Kweli tumetofautiana! Mimi baba kafariki nikiwa na miaka nane, ila alikuwa anapenda sana kuongea na watoto wake hata ambao wako mbali na sisi wa karibu pia.
Nikikumbuka kwa mfano tukiwa tupo bila mama labda tukapita sehemu tukapishana na msichana ambaye yupo rika la brother anamtania "vp huoni mzigo huo mwanangu" sasa wewe mdogo ukijichanganya ukaenda kumwambia mama, wanakukana wote kwamba hawawezi kuongea jambo hilo mbele ya mtoto. Na kama mkitembea wote pamoja baba na mama, ule utani anakuwa haongei tena.