Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Frederick Werema ajiuzulu

Vipi sasa rais anamshukuru kwa uaminifu na uadilifu wakati anakabiliwa na mashtaka ya matumizi mabaya ya offisi na rushwa?
 
Wanataka watu wahache kuzungumzia kipigo Uchaguzi Serikali za Mitaa. Sikio la kufa, kesho utaona TD ataibuka na kusema ripoti inaonesha chanzo kilikuwa AG, naye amejiuzuru... mwakani tunakaba hadi penati, hakuna pingamizi wala kupita bila kupingwa! Mxuuuuu
 
Mengi naye katoa taarifa kwa vyombo vya habari kukanusha kuhusishwa kwako kuhonga wabunge ili waunge mkono taarifa ya PAC, mwenye access atupie humu
Mengi aache ujinga tunajua yote alivyokuwa anahonga wabunge wamshinikize muhongo aondoke ili apate vitaru vya gesi vya bure.
 
Too shame hana shida yeye ilibidi hawe wafundisho wajao watakua na heshima lakin too much wameiba sana tushirikiane kutokomeza janga la taifa ccccmm.
 
hii serikali imepoteza dira maana kila kiongozi anayekumbwa na kashwa hakisha jiuzulu kuna kuwa hakuna kesi tena zaidi ya kula pensheni yake tu mpk mwisho, kwahiyo inabidi wabunge wapeleke hoja ya kushtakiwa kwa watuhumiwa wote wanaokutwa na kashifa zinazoipelekea serikali kuchafuriwa
 
Mkuu......rekebisha basi kichwa cha habari kisomeke.........KUJIUZULU NDIO SULUHISHO ?.........kujiudhuru inasogea kwenye maana nyingine tena......
 
watanzania tunadanganyika haraka mno! kuna uzi ulielezea kuwa. muda ws AG wa kustafu ilishapita! hivyo kuambia kuwa AG amejiulu tusifikili amewajibika. muda wake kisheria ulishaisha.sioni cha kufurahia hapa! nimwendelezo wa uhuni wa viongozi wetu!
 
Maneno ya MH Kikwete yanathibitisha hisia zangu za siku nyingi kwamba kipimo cha maadili Tanzania kimeshuka na kuzorota sana kiasi kwamba Jizi na babaishaji linapewa sifa za uadilifu.
Mwongo anaitwa mwadilifu
Mwizi anaitwa mwadilifu
Mzugaji na mababaishaj mkuu anaitwa mwadilifu.
Mwishoni akibanwa sana utasikia wapambe wa MH Rais wanasema alinukuliwa vibaya au alishauriwa vibaya.

Maneno yamtokayo mtu mdomoni ni sehemu ya hitimisho la mawazo yake yote kuhusiana na mada.
Hakuna kinywa kiwezacho kunena makuu kuliko ukuu wa akili yake.

Sijui MH Rais Kikwete anawaza nini kichwani kwake kuhusu account ya Escrow,lakini kwa mtaji wa maneno haya siamini hata kidogo kwamba kuna chochote cha maana kinachoendelea kichwani mwake.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema amejiuzulu nafasi yake hiyo kuanzia leo, Jumanne, Desemba 16, 2014 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amekubali ombi hilo la kujiuzulu.

Katika barua yake kwa Mhe. Rais Kikwete, Jaji Werema amesema kuwa ameomba kujiuzulu kwa sababu ushauri wake kuhusiana na suala ya Akaunti ya Tegeta Escrow hakueleweka na umechafua hali ya hewa.

Mhe. Rais Kikwete amemshukuru Jaji Werema kwa utumishi wake ulioongozwa na uaminifu na uadilifu.
 
Sasa kama aljua ameharbu hali ya hewa kwnn asingejiuzuru mapema, au ndio ionekane hajafukuzwa. Lazma afilisiwe tu
 
Sahoihisho dogo la lugha.

Kujiudhuru na kujiuzulu ni vitu viwili tofauti.

Kujiudhuru ni kuomba udhuru. Kuomba kusamehewa kwenye wajibu fulani, to ask to be excused. Kwa mfano, mchungaji alijiudhuru kutofika kanisani Jumapili hii kutokana na maradhi.

Kujiuzulu ni kuacha kazi kwa matakwa binafsi. Kwa mfano, Ali hassan Mwinyi alijiuzulu Uwaziri wa Mambo ya Ndani baada ya kinamama kuuawa Shinyanga kwa kukisiwa kuwa wachawi.

Werema hakujiudhuru, amejiuzulu.
 
Back
Top Bottom