Mwanangu hataki kuongea nami, nafanyaje?

Baba yangu ni mkimya sana na mama yangu ni mcheshi sana na hii karithisha watoto wake wote hakuna mtu mkimya kwetu.

Ukimya wa baba haujamfanya aishi maisha ya upweke kwa wanae, tunamuelewa na tunaishi nae vile alivyo, ni mtu anayefurahi sana mtoto wake akimfata na kumwambia jambo au kumuomba ushauri hata kama wa kijinga yeye atajali na atasaidia.

Baba alikua mtu wa pili (kumtoa my bro) kumwambia kua "i am a lesbian" aliniangalia na kutabasamu kisha akasema "jembe langu fanya kile kinachokupa furaha as long as huumizi mtu".

Nirudi kwa mtoa mada, ushajua baba yako ni mkimya basi anza mazoea ya kumshirikisha katika vitu vyako na kumtaka shauri mbali mbali, sahau yaliyopita nyuma jenga sasa ushakua mtu mzima ambapo soon utakua na family yako na wewe utakua unaangaliwa.
 
Makubwa..pole sana.
Mimi najua kwenu wadada zinakua zinaiva sana na wababa kuliko mama..kwa mfano sisi tu nashindwa kuongea na baba ila wadogo zetu wa kike wanampelekesha wanavyoweza na anawadekeza. Ila sie wanaume ndio hatuko huko.

Je chanzo cha hayo yote ni nini..?
Hiyo ni kati yangu na babangu! Na hawezi kunilaumu kwa hilo
 
Moja ya kitu nachopenda kutoka kwako u so real.. Unajiamini na unachokifanya, Hongeraa sana.
Ndio mkuu nimeamua ku pay price yoyote itakayo hitajika ili kuimarisha mahusiano
 
Makubwa..pole sana.
Mimi najua kwenu wadada zinakua zinaiva sana na wababa kuliko mama..kwa mfano sisi tu nashindwa kuongea na baba ila wadogo zetu wa kike wanampelekesha wanavyoweza na anawadekeza. Ila sie wanaume ndio hatuko huko.

Je chanzo cha hayo yote ni nini..?
Badili mindset yako kwanza
 
Pole sana Mkuu!
Siku zote huwa tunavuna tuliyoyapanda! Mimi sio wa kulaumiwa kwa hilo kabisaa
Yaani nimevaa hivyo viatu vya baba sakayo..daah🤦‍♂️ sikulaumu wewe ila nimeumia sana mwanangu!
Usinilipie hivi mwanangu, mimi ni baba yako hata kama sikuwa rafiki kwako lakin nia yangu ilikua kukujenga ili uweze kusimama kama unvyosimama hivyo leo, na ninaona fahari kuwa na binti wa aina yako labda kwa sabb niliyafanya hayo yote nyuma ya pazia mbele nikimtanguliza mama yako, nikumbuke tu mwanangu ni faraja sana kwangu usione sisemi!1
 
Yaani nimevaa hivyo viatu vya baba sakayo..daah[emoji2357] sikulaumu wewe ila nimeumia sana mwanangu!
Usinilipie hivi mwanangu, mimi ni baba yako hata kama sikuwa rafiki kwako lakin nia yangu ilikua kukujenga ili uweze kusimama kama unvyosimama hivyo leo, na ninaona fahari kuwa na binti wa aina yako labda kwa sabb niliyafanya hayo yote nyuma ya pazia mbele nikimtanguliza mama yako, nikumbuke tu mwanangu ni faraja sana kwangu usione sisemi!1
Baba
Ungejua namna ninavyokupenda, ungemshukuru Mungu kwa namna nilivyo. Nilishakusamehe babangu, siku uliyoongea na mimi kwa uchungu niliachilia uchungu wote kwenye kifua changu!

Nilikuwa nakuombea kila siku, uwe kama babake fulani, sema umechelewa kubadilika!
 
Sio ajabu
wanaume wengi ni watoto wa mama hata kwetu wapo, Humu Jf ndio wamejaa kule kwa mama vs Mke...
Btw baba ako ameumia kibinaadamu mtu mpaka akwambie hivyo ameumia jaribu kumpa hata Hi salamu haigombwi mkuu, ukimya kwa wanafamilia sio kwenu tu hata kwetu upo hatusemeshani tena naona kwenu bora sisi ndio hatuonani miaka na siku tukionana ni salamu basi unaweza sema sio ndugu, kwasababu hatukulelewa ivyo. Anza kunpigia simu mzee mara 1 moja , piga story hata kama hazina maana hata dakika 5 tu naamini moyo wake utafurahi, tusielemee upande mmoja tu wote ni wazazi. Utakua baba na wewe utaona inavyonoga kutengwa na uache tabia ya kwenda kukaa na mama jikoni Mboga itanukia ndevu
 
Baba yangu ni mkimya sana na mama yangu ni mcheshi sana na hii karithisha watoto wake wote hakuna mtu mkimya kwetu.

