Kwa kuwa ni mwanaume nitakuambia jambo hili ulizingatie sana maana utakuwa mzazi pia. Umesema dada yenu anaongea sana na baba yenu kuliko nyinyi, unafikiri kwa nini? Kuna uwezekano mkubwa pia dada yenu hayuko huru sana kuongea na mama yenu kuliko baba. Na huenda mama anamlalamikia dada yenu kumshirikisha mambo yake badala ya ya yeye mama.
Iko hivi, siku zote baba hujikuta katika upendo kwa mtoto wa kike na mama kwa mtoto wa kiume kutokana na matarajio ya wazazi yenye nia njema kwa watoto wao.
Baba siku zote anataka mtoto wake wa kiume awe mwanaume kweli anayetegemeka, jasiri, shupavu, mwenye msimamo thabiti na ikiwezekana afuate nyayo zake hata kumpita. Hilo ndio tarajio la baba yeyote, hivyo ukilegalega utakula makofi, ngumi, makofi ili kukuweka sawa. Na sehemu utakayopata kitulizo ni kwa mama na ndio sababu watoto wa kiume wengi ni watoto wa mama mpaka uzeeni. Wanahisi baba hakuwahi kuwapenda ila mama aliwapenda zaidi kitu ambacho kumbe sivyo.
Vivyo hivyo kwa watoto wa kike. Siku zote mama anataka binti yake awe mwanamke wa ukweli kama yeye akifanya uzembe anakula miko, anatandikwa na bakuli. Na mtu anayembembeleza ni baba hali inayopelekea kuwe na bond kubwa kati ya baba na binti kuliko binti na mama. Na ndio maana binti hata akiolewa mtu anayemsikiliza zaidi ni baba yake na ukikutana na mwanamke anayependwa sana na baba yake na kwao wana uwezo mwanaume utapata shida.
Jaribu kukumbuka wewe mwenyewe nini kilikufanya usiwe karibu na baba? Kwa kuwa ni mtu mzima uanaweza kutafakari yote aliyokuwa anakufanyia ilikuwa kwa nia njema au mbaya? Na umeshasema baba ana sifa ya ukimya hivyo yawezekana mengine ulimfukiria tofauti na alivyo moyoni. Mpende baba yako, ongea naye, muulize wanaendeleaje yeye na mama, muulize kuhusu shuguli zake, mpe hela ya soda au chochote anachotumia, mpe mipango yako ya maisha kisha msikilize atasemaje. Usidharau maoni yake hata kama mnatofautiana kimtazamo kwa baadhi ya mambo. Na huenda akakwambia mambo mengi ambayo huyajui kuhusu familia yenu yatakayokusaidia hata siku akitoweka duniani.