na utendaji wa ofisi hiyo, kwenye ofisi hiyo unatakiwa kumweka mtu ambaye alishafanya kazi kwenye ofisi hiyo na anajua ofisi inavyofanya kazi, sio kumleta kila mtu tu. la sivyo, mtajuta.

chuki chuki chuki tuuuu
 
Ndugu zangu watanzania,tusiwe wajinga na kugeuzwa watoto wadogo wanaodanganywa na pipi,hebu tijiulize,kujiudhiru tu inatosha kuwajibika juu ya upotevu wa mabilioni ya pesa!!?au ndio tunampa muda wakwenda kuzitumia vizuri hizo pesa.!!
TANZANIA TANZANIA naipenda nchi yangu ila sipendi viongozi wake!!!
 
Back
Top Bottom