Ukimya wa baba haujamfanya aishi maisha ya upweke kwa wanae, tunamuelewa na tunaishi nae vile alivyo, ni mtu anayefurahi sana mtoto wake akimfata na kumwambia jambo au kumuomba ushauri hata kama wa kijinga yeye atajali na atasaidia.

Baba alikua mtu wa pili (kumtoa my bro) kumwambia kua "i am a lesbian" aliniangalia na kutabasamu kisha akasema "jembe langu fanya kile kinachokupa furaha as long as huumizi mtu".

Nirudi kwa mtoa mada, ushajua baba yako ni mkimya basi anza mazoea ya kumshirikisha katika vitu vyako na kumtaka shauri mbali mbali, sahau yaliyopita nyuma jenga sasa ushakua mtu mzima ambapo soon utakua na family yako na wewe utakua unaangaliwa.
Shkamoo dada
 
Baba
Ungejua namna ninavyokupenda, ungemshukuru Mungu kwa namna nilivyo. Nilishakusamehe babangu, siku uliyoongea na mimi kwa uchungu niliachilia uchungu wote kwenye kifua changu!

Nilikuwa nakuombea kila siku, uwe kama babake fulani, sema umechelewa kubadilika!
Asante kwa kunipenda mwanangu Sakayo, nitazidi kukuombea kwa Mungu uwe bora zaidi, ni kweli wazazi wa enzi zetu tumeshachelewa mengi katika malezi ambayo leo hii yanatuumiza wenyewe lakini hamna budi kutusamehe wazaz wenu na kutuchukulia kwa kiasi, faraja pekee niliyonayo wakati huu ni mama yako na wewe unajua hilo.... Asante kwa kunikumbka nafurahi sana naposikia salamu zako kutoka kwa mama yako lakini unapopigia moja kwa moja kwangu hata marra chache Moyo wangu unaona fahari na furaha isiyo kifanii..
Mungu aendelee kukutunza mwanangu Sakayo !!
 
Sio ajabu
wanaume wengi ni watoto wa mama hata kwetu wapo, Humu Jf ndio wamejaa kule kwa mama vs Mke...
Btw baba ako ameumia kibinaadamu mtu mpaka akwambie hivyo ameumia jaribu kumpa hata Hi salamu haigombwi mkuu, ukimya kwa wanafamilia sio kwenu tu hata kwetu upo hatusemeshani tena naona kwenu bora sisi ndio hatuonani miaka na siku tukionana ni salamu basi unaweza sema sio ndugu, kwasababu hatukulelewa ivyo. Anza kunpigia simu mzee mara 1 moja , piga story hata kama hazina maana hata dakika 5 tu naamini moyo wake utafurahi, tusielemee upande mmoja tu wote ni wazazi. Utakua baba na wewe utaona inavyonoga kutengwa na uache tabia ya kwenda kukaa na mama jikoni Mboga itanukia ndevu
Hahaaaaaaaa siwezi acha kukaa na mama..popote alipo nikiona nataka kuongea nae namfuata tuongee..kwanza napenda wakati anapika mm namsaidia kusogeza vitu.!
Jitahidi mkuu mdumishe mahusiano.. ngoja nimpigie leo tuongee kidogo
 
Usijilazimishe lakini mkuu kama moyo wako hautaki
Ngoja tu miaka ijayo utaona mavuno ya unachokipanda.. wakati huo wanao ndio wanafanya mara2 ya haya
 
Asante kwa kunipenda mwanangu Sakayo, nitazidi kukuombea kwa Mungu uwe bora zaidi, ni kweli wazazi wa enzi zetu tumeshachelewa mengi katika malezi ambayo leo hii yanatuumiza wenyewe lakini hamna budi kutusamehe wazaz wenu na kutuchukulia kwa kiasi, faraja pekee niliyonayo wakati huu ni mama yako na wewe unajua hilo.... Asante kwa kunikumbka nafurahi sana naposikia salamu zako kutoka kwa mama yako lakini unapopigia moja kwa moja kwangu hata marra chache Moyo wangu unaona fahari na furaha isiyo kifanii..
Mungu aendelee kukutunza mwanangu Sakayo !!
Mungu atutunze sote jamani baba!
Nisamehe mimi baba, najua mekuumiza kukutupia salamu! Nitajitahidi kurekebisha hilo babangu!
 
Morning. Naombeni ushauri wenu kidogo wakuu..

Mimi ni kijana first born kwenye familia ya watoto 5. Wanaonifuata ni vijana walio juu ya miaka 18 mmoja wa kiume anaenifuata na wa kike. Huyu wa kiume anaishi Tanga na wa kike yupo kwa wazazi, mimi niko Northland.

Tuna wazazi wote wawili vijana kiasi (Hawajafika 50). Juzi nilikuwa namtafuta kwa simu my mom nikawa simpati ikabidi nimtext dingii "Ukiwa karibu na mama nipige nataka niongee nae maana simu yake hapokei" (ana mtindo wa kuacha simu jikon au chumbani).Dingii hata hakunipigia!

Baadae akanipigia akaanza kunilalamikia sana, anasema kuwa kwanini kila mkipiga simu hamuongei na mimi? Mnaongea na mama yenu tu! Kwani mimi niliwakosea nini? Au mimi sina umuhimu kwenu? Niliduwaa!!

Mimi nikajitetea kuwa kuna vitu nilikuwa nataka nimwambie mama kuhusu mimi.. akashika hapo hapo tena kwa kusema..kwa hiyo kuna vitu mpo tayari kumshirikisha mama yako mimi haupo tayari? Nikasema kuwa sikuona umuhimu wa kukuambia wewe jambo dogo kama hili ila ikifika muda nitakuambia. Aliongea sana kwanini tunamfanyia vile. Akakata simu!

Maneno ya dingii yaliniumiza kiasi yakafanya nimuonee huruma maana alikuwa anazungumza ukweli, huwa siongei nae kitu zaidi ya salamu then naongea na mama mpaka basi.Nakumbuka kipindi fulani nilikuwa naongea na rafiki yake dingii akaniambia eti mimi ni mtoto wa mama nampenda mama yangu tu nikamjibu ndio mimi ni mtoto wa mama sababunimezaliwa na mama alafu watoto wa kiume huwa tunapenda wazazi wa kike.

Hilo likapita nikachukulia poa ila hili la sasa ni serious.Mwanzo nilijua kuwa ni mimi tu ndio huwa naongea na mama pekee kumbe hata huyu jamaa wa Tanga huwa haongei na baba kabisa anaongea na mama tu. Baba analalamika pia kuwa hataki kuongea nae.

Chanzo cha tatizo:

Japo baba sio mzee ila ni kijana mwenye misimamo ya kizee. Ni ile aina ya wazazi wanaoona kuwa mtoto inatakiwa amuogope baba. Kubwa zaidi huwa ni mtu mkimya mno (ndio katuambukiza watoto ukimya hasa mimi na dogo). Huwa tukiwa ndani ni shikamoo tu ndio zinatembea tu no stori maana hakuna wa kumsemesha mwenzie..Nitaongea stori gani na baba wakati namuogopa, ni mkimya na mimi mkimya, ni mkali? Napiga kimya tu.

Ukiangalia kwa makini utajua ni malezi aliyotujengea ndio yamefanya tushindwe kuongea nae (Japo mimi nimeishi nae nyumba moja kwa miaka 4 tu) sasa wanae wamekuwa vijana anaona wanamtenga watoto wote wanampenda mama so anajisikia vibaya na upweke hakuna kibaya kama kukataliwa na familia yako mwenyewe.

Pia mimi na huyu dogo wa Tanga hatunaga stori kabisa huwa tunajuliana hali tu kwa simu. Kama tukiwa home pamoja tunakuwa kimya tu maana hakuna cha kuongea wote tuna asili ya ukimya. Ni salamu tu hata tukiwa tunaenda sehemu pamoja huwa tupo kimya no stori. Maana family conversation it wasn't applied to our family. Labda mama awe pamoja na sisi ndio tunaongea mno. Mimi nikiwa home nashinda zangu jikoni na mama stori tu mwanzo mwisho maana ndio kiumbe niliyemzoea zaidi duniani.

Ila kwa yule wa kike yeye tunaongea vizuri sana laafu yeye hana asili ya ukimya! Hata baba yake anaongea nae mno kuliko sisi.

Wakuu ambao ni wazazi tujifunze kuongea na wanetu vizuri yasije yakawakuta haya mambo. Ishi na watoto zenu kama marafiki. Wazazi wa kike wana win mioyo ya watoto ajili wao ni watu waelewa na wapole kwa watoto wao.

Msaada:
Nataka nijizoeshe kuwa naongea na father kila wiki hata kama sina shida nimpigie. Sasa naombeni mnishauri jinsi ya kuanza kupiga nae stori, stori gani niwe naongea nae? Mimi sio muongeaji mzuri.

Thanks
~Vers
Utakuwa mlevi acha
 
Usijilazimishe lakini mkuu kama moyo wako hautaki
Ngoja tu miaka ijayo utaona mavuno ya unachokipanda.. wakati huo wanao ndio wanafanya mara2 ya haya
Mamii nimejipanga kuwa baba bora ambae ahjawahi kuwepo.. najifunza makosa ya walio tulea.. Nimesomea Psychology, nasoma sana vitabu vya mambo ya makuzi na malezi najitahidi kujianda kuwa baba mzuri huko mbeleni
 
Back
Top Bottom